Kwanza kabisa, wakuu
hongereni kwa sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar!
Pili, nitangulize samahani iwapo nita-sound vibaya kwa baadhi yetu
kwani binadamu tumeumbwa tukiwa na mitazamo tofauti ktk masuala
mbalimbali.
Leo nazungumzia juu ya MICHANGO YA HARUSI, hasa za siku hizi, nalisema
hili bila kumung'unya maneno, utakuta mtu yuko Lindi, na wewe uko
Mwanza, anadai kakuweka kwenye kamati kuu ya harusi yake na hivyo
kadirio la chini utapaswa kuchangia Tsh. 100,000 na itakubidi uhudhurie
sherehe hizo Lindi ukitokea Mwanza! Piga picha, utakuta mtu mwenyewe
ulikutana nae Advanced Level miaka minane iliyopita na wala haujakutana
nae tena zaidi ya kuongea naye kwa simu kwa interval ya mara moja kwa
mwaka huku mkikumbushiana yalopita!
Harusi imekaribia utapokea sms mara tano kwa kutwa unakumbushiwa juu ya
mchango wako! Usipotoa atanuuuuuna, atakuseeeeema.....! Hii imekaaje
wakuu?
Naomba kuwasilisha.
ndoa za dharura hazina guarrantee.endelea kuweka hazina dada yangu nikiwe SebekoMee too inanikera xana nina kadi 4 za workmates wanasema najiwekea hazina ya wachangiaji kwenye harusi yangu while marriage is not on my life plan list
Single 5,000 na double 10,000/. ok tutakuleteajamani nina olewa mwezi wa nane naombeni mnichangie msinichanganye hapa wala nini!! mbona ulabu mnapiga kama kawa.
Nafikiri tuwashauri watu wawe wanafungia ndoa kwa KAKOBE.'Mmmmm! Leo imeletwa ya pili zote hela
Kwanza kabisa, wakuu hongereni kwa sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar! Pili, nitangulize samahani iwapo nita-sound vibaya kwa baadhi yetu kwani binadamu tumeumbwa tukiwa na mitazamo tofauti ktk masuala mbalimbali.
Leo nazungumzia juu ya MICHANGO YA HARUSI, hasa za siku hizi, nalisema hili bila kumung'unya maneno, utakuta mtu yuko Lindi, na wewe uko Mwanza, anadai kakuweka kwenye kamati kuu ya harusi yake na hivyo kadirio la chini utapaswa kuchangia Tsh. 100,000 na itakubidi uhudhurie sherehe hizo Lindi ukitokea Mwanza! Piga picha, utakuta mtu mwenyewe ulikutana nae Advanced Level miaka minane iliyopita na wala haujakutana nae tena zaidi ya kuongea naye kwa simu kwa interval ya mara moja kwa mwaka huku mkikumbushiana yalopita!
Harusi imekaribia utapokea sms mara tano kwa kutwa unakumbushiwa juu ya mchango wako! Usipotoa atanuuuuuna, atakuseeeeema.....! Hii imekaaje wakuu?
Naomba kuwasilisha.
Umeandika unasema bila kumung'unya maneno hapa JF.
Wanaokuomba michango nao unawaambia hivyo hivyo bila kumung'unya maneno kwamba michango yao ni kero?
Ulalamishi kwa mambo uliyo na ufumbuzi mwenyewe nao ni kero vilevile, hususan kwa sababu mpango mzima wa kusema bila kumung'unya maneno unaufahamu.
Hahaha. Umenikumbusha i met a total stranger in a training. Siku ya pili tu anasema kaunguliwa nyumba huko alikotoka. Ati anataka kupitisha mchango! Nikauliza ni mchango wa kurepair nyumba ama! Manake nyumba imeungua vibaya sana. Nilimueleza wazi mchango wangu ni wa hali. Ukihitaji mtu wa kuongea nae im here! Urafiki wa siku 2 hautoshi kuchangiana majanga, wanahusika mnaokula nao raha daily! Nahisi aliniona mchawi japo wengine walimchangia alfu kumi kumi!
Daadek kauzu zaidi ya dagaa!!
Wasiochangia hiyo kitu ni wengi sana, ungana nao! Kiukweli inabore. Najuta kwanini nilichangisha watu wakati naoa vinginevyo ningekuwa mmoja wao wasiochangia.
Vinginevyo tukubali kuwa sisi si mali yetu wenyewe, tu mali ya jamii tunazozichangia ktk mambo mbali mbali likiwemo Hilo la harusi na send off.
Hehehe. Mie siku hizi za uso tu! Mambo ya kugugumia maumivu staki. Ofisini nilishawaambia mambo ya kuchangiana hadi mume wa binamu wa cousin wake shangazi staki! Na mie sichangishi mtu. Kuna mijitu ikienda vikao vya harusi inabeba kadi 20 inakuja kugawa kama sakrament. Akhuu.