Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

umenikumbusha ,wakati nataka kuolewa niliwaambia ndugu zangu sitaki send off wala kitchen party! wakasema huwezi kwenda hivyo nawajua sana ndugu zangu ni watu wa lawama na wakikufanyia kitu utakuwa mtumwa wao!wakajichanga wakaandaa kisherehe nikasema sawa mimi nikajishonea kanguo changu na mpambe wanagu! ndoa yangu iliandaliwa ndani ya mwezi mmja tu!na ilikuwa maksudi ili kukwepa usumbufu na watu mume wangu ni mchangiaji mzuri sana watu wakamwamba kaka umetuchangia sana hatuwezi kukuacha haya ,ikaisha harusi sasa eti kila ndugu wanakuja niomba michango na mmja akanitamkia si na wewe tulikuchangia ,nikamuuliza nilikuomba au kukulazimisha it was ua good will sasa hivi nina watoto wa shule wakulipia ni june hii siwezi kukupa mchango mtoto wangu asiende shule !mpaka leo hakuna salamu.ila nimeshajitoa kwenye kuchangia mtu tu kisa anakujua ndio akupe mikadi!sitak mazoea
 
mimi niliamua michango basi baada ya mwezi mmoja mwaka juzi kupata kadi ambazo zilizidi mshahara wangu kwa 150%.Toka siku hiyo simchangii mtu,wewe ukiwa unaoa nialike nije kwenye sherehe,ntakachokuja nacho ndo mchango wangu kwako unialiki poa,sina shida....maana nnachanga laki moja,nije niuzulie vikao vya kujadili jinsi ya kugawa beer siku ya harusi,kila siku ya kikao kwanza nnachoka pili nnatumia mafuta ya gari ,then siku ya harusi ukumbi upo mbezi beach tuko ninapokaa na hizi foleni nnatumia tena karribu elfu 30 za petrol,cjanunua dhawadi,saloon n.k alafu harusi yenyewe naweza enda huko koote nikaishia tubia tutatu mc nae anaboa story zile zile kama harusi 5 hivi nilizoudhuria miezi miwili iliyopita.Wa tanzania inabidi tuanze kuchangiana kupeleka waototo vyuo vikuu au tuanze kuachangiana kujenga nyumba au kuanzisha biashara haya mambo ya kuchangia harusi ata ulaya ayapo
 
haahaa! Niko hapa! 2namwita tu mjumbe wa nyumba 10 anatufungisha ndoa,2nanunua zetu azam kola,2napika wali wetu maharage na mchicha pembeni akaaah! Ndoa tayar!
Wala sijammanisha hivo Munkari..
Fanya arusi/sherehe unayoweza kuimudu, kama huna uwezo wa 15M, kwa nini uwape watu tabu? kuwachangisha watu, wengine hata hamna urafiki, kisa tu mlikutana kwenye shopping moll siku moja mkachagua nguo/viatu pamoja.
 
Last edited by a moderator:
Yaani nikipata m/ke asiyependa miharusi nitafurahi!!!!!!!!
Eli79 niko hapa adha ya kuanza kupigiwa watu wakuchangie mi mwenyewe siitaki...

mtu akiona sim yako anajua tu tayari hata kama umepiga kwa LENGO lingine!!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Hili swala la michango ya harusi kila mtu analalamika lakini ikifika wakati wake anachangisha wengine. Ndio maana tabia inaendelea bila kikomo.

Na hii ni kwasababu yeye aliwachangia wenzie ndo maana anataka kulipiza!
Kwa mawazo yako mtoa mada hatachangisha watu wakati yeye wamemkamua hadi kaamua kuleta mada?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Na watu wakimchangia yeye watataka nao baadae awachangie. And the cycle continues...

One has to be courageous to break the cycle. The only point where one can break the cycle is on his own event...
 
Eli79 niko hapa adha ya kuanza kupigiwa watu wakuchangie mi mwenyewe siitaki...

mtu akiona sim yako anajua tu tayari hata kama umepiga kwa LENGO lingine!!!!!!!!!!!
Heaven on earth...teh! umesahau? si nimeshatanguliwa tayari..haha..
Turudi kwenye mada; sipingi arusi 100% ila wengine wanataka kuzidi uwezo wao..fanya sherehe iliyo kwenye uwezo wako. Madhara ya arusi ni makubwa kuliko hata faida...watu wanaanza maisha na madeni makubwa! wengine wanachukua hata mikopo..
 
Last edited by a moderator:
napata kadi za kuchangia harusi karibu kila mwezi naletewa karibu kadi 3, @50,000 approximately =150 , 000 .
Haya majanga sana ,mshahara wangu 550,000 , which means 30% michango harusi ,ninaacha haya mambo ,mimi mwenyewe sitafanya hiyo mambo, yaani kila weekend tupo busy kuchangisha harusi ,kama tunataka kutokomeza umasikini na wakati tunatiana umasikini ,siwezi tena.jamani kama huna uwezo usisumbue watu bwana ,funga ndoa ya kawaida tuache mambo ya kuiga

baada ya ww kuchangiwa na kuoa leo kwa waliokuchangia imekuwa kero ha ha ha binadamu banaa!
 
Na watu wakimchangia yeye watataka nao baadae awachangie. And the cycle continues...

One has to be courageous to break the cycle. The only point where one can break the cycle is on his own event...

kiukweli hii mambo inapoenda sio vizuri.
kuna mtu nlimpa 50 ya mchango, eti akaanza kuniambia ooh hiyo ni single. that means nimuache wife nyumbani
nikamuambia huo upumbavu sifanyi,chukua hiyo 50 ila kwenye harusi yako hunioni.

this is too much aisee, now minimum wanakuambia double 80,000
 
yani mie kuna mtu ananisumbua hapa...................mpaka kero! nna mapango wa kumpa elf 20!
na kuna mwingine anauguliwa...............sijui nafanyaje?!?!
 
nilishatoa msimamo wangu, ninayemchangia ni kwa sababu namfahamu na kuna umuhimu wa kumsaidia si kwa sababu ya harusi.
 
ndo hasara za kutegemea mshahara hizo..ongeza vyanzo vya mapato aisee...the irony could be anaelalamika amechangiwa na watu..kama ameshaoa au kuolewa, or dada zake au kaka zake wamechangiwa wakati wanafunga ndoa..toa hela hizo..kama una guts mwambie mtu hauna hela sio unalalama...tu....mtazamo binafsi
 
heee hahahahahahah usinichekeshe mie cha kufanya ni kuwatolea nje tu hao hawatakuzonga zonga na kadi bestito
Napata kadi za kuchangia harusi karibu kila mwezi naletewa karibu kadi 3, @50,000 approximately =150 , 000 .
Haya majanga sana ,mshahara wangu 550,000 , which means 30% michango harusi ,Ninaacha haya mambo ,mimi mwenyewe sitafanya hiyo mambo, yaani kila weekend tupo busy kuchangisha harusi ,kama tunataka kutokomeza umasikini na wakati tunatiana umasikini ,siwezi tena.Jamani kama huna uwezo usisumbue watu bwana ,funga ndoa ya kawaida tuache mambo ya kuiga
 
Kwa wengi wetu tukishaoa au kuolewa tunaanza kutokuona umuhimu tena wa kuchangia wenzetu. Si vizuri. Changia lakini kwa kiwango unachokimudu. Ukiwa huna genuinely, bajeti imebana kwa nini usimwambie mhusika? Na kama huna kiwango kinachotarajiwa si utoe kilichopo?

Tuache uzungu. Utamaduni wa kuchangiana ni mzuri. Unajenga udugu tukiondoa hizi takataka za kuwekeana viwango na kulazimishana.
 
Napata kadi za kuchangia harusi karibu kila mwezi naletewa karibu kadi 3, @50,000 approximately =150 , 000 .
Haya majanga sana ,mshahara wangu 550,000 , which means 30% michango harusi ,Ninaacha haya mambo ,mimi mwenyewe sitafanya hiyo mambo, yaani kila weekend tupo busy kuchangisha harusi ,kama tunataka kutokomeza umasikini na wakati tunatiana umasikini ,siwezi tena.Jamani kama huna uwezo usisumbue watu bwana ,funga ndoa ya kawaida tuache mambo ya kuiga

Daaah mkuu umeongea kwa uchungu sana which means imekuuma hiyo kitu, kiukweli mm binafsi hainiingii ikilini kutaka kuonyesha ufahari wakati uwezo wako ni mdogo, bora kuoana kimyakimya tu
 
Sherehe ya ndoa inategema na Uwezo,networking,mipango na nafasi.
Kuna kitu kinaitwa Maslow hierachy needs,Motivation theory.....ni kila mtu ana jinsi yake ya kufurahia jambo,mwingine atataka kupiga makelele,mwingine atataka kukaa kimyaaa kama mgonjwa.
Kuhusu kuwaalika watu kumchangia:kam nilivosema,its rotating,kama wewe ulichangiwa ktk harusi yako hutakiwi kuanza kuchukia kuchangia lazima uchange na wewe waliokuchangia,
Ok,kama hujawahi kufanya harusi kwa sababu zako binafsi unazoziona wewe za muhimu sasa kama mtu anakufuata umchangie na wewe uchumi wako ni mdogo,angalia nafasi yako,ukaribu nae,na satisfaction yako iko wapi,isije kuwa wewe hujafanya kisa huna uwezo.
wazungu wao mwanaume anaalika watu,ndugu na rafiki wa karibu sana kujumuika nae eneo fulani ,nao wanakuja kujilipia kwa Gharama zao wenyewe,sasa hii ni sawa na kuchangishana huku Africa,
ili uende kwenye sherehe si inabidi ujitolee kiasi cha fedha,badala ya kwenda na hela yako mfukoni,mtu anakusanya kwa kadri mila na tamaduni zinavomruhusu.
but una Uamuzi Uhuru wa kufanya au kuacha kuchangia,na hivyo unaweza kujiwekea mfumo wako wa kuishi ktk jamii,
kwasababu kuna michango mingine ipo ktk jamii kama mchango wa shule,kanisa,barabara nk.
So tengeneza utaratibu utakaoona unakufaa ili usimbugudhi mtu.
Maisha ni jinsi unavyoyapanga.
Kila mafanikio yana kilele chake,mwingine atataka watu wote wajue leo ni siku ya kilele chake hivyo kutumia utaratibu ule ule uliopo ktk jamii,kuchangisha.
 
Napata kadi za kuchangia harusi karibu kila mwezi naletewa karibu kadi 3, @50,000 approximately =150 , 000 .
Haya majanga sana ,mshahara wangu 550,000 , which means 30% michango harusi ,Ninaacha haya mambo ,mimi mwenyewe sitafanya hiyo mambo, yaani kila weekend tupo busy kuchangisha harusi ,kama tunataka kutokomeza umasikini na wakati tunatiana umasikini ,siwezi tena.Jamani kama huna uwezo usisumbue watu bwana ,funga ndoa ya kawaida tuache mambo ya kuiga

Mimi niliisha acha kuchangia, ukiendekeza utakuwa masikini, ofisi nzima MTU akioa au akiolewa uchange, mtoto wa dada kaka yake anataka umchangie. Hao maharusi hata kuwajua huwajui, taxi driver wa nyumbani wa ofisini umchangie. Dada wa salon, FUNDI wa gari wa NGUO wote kadi, nimeisha SEMA BIG NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
 
Back
Top Bottom