Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Tatizo mtu anakupigia simu halafu anakuuliza hivi siku hizi unafanya kazi wapi??
Ukimtajia tu anakukadiria na kiwango cha mshahara unachopata halafu anakukandamizia na mchango hapo hapo.......

Hii kitu inanikera sana wanashindwa kufahamu ubongo wa mtu unawaza nn katika mipangilio ya kimaisha. Michango ya harusi No.
 
Ndiyo majukumu yenyewe hayo. Mbona mkialikwa kwenye kikao mnapleji mahela kibaao, huku jukwaani mnalalamikia kadi.....
 
Nakumbuka Rais wetu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa aliwahi kulikemea hilo na akashauri watu wachangie masuala ya kuleta maendeleo ktk jamii na sio harusi !
 
Kwa mkoa wa kilimanjaro na arusha usipochangia wanakutenga ,hata kama Uko ughaibuni lazima wakutumie email .wanakupa na a/c # au wanasema Tuma kwa money gram au western union
 
Hii michango ni ni majanga .Arusi mchango ,ubarikio mchango .komunyoo mchango ,kipaimara mchango ,send off mchango ,misiba mchango kuhusu misiba Sina tatizo la kuchangia maana ukipaata matatizo wanasema ngoja akazike mwenyewe .
 
hili la michango ya harusi linaonyesha kama taifa tulivyo wajinga, hakuna taifa la werevu utakuta usengehe huu.
 
Chukua hatua acha kuchangia harusi na wewe ukiwa na harusi alika watu waje kusherekhekea na sio kutoa mchango. Hii kitu inaweza kabisa kufa iwapo tutaanza nasisi wenyewe tusisubiri mtu mwingine atuamulie . Tuwe mbele ktk kuisaidia jamii hasa kwenye maradhi. Ukiwa na 50000 nenda pale muhimbili angalia ni nani amekosa pesa ya dawa au vipimo msaidie huyo au nenda mashuleni utapewa majina ya watoto walio na hali ngumu then wasaidie ada au uniform.
 
Nachangia watu wa karibu sana hasa Ndugu rafiki nikufikirie sana tena baada ya kukukwepa sana Mwaka huu nimepokea kadi 10 woi walioambulia ni ndugu wawili .... kuna jamaa kwa office yeye kwenye droo yake kuna change change ukipeleka kadi unaambulia buku mbili tu ukishangaa unafukuzwa...
 


Michango go ya harusi ni majangaaaaaa, cha MSINGI ni kuacha Kabisa kuchangia
 


Sawa, LAKINI fikiria yafuatayo:-

1. Nyama ya kuku na ng'ombe huliwa sana kwenye sherehe; wafugaji na wauzaji pamoja na familia zao wanafaidika.
2. Wali, ndizi, mbogamboga n.k havikosekani kwenye sherehe; wakulima, wafanyabiashara sokoni pamoja na familia zao wanafaidika.
3. Wapiga picha, MCs, Video shooters, watengeneza kadi pamoja na familia zao wanafaidika.
4. Wenye kumbi pamoja na familia zao wanafaidika.
5. N.k

MUHIMU:
Ni vema tukajenga utamaduni wa kuchangia kulingana na uwezo ulio nao.
 
Hakuna upuuzi ambao siupendi kama huo,na source ya yote ni umaskini wa nchi zetu za Africa but wenzetu developed countries scenario kama hii ni chache sana,kuna mwana ananifanyia followup za ajabu dhidi ya mchango hadi kero......
 

Ukiweza kuchangia changia. Ukiwa huna uwezo sio vibaya kuwajulisha wahusika kuwa huna uwezo. Kumbuka kuchangia harusi sio lazima ni hiari
 
Hii mada nadhani ni mara ya 10 kama si zaidi kuwekwa humu!!!!. Mkuu kama mtu anakukera mpe laivu, kuja kulalamika lalamika hapa hakusaidii kitu. Kama hutaki kuchanga acha PERIOD.
 

Du! Hii nimeipenda , imenichekesha sana!
 
hakuna anaependa harusi hasa wanaume ila familia zinasema zimeshachangia sana na zenyewe MDA WAO NDIO HUU... so hutaki WATAKUFANYIA:A S thumbs_down:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…