Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mkuu wala usihofu, mchango wa harusi/send off hauokuongezei au kukupunguzia marafiki. Usifikiri kama ukimchangia mtu ndo atakuona wa maana au kuwa usipomchangia atakulaumu. Changia tu kama una nafasi maana binadamu siyo 'parokia' ni mjamii.
 

kila anayeniletea kadi ya harusi na mimi huwa nampelekea kadi kwa ajili ya mchango wa ada za watoto wangu.
 
kuna familia nyingine unakuta ndugu wana pesa sana ukitangaza ndoa utachangiwa mkwanja wa kutosha ila ukiomba mtaji ufanye business at least 1 m no one is ready!

nakubalina na wewe mkuu 100%
 
umefika wakati sasa familia husika wajipange wenyewe na harusi yao. Tuachane na utamaduni wa kutoa kadi za michango. Maharusi wenyewe wajipange wakishirikiana na familia zao. Kama hawawezi basi wafanye sherehe ndogo tu.

unachokisema ni kweli mkuu,je kama na wewe ni miongoni mwa wale waliochangiwa inakuaje hapo
 
Wape makavu laivu, na kwa nini unapokea hizo kadi? Kulalamika humu haitasaidia waambie wazi hutachangia.
 
mkuu utingo umenivunja mbavu hapa,ha ha ha

mkuu, too much is enough. wakati mwingine inakera sana. vitoto vyako viko nursery lakini kila mwezi una bajeti ya zaidi ya laki kuchangia harusi na viada vya watoto vinakusumbua.
 
umefika wakati sasa familia husika wajipange wenyewe na harusi yao. tuachane na utamaduni wa kutoa kadi za michango. maharusi wenyewe wajipange wakishirikiana na familia zao. kama hawawezi basi wafanye sherehe ndogo tu.

Ufahari ndugu yangu ndio unasababisha yote haya na kushindana wakati uwezo hakuna.
 
mkuu, too much is enough. Wakati mwingine inakera sana. Vitoto vyako viko nursery lakini kila mwezi una bajeti ya zaidi ya laki kuchangia harusi na viada vya watoto vinakusumbua.

alafu anakwambia mchongo si chini ya laki moja
 
Tatizo linakuja pale nawe ulioa kwa stail hiyo ya kuchangiwa lazima urudishe fedha za watu,ila kutoa ni hiari sio lazima kama umekwama potezea
 
kuna familia nyingine unakuta ndugu wana pesa sana ukitangaza ndoa utachangiwa mkwanja wa kutosha ila ukiomba mtaji ufanye business at least 1 m no one is ready!
Hiyo si Kama ushirika wa pombe kwenye bar? Marafiki watakunywesha mpaka ushindwe kukumbuka nyumbani kwako, lakini muombe akusaidie japo sembe ya Siku hiyo atakwambia "....brother pombe nkunyweshe na mkeo nkulishie?......"
 
hiyo si kama ushirika wa pombe kwenye bar? Marafiki watakunywesha mpaka ushindwe kukumbuka nyumbani kwako, lakini muombe akusaidie japo sembe ya siku hiyo atakwambia "....brother pombe nkunyweshe na mkeo nkulishie?......"

huu utamaduni sio mzuri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…