mkuu kama umekuja kulalamika huku wala sitaki unichangie tena. Baki na hizo cent zako
Wadau hii michango imekuwakero sasa,
binafsi mpaka sasa hivi nina kadi 6 za michango,simu kila mda inapigwa kukumbushwa michango,sms
ndo usiseme.
Inatubidi kubadilika kabisa na hii michango isiyokuwa na tija zaidi ya kuacha madeni na lawama.
Unapigiwa simu kila mara kama unadaiwa vile.
Kama na wewe umekutana na kero yoyote embu tujuze hapa na nini suluhisho?
simple, kuwa na fixed amount ambayo upo radhi kutoa,
e.g 4000,5000 ,20000 etc.
ukipewa kadi ya mchango pale pale unampa mtu elfu 5, za mchango wako. baada ya muda watu watakujua kuwa unatoa chini ya matarajio yao,wataacha kukusumbua na kadi za mchango.
mimi huwa namwambia mtoa kadi, sitochanga nikiweza ntakupa zawadi,na nitakuja Kanisani,au nyumbani ,so inapunguza usumbufu.
Hilo ni tatizo sana mijini,vijijini huku hakuna mambo hayo, hatahivyo kama ulivyosema inategemeana na ukaribu wenu na muoaji!
Ifike wakati ndugu zangu tubadilike, mambo ya arusi yabaki kuwa ya kifamilia zaidi ili sasa tuelekeze michango kwenye elimu na afya maana ukifika kwenye mashule ya serikali hali inatisha ukienda hospital watanzania wenzetu wamepoteza matumaini, nadhani kuna haja ya kuwepo mabadiliko makubwa kifikra