Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Hili jambo linanikera sana japo sijao. Nimeshindwana na wanawake kibao kwa kuendekeza kufunga harusi za gharama kubwa.
 
Kuna watu kama wa4 hivi wananisumbua kwenye simu nikaamua kuwaweka kwenye blacklist...Ujinga tu mtu uwezo huna unataka kufunga ndoa ya milioni 100.
 
Cha kushangaza ni kwamba usipomchangia aliyekuomba mchango anakufanya adui wake. Jamani jamani, tunaenda wapi watanzania???
Kila kona harusi michango, kwenden zenu huko. Shenzy kabisa
 
Habari za asubuhi
wakuu? Hii wiki tu nimepokea sms na kupigiwa simu zaidi ya 5 watu
wanakudai mchango uchangie harusi yake. Namaanisha kudai mchango nawala
sio kuomba uchangie. Mtu anakupigia simu alafu anakwambia taja "pledge'
yako kwenye harusi yangu. Unamjibu kistaarabu tu ondoa shaka muda
ukifika nitakuchangia tu. Yeye anakulazimisha usiwe na wasi ahidi kiasi
chochote kile haina tatizo. Baada ya kukubana sana unamweleza kiasi
fulani, huyo anayedai anakujibu samahani kaka/dada kiwango changu cha
chini cha kunichangia ni laki moja.

Samahani lakini sijui kwa vile mimi ni mgeni na haya maswala au ndio
kawaida kwa wote.
Maana ndani ya mwezi mmoja natakiwa niwachangie watu zaidi ya 5.
Swali hiyo hela anayodai mtu aliiweka mfukoni mwako? Maana kwa mimi
ninavyojua mtu unapoguswa na swala hili na ukaribu na mhusika ndivyo
utakavyotoa kiasi kikubwa.
Chakushangaza kingine unapigiwa simu na marafiki nao utoe pledge kwa mtu
ambaye humfahamu.

Mimi binafsi sitamkwaza mtu wakati wa kuomba kuchangiwa.

NIMEMALIZA, NAWAKILISHA.

Hiyo tabia ilinifnya mm nikabadili misa, kutoka ya kwanza kuwa nasali ya pili.
jamaa anadai kama alinikopesha, siku moja nikampa elfu 50,tulkutana kanisani, kufika mchana ananipgia(tena kwa kulazmisha, oohh hii haitoshi ongeza elfu 30 ili upate single), yan jamaa alkuwa haombi, analazmisha.
ki ukweli alinitoa hamu ya kuchangia kabisa, sasa hv anafululiza kupga simu asbhi kabla hata sijapgiwa simu na mpenzi wangu! nataka nikikutana nae, nmwambia anipe hyo hamsini nimpe dola, akinipa imekula kwake.
 
Alafu sasa utakuta mtu hamjawasiliana kwa zaidi ya hata miaka minne, ghafla unaona anakutafuta akidai umepotea sana na anakusalimia tu. Then siku mbili zijazo unaona msg ya kikao cha kwanza cha harusi, hujakaa vizuri anaanza kukung'ang'aniza ahadi cjui pledge then unaamua kumchangia, sasa ckilizia iyo follow-up anayoifanya utadhan unataka kumzulumu haki yake ya kuishi!! Sikuizi wala hata cjusumbui, na isitoshe kausafiri kanakula mafuta kweli kwa ajili ya foleni bac ni fasta tu jibu la cjapata linatoka!



namchana live
 
hii michango bwn,natamani ikifika yangu nisichangishe watu aisee...afu hela kibao za michango zinalipiwa ukumbi,
masherehe ya kumbi zingine mi naona hata hayanogi jmn,boring kabisaaa..bora kwenye garden hivii au beach..
 
Nini hasa main reason ya kuchanga watu hela kwa ajili ya harusi au cost sharing ? Alafu kwanini uweke kadirio as if hiyo hela ni compulsory amount while its just voluntary amount .? We have to change.
 
Harusi mimi wala haziniumizi kichwa.Nikipewa kadi namuambia mtoaji,tutaangalia maana nina kadi nyingi then wala sihangaiki tena. Pili nikubaliane na mchangiaji mmoja hapo juu pamoja mbunge wa Nkasi kuwa hizi fedha zinapaswa zitozwe kodi kubwa sana,say 35% ili watu waumie lakini pia itasaidia kutanua tax base ya nchi hii inayotegemea misaada sana.
Mwisho niwakumbushe tu wale ambao hawajaoa kuwa kama unampango wa kuchangisha pesa ili kufanikisha harusi yako then changia za wenzako kwakuwa wote wanaochanga wanaivest ili ikifika wakati wao,ndugu zao au watoto wao wachangiwe na hawachangi kwasababu ya upendo. Ila kwakuwa mimi sina mpango kumchangisha mtu SITOMCHANGIA MWINGINE PIA ( isipokuwa tu kwenye matatizo)
 
Mie nilishasema SICHANGII mtu lakini kusema kweli uso ume umbwa na haya,,,kuna mtu atakuja unashindwa hata kumkatalia.
 
Habari za asubuhi wakuu? Hii wiki tu nimepokea sms na kupigiwa simu zaidi ya 5 watu wanakudai mchango uchangie harusi yake. Namaanisha kudai mchango nawala sio kuomba uchangie. Mtu anakupigia simu alafu anakwambia taja "pledge' yako kwenye harusi yangu. Unamjibu kistaarabu tu ondoa shaka muda ukifika nitakuchangia tu. Yeye anakulazimisha usiwe na wasi ahidi kiasi chochote kile haina tatizo. Baada ya kukubana sana unamweleza kiasi fulani, huyo anayedai anakujibu samahani kaka/dada kiwango changu cha chini cha kunichangia ni laki moja.

Samahani lakini sijui kwa vile mimi ni mgeni na haya maswala au ndio kawaida kwa wote.
Maana ndani ya mwezi mmoja natakiwa niwachangie watu zaidi ya 5.
Swali hiyo hela anayodai mtu aliiweka mfukoni mwako? Maana kwa mimi ninavyojua mtu unapoguswa na swala hili na ukaribu na mhusika ndivyo utakavyotoa kiasi kikubwa.
Chakushangaza kingine unapigiwa simu na marafiki nao utoe pledge kwa mtu ambaye humfahamu.

Mimi binafsi sitamkwaza mtu wakati wa kuomba kuchangiwa.

NIMEMALIZA, NAWAKILISHA.

Hii michango ya harusi ni ujinga wa hali ya juu, binafsi huwa sichangii. Mjadala kama huu uliwahi kuletwa hapa JF 2007 au 2008. Kuna mtu alitangaza kuchangiwa harusi humuhumu JF. Duh! kuna tulioupinga sana tu, naona wakaacha baada ya hapo kuomba michango mpaka JF.

Mimi nikiletewa kadi ya mchango huwa naijibu kuwa, samahani sichangii harusi. Na nikiambiwa kwa mdomo huwa nasema ukweli kuwa, samahani sichangii harusi.

Inahusu nini kuchangia harusi?
 
Aisee unajibu kigumu sana ! Sidhani kama wanarudi tena kukushawishi uwachangie.
Hii michango ya harusi ni ujinga wa hali ya juu, binafsi huwa sichangii. Mjadala kama huu uliwahi kuletwa hapa JF 2007 au 2008. Kuna mtu alitangaza kuchangiwa harusi humuhumu JF. Duh! kuna tulioupinga sana tu, naona wakaacha baada ya hapo kuomba michango mpaka JF.

Mimi nikiletewa kadi ya mchango huwa naijibu kuwa, samahani sichangii harusi. Na nikiambiwa kwa mdomo huwa nasema ukweli kuwa, samahani sichangii harusi.

Inahusu nini kuchangia harusi?
 
Dah hapa na kadi 6 zote si chini ya elfu 50 unaambiwa afu kuna mbili ni nime pledge 100,000 kila moja izi za ndugu, hapo kwa haraka haraka si chini ya 500,000 zote izo nilipe kuanzia mwezi huu mpaka wa 7 mwishoni, dah naunga mkono hoja hii kitu ibaki ndani ya familia
 
Ndoa Ni lazma harus AMA sherehe c lazma hasa kulazmishana Kwan NDOA SIDHARULA. Mimi Na my wife wangu tulikusanya Watu kanisani kwa kad za Mwaliko tu tukakoboa mchele gunia kwa UPENDO Wa kanisa wakapka wali bwena Na sherehe ndogo kanisani had saa 4usku mambo yamekwisha.usidhan sna hadhi wala cash hapana Nina mambo tu hata wife Ni bint Wa tajri m1 MG wala hakumind Na akabark kwa ahad ya bat 60 za chataa smba.Cha ajabu Mbali Na Watu Wa kanisan....wanaojfanya Wa mataw dunian hawakuja kabisa Na chakula kuliwa Na watoto weng wadogo Na Watu Wa kanisa kubebaa mavyakula lukuki ktk ndoo zao. Na iman Ni Baraka tupu mbele za bwana.Ndoa yetu Kwakweli Ni yenye furaha sana,Amani.UPENDO,heshma,Na matumain yenye harufu ya utajr.MAISHA Ni VILE UNAVYOISHI.
 
ni upuuzi na ujinga mtupu. Tunapoteza Resources, muda, nguvu nyingi na tunachosha akili sana kwa ajili ya sherehe na gharama kubwa za harusi. tufike mahali kila mtu aamue kuoa kwa gharama ambazo ana uwezo nazo.
Lakini nadhani tunaenda vizuri kdg naona jamii inaanza kuelimika juu ya hili na indications mojawapo ni jinsi ambavyo utastruggle kupata michango kutoka kwa watu lazima utumie nguvu ya ziada. Wengi wetu tunatoa michango nwdys kwa kuoneana aibu tu lakini moyoni inatuuma sana. mf. mm nimejitahidi kuavoid hii kitu kwa 70% hiyo 30% ni wale ndugu na jamaa wa karibu ambao nashindwa kbs kujinasua bt i believe with time nitaweza kujinasua kwa 100%
 
sisi watanzania hatupendi kuwajibika na kufanya kazi kwa bidii, unakuta jamaa lofa tu wa kijiweni anatengeneza kamati nzuri ya harusi na kukusanya Mil. 6 au zaidi, then anafanya harusi ya kifahari, that is irresponsible and corrupt behavior!

mimi na my wife wangu tulibariki ndoa bila sherehe mapema alfajiri, na niliwahi kazini saa moja na nusu asubuhi.Total cost haikuzidi Sh. ELFU HAMSINI!

hii nimeipenda sana
huna deni na mtu maana utakuta mara nyingi kama ulifanya sherehe ya kuchangisha watu, hao waliochanga wote wanajua wamewekeza hapo na ndio maana zikifika zao au hata za ndugu zao wanafanya kama ni deni hivi.
sijaolewa lakini hapo kabla nilikuwa napenda sana siku nikiolewa nifanye sherehe kubwa ila huyu anayetaka kunioa kwa amenibadilisha mawazo maana amefanya nijione kuwa wazo langu lilikuwa la kijinga sana
harusi kubwa then what????
 
hahahahahaha hapo una harusi kama tano na tena minimum kutoa ni elfu 50 mbona utaumwa kichwa
 
Vipi wale jamaa ambao walimchangia mh. Vicky kamata wamerudishiwa michango yao au ndo ile kwa mganga hakirudi kitu????????????
 
Back
Top Bottom