Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna watu kama wa4 hivi wananisumbua kwenye simu nikaamua kuwaweka kwenye blacklist...Ujinga tu mtu uwezo huna unataka kufunga ndoa ya milioni 100.
Ndiko tunakoelekea huko mkuu muda si mrefu...heri ya nusu shari kuliko shari kamili
Habari za asubuhi
wakuu? Hii wiki tu nimepokea sms na kupigiwa simu zaidi ya 5 watu
wanakudai mchango uchangie harusi yake. Namaanisha kudai mchango nawala
sio kuomba uchangie. Mtu anakupigia simu alafu anakwambia taja "pledge'
yako kwenye harusi yangu. Unamjibu kistaarabu tu ondoa shaka muda
ukifika nitakuchangia tu. Yeye anakulazimisha usiwe na wasi ahidi kiasi
chochote kile haina tatizo. Baada ya kukubana sana unamweleza kiasi
fulani, huyo anayedai anakujibu samahani kaka/dada kiwango changu cha
chini cha kunichangia ni laki moja.
Samahani lakini sijui kwa vile mimi ni mgeni na haya maswala au ndio
kawaida kwa wote.
Maana ndani ya mwezi mmoja natakiwa niwachangie watu zaidi ya 5.
Swali hiyo hela anayodai mtu aliiweka mfukoni mwako? Maana kwa mimi
ninavyojua mtu unapoguswa na swala hili na ukaribu na mhusika ndivyo
utakavyotoa kiasi kikubwa.
Chakushangaza kingine unapigiwa simu na marafiki nao utoe pledge kwa mtu
ambaye humfahamu.
Mimi binafsi sitamkwaza mtu wakati wa kuomba kuchangiwa.
NIMEMALIZA, NAWAKILISHA.
Alafu sasa utakuta mtu hamjawasiliana kwa zaidi ya hata miaka minne, ghafla unaona anakutafuta akidai umepotea sana na anakusalimia tu. Then siku mbili zijazo unaona msg ya kikao cha kwanza cha harusi, hujakaa vizuri anaanza kukung'ang'aniza ahadi cjui pledge then unaamua kumchangia, sasa ckilizia iyo follow-up anayoifanya utadhan unataka kumzulumu haki yake ya kuishi!! Sikuizi wala hata cjusumbui, na isitoshe kausafiri kanakula mafuta kweli kwa ajili ya foleni bac ni fasta tu jibu la cjapata linatoka!
Habari za asubuhi wakuu? Hii wiki tu nimepokea sms na kupigiwa simu zaidi ya 5 watu wanakudai mchango uchangie harusi yake. Namaanisha kudai mchango nawala sio kuomba uchangie. Mtu anakupigia simu alafu anakwambia taja "pledge' yako kwenye harusi yangu. Unamjibu kistaarabu tu ondoa shaka muda ukifika nitakuchangia tu. Yeye anakulazimisha usiwe na wasi ahidi kiasi chochote kile haina tatizo. Baada ya kukubana sana unamweleza kiasi fulani, huyo anayedai anakujibu samahani kaka/dada kiwango changu cha chini cha kunichangia ni laki moja.
Samahani lakini sijui kwa vile mimi ni mgeni na haya maswala au ndio kawaida kwa wote.
Maana ndani ya mwezi mmoja natakiwa niwachangie watu zaidi ya 5.
Swali hiyo hela anayodai mtu aliiweka mfukoni mwako? Maana kwa mimi ninavyojua mtu unapoguswa na swala hili na ukaribu na mhusika ndivyo utakavyotoa kiasi kikubwa.
Chakushangaza kingine unapigiwa simu na marafiki nao utoe pledge kwa mtu ambaye humfahamu.
Mimi binafsi sitamkwaza mtu wakati wa kuomba kuchangiwa.
NIMEMALIZA, NAWAKILISHA.
Hii michango ya harusi ni ujinga wa hali ya juu, binafsi huwa sichangii. Mjadala kama huu uliwahi kuletwa hapa JF 2007 au 2008. Kuna mtu alitangaza kuchangiwa harusi humuhumu JF. Duh! kuna tulioupinga sana tu, naona wakaacha baada ya hapo kuomba michango mpaka JF.
Mimi nikiletewa kadi ya mchango huwa naijibu kuwa, samahani sichangii harusi. Na nikiambiwa kwa mdomo huwa nasema ukweli kuwa, samahani sichangii harusi.
Inahusu nini kuchangia harusi?
sisi watanzania hatupendi kuwajibika na kufanya kazi kwa bidii, unakuta jamaa lofa tu wa kijiweni anatengeneza kamati nzuri ya harusi na kukusanya Mil. 6 au zaidi, then anafanya harusi ya kifahari, that is irresponsible and corrupt behavior!
mimi na my wife wangu tulibariki ndoa bila sherehe mapema alfajiri, na niliwahi kazini saa moja na nusu asubuhi.Total cost haikuzidi Sh. ELFU HAMSINI!
Mie nilishasema SICHANGII mtu lakini kusema kweli uso ume umbwa na haya,,,kuna mtu atakuja unashindwa hata kumkatalia.