Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mkuu wenzio wataendelea kuchangia, wewe kama umeishiwa utabaki peke yako!
 
Wengine wanachangisha kwa ajili ya ndugu zao, utasikia nina harusi ya mtoto wa shangazi yangu nitakuletea kadi unichangie dah, jamani!
 
Personally nilishajiwekea principle ya kutochangia hizo harusi au send off.
Mtu akiniletea kadi namwambia face-to-face kuwa mimi sichangii namweleza kuwa huo ndo utaratibu wangu.
In short sitaki kabisa hayo mambo kwanza hata kwenye harusi siendi labda iwe ya ndugu wa damu kabisa mtu wa karibu mno.
 
Nimeripoti kwa muajiri wangu mpya, hata mshahara wa kwanza bado sijapokea, tayari nimemchangia mshikaji wa pmu anaenda kuoa, kiroho safi tu, hata hajaniomba na wala hajanipa, card!

Sijakaa sawa, mdada wa masjala, tena yupo likizo, katoka alikotoka kaja (kaacha likizo ili aje kusambaza cards za michango) kusambaza cards maofisini, yangu kaniachia mezani, cha kuudhi zaidi, haolewi yeye wala mamake, anaolewa mdogo wake! Na tayari kuna dada mwinginne kajichekesha chekesha siku hiyo, akanchomekea: "....... nina card yako!"

Basi angenipa pumzi walau kidogo!
 
Hapa nilipo nimenuniwa lakini na mimi nawaona kama ukoma, hawanisumbui nimegoma kuchanga sherehe gani bajeti milioni 30? nilona upuuzi wa karne. Lengo langu niwe na gari japo mbili nisiishi maisha ya kauka nikuvae kwa kuchangia starehe.

Kutiana ulofa ujinga:A S-eek:
 
Napata kadi za kuchangia harusi karibu kila mwezi naletewa karibu kadi 3, @50,000 approximately =150 , 000 .
Haya majanga sana ,mshahara wangu 550,000 , which means 30% michango harusi ,Ninaacha haya mambo ,mimi mwenyewe sitafanya hiyo mambo, yaani kila weekend tupo busy kuchangisha harusi ,kama tunataka kutokomeza umasikini na wakati tunatiana umasikini ,siwezi tena.Jamani kama huna uwezo usisumbue watu bwana ,funga ndoa ya kawaida tuache mambo ya kuiga

cha kushangaza kijana anaomba msaada sh 500,000 kama mtaji afanye biashara hakuna aliye tayari kumsaidia ila akitangaza harusi hata mil 20 atachangiwa!
 
haahaa! Niko hapa! 2namwita tu mjumbe wa nyumba 10 anatufungisha ndoa,2nanunua zetu azam kola,2napika wali wetu maharage na mchicha pembeni akaaah! Ndoa tayar!

cheka sana mimi! good sunday Munkari
 
Last edited by a moderator:
michango ya harusi imekuwa kero, tuacheni hii tabia inarudisha nyuma maendeleo
 
Tena unakuta mtu anadai km deni Mara simu mara katuma mtoto mara akufate kazin aah nimeichokaaa
 
harusi ya ml 30 miezi mitatu unasikia wameachana.
_nshakataa sichangii harusi kama ni kukosa marafiki na nikose tu! nitawazungusha hadi wachoke
 
Michango ya Harusi inakera sana; mtu afanye sherehe kulingana Na uwezo wake
 
Kumbe watu mmeanza kuelimika kwa vitendo! huwezi kupanga kuoa kwa kutegemea michango ya watu kama huwez acha usiwashurutishe watu eboooo!!
 
Back
Top Bottom