Utakuta karibu ya 50% ya kipato chako kinaenda kwenye michango isiokuwa na tija.
utakuwa mdogo wangu, si bure.
Nina zaidi ya miaka 5 nimeachana na huo upuuzi, kwenye elimu, magonjwa na misiba ndipo ninapotoa my hard erned money.
Bila shaka atakuwa na matatizo ya akili.
Kwasababu wewe umechangisha kwa sherehe yako??? Shame on you
Namaanisha aliyekuja kuomba mchango wa harusi kwa mfiwa mkuu.
Kwakweli, mimi nimepunguza kabisa, nikiwa njia moja kuachana kabisa na michango ya sherehe ZA harusi
Ni kweli mtoa mada hili swala mm limenikuta.nina cousin wangu Mkoa amepata tatizo la figo na akapata rufaa kuja MNH.Kwa kuona gharama za matatibu ya figo ni kubwa na dogo wazazi wako kijijini hali ngumu,ikabidi nibebe mzigo ,nikajarabu kutuma SMS kwa ndugu kama 30 tujaribu kuokoa maisha ya dogo ,kati ya hao 1 alitoa30,20,15,na 10 .ni watu 5 walijitoa.wakati huo kuna harusi ya ndugu mwishoni mwa novemba kuna watu wamehaidi mpaka laki wakishindwa kumsaidia dogo hata buku.Hapa ndiyo nimehapa kuto changia harusi nitasaidia tu watu wenye huitaji.
mimi nitachangia ndugu zangu wa damu kabisa
Hii michango imekuwa kero sasa hivi watu wamechanganyikiwa au nini maana kipindi cha nyuma hakukuwa Na mambo haya.
Kuna watu wa ajabu sana,unapanga kuoa huku huna hela unataka watu wengine wakuchangie,huu ni ujinga mkubwa. Raha zako ziwape wengine shida.
Unakuta mtu anataka kuoa,bajeti milioni 10,yeye ana milioni 1 na nusu,hizo zinginge anataka watu wamchangie,,ukipanga kuchangiwa harusi jiandae pia kuchangia mke.
Acheni kusumbua watu na harusi zenu..
i think na huu uzi umekaa kiusumbufu zaidi..
biblia imesema kila jambo na wakati wake...
kuna wakati wa kulia....lia!
kuna wakati wa kucheka...cheka!
kuna wakati wa kulalamika..lalamika
kama sasa imekuja time ya michango kwa ajili harusi ambayo ni sehemu ya furaha...changa japo kiduchu! au kama hauna basi jitolee hata kwenye kamati ya ulinzi! lol..