Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Ndoa nn harusi nn changanua
Ndoa ni sakrament (kile kitendo kinachofanywa na padri/mchungaji/sheikh cha kuwaunganisha) na harusi ni ile sherehe ya kusherehekea tukio hilo. Ndio maana unaitwa mchango wa harusi na sio mchango wa ndoa!
 
me nasema wazi me nitaoa kimtume kabisaaaaaa...thaiv napunguza ukali wa nyeeeeeeeeeeegeeeeeeezzzzzzzzzz stend ya mabasi mwanzaaaaaaaaaaaa
 
hahahahhaaaaaaaaaaaaaaaaaa nimeona umeongea kana kwamba tayari ndo maana nikakuuliza tu

bestito, mmh...!
nilitegemea tungeongea vizuri, kumbe unataka kujua tu. Kwani wewe ushampata asali wako??
 
Kama hujaoa huwez kujua maana ya hii kitu,binadam ameumbwa kusema tu,usipomwambia kero,ukimwambia kero,kiufupi harus ina lengo la watu kushuhudia ukiwa unatoka ktka hatua flan ya maisha,kuingia nyingine, cha msingi ni kuangalia mfuko wako ukoje na kupanga mipango inayoendana na uhalisia. Ila wakuu lazima mjue urafiki wa kweli una gharama na gharama wakat mwingine sio pesa tu hata muda.
 
Kama
hujaoa huwez kujua
maana ya hii kitu,binadam ameumbwa kusema tu,usipomwambia
kero,ukimwambia kero,kiufupi harus ina lengo la watu kushuhudia ukiwa
unatoka ktka hatua flan ya maisha,kuingia nyingine, cha msingi ni
kuangalia mfuko wako ukoje na kupanga mipango inayoendana na uhalisia.
Ila wakuu lazima mjue urafiki wa kweli una gharama na gharama wakat
mwingine sio pesa tu hata muda.

inaonekana limekugusa hili ushauri wa bure ni kwamba kama umeamua
kufanya harusi usisumbue watu kwa michango acha hao marafiki au ndugu
wakuchangie kwa hiari yao mambo ya kulazimisha niwe mwanakamati ili nitoe fedha nyingi ni upuuzi
 
Napata kadi za kuchangia harusi karibu kila mwezi naletewa karibu kadi 3, @50,000 approximately =150 , 000 .
Haya majanga sana ,mshahara wangu 550,000 , which means 30% michango harusi ,Ninaacha haya mambo ,mimi mwenyewe sitafanya hiyo mambo, yaani kila weekend tupo busy kuchangisha harusi ,kama tunataka kutokomeza umasikini na wakati tunatiana umasikini ,siwezi tena.Jamani kama huna uwezo usisumbue watu bwana ,funga ndoa ya kawaida tuache mambo ya kuiga

Mimi ninakadi ya dada mmoja anayeishi na mumewe kwa miaka 5 sasa lakini alisahau kufanya harusi wakati huo sasa ameleta kadi ya Kitchen Party na kisha atataka achangiwe na harusi. Kweli harusi ni kero na mbaya zaidi tunaelekea msimu wa harusi mwishoni mwa mwaka kadi zimeshaanza kumiminika. Mimi ya kwangu ambayo ilikuwa ni ya kubariki ndoa kwani nilishakuwa nimeishi na wife kwa miaka 8 tukiwa na watoto 3 (na sijaongeza mwingine, sasa hivi wa kwanza anaingia mwaka wa pili chuo kikuu) nilifanyia kijijini ilinigharimu Shilingi Sh. 92,000/= mwaka 2000na wala sikumchangisha mtu. Watu walikunywa ulabu kwa raha zao. Hakuna haja ya kuchangisha watu kwaajili ya harusi. Wewe unayetaka harusi andaa kadiri ya uwezo wako na ualike wale unaowataka. Mbona vipaimara, komunio na birthdays huwa tunafanya bila kuchangisha watu kwanini iwe harusi?
 
inaonekana limekugusa hili ushauri wa bure ni kwamba kama umeamua
kufanya harusi usisumbue watu kwa michango acha hao marafiki au ndugu
wakuchangie kwa hiari yao mambo ya kulazimisha niwe mwanakamati ili nitoe fedha nyingi ni upuuzi

Mkuu me cjakupinga,mtu huwez kuwapa kadi watu usiowajua, ni mwendawazimu atakayekuweka kwenye kamati mtu ambae hamjashibana after all wanakamat huwa wanaomba wenyewe.halaf kuna watu wengine wanapenda hizo mambo na wanafanya kama mtoko wa siku hiyo sababu hata spending yao kwa wkend moja haichez mbali na mchango wa harus,povu huwa linawatoka vijana waliotoka vyuo ndo wanaanza lyfe una mkopo wa alteza deduction zinakukamua,dem wako unataka akujue uko juu kumbe samaki samaki,unaingia na nyagi halaf unaagiza maji, lazima ulie ulie hapa,
 
Huu ujinga na uupuz mke wako mume wako unataka kufanya mambo makubwa kwa pesa za watu ujingaa huuu mnawaendekeza tuu kuchanga sawa ila amount ambazo ni reasonable ka 20,000 lakin 50000 ni kutiana umaskin na tunarudishana nyumba achachen na ujinga huu
 
na huwa tunatafutana wakati wa michango tu, harusi ikipita na mawasiliano yanakata.
 
yani mimi naboreka na haya makadiile mbaya. Kipato chenyewe kidogo yani full majanga.
 
Natamani kuchangia hata 2M. Lkn apewe mume kwa kujiengeleza kimaisha sio sherehe. Mtu anafanya arus ya 17m baadae anaenda kukaa room moja na.choo cha nje. Haikubaliki
 
Hivi ni sawa jamaa anataka kuoa hana hata sent mfukoni anategemea michango ya washkaji...?...Mi naona Harusi BOMBA ni ile jamaa anaandaa kila kitu anawaita washkaji kwenda kushuhudia,kumpongeza na kumpa zawadi....Au wana JF mnasemaje..?
 
Hapo umelenga penyewe, na inatakiwa bwana harusi aweze kuchangia atleast 75% ya gharama za harusi.
 
Hivi ni sawa jamaa anataka kuoa hana hata sent mfukoni anategemea michango ya washkaji...?...Mi naona Harusi BOMBA ni ile jamaa anaandaa kila kitu anawaita washkaji kwenda kushuhudia,kumpongeza na kumpa zawadi....Au wana JF mnasemaje..?

ulichoandika na id yako havifanani pyeeeee..
 
Back
Top Bottom