Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Nilishakataa michango ya harusi nami ikifika zamu sitaki mchango wako, nitachangia majanga ya elimu, magonjwa na njaa.

Hata mimi huo ujinga sifanyi,sitoi michango ya harusi na wala sitaomba ya mtu. Ukiendekeza huu ujinga wa kuchangia harusi mwisho wa mwaka utajikuta umetumia pesa nyingi sana. Kuoa ni kwa faida yako haina maana kusumbua wengine.
 
Harus kugharamia n.kutaka wewe muoaji unaweza ukafanya simple tu na ikafana
 
Nina wazo nataka kuchangia,swala la ndoa ni deni kwa mwenyezi mungu hivyo kila mtu lazima afunge ndoa,ili tuepukane na uzinifu,na swala la mtu asichangishe watu eti kisa raha atapata yeye mimi binafsi naona ni roho ya kimaskini na choyo na pia kujifanya tumeelimika sana bila kujali kuwa ni upuuzi kwa kuongea swala ambalo watu waliosoma wenzio wakilichambua wanakuona umetoa uzi wa kipuuzi,uchumi wa nchi,mifuko imetoboka,hali mbaya lazima mtu achangishe kwa wadau wake wakaribu na si lazima unaweza usitoe,kuna swala la kadi,mtu anasambaza kadi kwa watu wa karibu sana ambao ni uhakika na waliokaribu lakini sio sana sana ambao sio wa uhakika sana zinaitwa kadi za kubahatisha sasa nadhani wewe mtoa mada upo kundi la pili la watu wa kubahatishwa
 
Reactions: J C
Pili bila shaka wewe ni muslim,mana nyie ndoa hata ukiwaambia watu kuanzia asubuhi kwamba unaoa saa mbili usiku nyie ni poa,ila kristos ndoa zao ni process,then naomba umuulize baba yako,alivyofunga ndoa alichangisha au? Labda ndoa iwe ya mkeka
 
Biblia inatuagiza kulia na wanaolia na kufurahi na wanaofurahi. Sasa wewe sijui umetoka shimo gani na kukurupuka na mada hii. Kuna shida gani kumpongeza aliyepata kitu chema?. Maana neno la Mungu lasema apataye mke apata kitu chema naye atapata kibali kutoka kwa Mungu. Naona wewe ni mjukuu wa Ismael pole sana.
 
Kwani lazima uchangie?we kama hutaki kuchangia usichange nakushangaa unaleta mada ya kijinga kama hii
 
Mleta uzi, inaonekana wewe umeshaoa siku nyingi bila kufuata utaratibu rasmi, sasa ynaona wanaotaka kuoa kwa utaratibu rasmi wanakusumbua.

Anyway, kuwachangia sio lazima, ukipewa kadi usipeleke mchango, ukialikwa kwenye kikao usiende. Lkn kumbuka kuna siku utahitaji watu wakuchangie michango.

Vv
 
Mie nimefunga ndoa huku nikiwa nimepanga bajeti yangu 1.5M. Nikawatarifu ndugu, marafiki, jamaa na majirani kwa sms na kuwapigia simu.
Kiukweli hata mmoja sikutaka kuomba mchango maana bajeti yangu niliipanga vizuri. Hakuna kwenda ukumbini wala nini na kama ujuavyo ndoa za Kiislam NYINGI zinafanywa simple sana.
Niliowataarifu walinichangia 2M wakati sikuomba mchango hata kidogo. Mtu tu na utoaji wake mkuu. Kwako ni kero lakini kwa wengine wanaona heshima kwamba umemzingatia kwamba kwenye suala lako pia yeye anaweza kuwa na impact.
 
Pili bila shaka wewe ni muslim,mana nyie ndoa hata ukiwaambia watu kuanzia asubuhi kwamba unaoa saa mbili usiku nyie ni poa,ila kristos ndoa zao ni process,then naomba umuulize baba yako,alivyofunga ndoa alichangisha au? Labda ndoa iwe ya mkeka

Na kama sio Muislamu je, mchango wako kwenye hii mada utakuwa na maana yoyote? Otherwise ni chuki ya kidini tu.

Vv.
 

Duuuuuuuuu!!!! sio uongo, nikweli,sasa wanavyo sumbua michango je? Kitandani twapanda wote?
 
Kwanza naomba nimuite mtoa mada MPUMBAVU uliyeelimika kwa shida sana na ukashindwa kuitumia elimu yako vizur...swala la kuchanga harusi ni utaratibu tuliojiwekea watanzania na tunautekeleza kwa moyo mmoja kama huupendi kaishi kenya hamna kuchangia harusi!! Ujue ipo siku na wewe utahitaji hii support kwa njia moja au nyingine,utayakumbuka haya maandishi yako kuwa hutak kuchangia harusi.

Usiniwaze kama huwezi kujiwaza.
 
Duuuuuuuuu!!!! sio uongo, nikweli,sasa wanavyo sumbua michango je? Kitandani twapanda wote?
We nawe kilaza umekurupuka..michango ipo miaka mingi sana na sijawahi kusikia mtu analalamika kuwa kachapiwa mkewe kisa kuchangiwa harusi...utakuwa wa kwanza wewe na ntamvizia mkeo njoo unchangishe kama unaona unaloongea ni sawa..changa harusi za wenzako acha ujinga.

Usiniwaze kama huwezi kujiwaza.
 
Mimi nipo tofaut kidgo.
Kwa destur yetu Watanzania ni watu wakirimu na kupenda kushirikiana. Ni jambo jema kupeana saport katika shida na raha

Tuache ubinafsi na kudopt maish ya jamii zingine
 
Kushrikiana kwenye furaha na hudhuni ni utamaduni wetu bahati mbaya hawa waliogeuza biashara sherehe za wenzao ndio wanao tuharibia mkuu. Unajua hata hiyo mil 1 inatosha kabisa kwa sherehe ya harusi tatizo huwa lipo kwa wanakamati.
 

Huo utaratibu ni upi?kuchangisha watu?. Michango ya watu ntaihitaji ila sio michango ya harusi.
 
Pili bila shaka wewe ni muslim,mana nyie ndoa hata ukiwaambia watu kuanzia asubuhi kwamba unaoa saa mbili usiku nyie ni poa,ila kristos ndoa zao ni process,then naomba umuulize baba yako,alivyofunga ndoa alichangisha au? Labda ndoa iwe ya mkeka

Mimi ni mkristo. Hizo process ni zipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…