Kuna watu wa ajabu sana,unapanga kuoa huku huna hela unataka watu wengine wakuchangie,huu ni ujinga mkubwa.
Raha zako ziwape wengine shida.
Unakuta mtu anataka kuoa,bajeti milioni 10, yeye ana milioni 1 na nusu,hizo zinginge anataka watu wamchangie, ukipanga kuchangiwa harusi jiandae pia kuchangia mke.
Acheni kusumbua watu na harusi zenu.
Katika masuala kama haya ni vema kutumia busara zaidi. Ukienda kama unavyosema tutafika mbali kwenye tafsiri. Harusi yake na raha zake, kwa hiyo abebe mzigo mwenyewe. Kwani kuna vingapi vinavyokuhusu ambavyo umechangia na wenzako?
Siku ukiuguliwa utahitaji msaada? Mgonjwa si ni wako mwenyewe?
Siku ukifikwa na msiba (kufiwa) utahitaji msaada? Marehemu si alikuwa ndugu yako peke yako?
Siku ukivamiwa na majambazi, utahitaji msaada? Nyumba hiyo na mali si vyako mwenyewe?
Siku ukioa/olewa ama kuozesha utahitaji msaada?
Na kwenye msaada tusiwaze pesa tu, maana najua ndio msingi wa uzi huu. Kama tukianzisha ubinafsi kwenye pesa, haitaishia hapo, inabidi tuwe wabinafsi hasa, yaani tusishirikiane katika mambo yote maana lako halinihusu na langu halikuhusu wala halimhusu yule mwingine.
Hali hiyo na maisha hayo nakuachia mtoa uzi ishi peke yako na wengi(ne) wanaokuunga mkono. Kama unajitosheleza kwa kila jambo hakuna shaka kabisa, uamuzi huo ni halali yako kabisa. Mimi jitajitahidi kuchanga pale nitakapoweza, nikishindwa nitajua nimeshindwa na mhusika nitamtafadhalisha atambue hali si shwari. Na mimi yakinifika, nitaomba msaada, na ushirikiano si katika raha tu, hata majanga pia.
After all, sina hakika kama ni sahihi kusema 'anataka', nina imani
anaomba wamchangie na washirikiane naye. Kama huwezi au hutaki tu huwa hakuna kesi baada ya hapo.
Unayo haki ya kukataa.