Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Jaji hujanielewa sijui...mimi niliomba kwa wazazi sitaki harusi kubwa na waliokuja wanawajuwa wao hao watu ambao sijawahi waona ...mimi kuchanga ni ndugu tena wa karibu.kama sikujui...sijawahi kukusikia hamna sababu ya mimi kuchanga sababu sitokuja.hii ni kwa upande wangu mimiMalogi76 wewe harusi yako ulichangiwa?
Okay,nimekifunza kitu,ukishapita hiyo hatua huoni sababu ya kuchanga kwakuwa unaye mwenza!
Basi waache vijana wachangishane
Aamin, Aamin, Aamin. Niseme kweli, kama ilivyo kwako; kwangu pia nuru mpya imeng'ara katika maisha yangu kwa hayo uliyoeleza hapa nimepata nguvu mpya na afya mpya kiroho.
Mimi huwa nawashangaa sana watu wakikaa vijiweni na kusema "binadamu wabaya" mara utasikia "ooh Dunia hii hakuna wa kukusaidia zaidi ya ndugu yako" n.k n.k mimi huwa nawasikiliza tu na kusema; Hakika atakayekufaa kesho humjui kwasababu mimi mwenyewe nimewasapoti watu ambao siwajui na hata nikionana nao kesho hawatanikumbuka wala sitawakumbuka.
Kitu kikubwa pia nilichojifunza maishani mwangu ni kuwa tenda wema na usisubiri shukurani. Malipo ya wema wa aina hii hulipwa na Mwenyezi MUNGU mwenyewe kwako mwenyewe au hata kwa kizazi chako. Maajabu ya wema ulioufanya utaanza kuyaona ukiwa na shida, utashangaa watu wa kukusaidia wanajitokeza tu bila hata kujua wametokea wapi tena huwajui na cha ajabu zaidi hawahitaji malipo kutoka kwako!!! Kanuni ya wema ni ya ajabu sana sana sana.
Kubwa zaidi tukumbuke kuwa tunavotenda wema ni tunatimiza kusudi la Mwenyezi MUNGU. Tujifunze kuwa unapotenda wema huwenda ukawa umefanya muujiza mkubwa sana kwa yule uliyemtendea bila hata wewe kujua. Kwa wema wako huenda yule uliyemtendea akakesha usiku kucha akimshukuru Mwenyezi MUNGU kuwa amemjibu maombi yake!!! Sote Hatujui lakini huwenda mtu uliyemsaidia aliomba Mwenyezi MUNGU amsaidie jambo, nawewe ukajitokeza ukafanya lile lile kama alivoomba kwa mwenyezi MUNGU! Tazama jinsi mtu huyu atakavomshukuru Mwenyezi MUNGU kwa kumjibu maombi yake. Kifupi ni kuwa kila mmoja hapa duniani katumwa na Mwenyezi MUNGU aje atimize kazi fulani alizopangiwa lakini wengi wameamua kufuata mambo yao wenyewe yanayowafurahisha wao na nafsi zao bila kujali walichotumwa na Mwenyezi MUNGU ndio maana harusi wanachangia 50,000/= lakini kwa mgonjwa na mwenye shida anatoa 500! Ni vitu vya ajabu sana vinatendeka hapa duniani hadi vinachekesha na kuhuzunisha.
Kwakweli mimi nishajisemea moyoni mwangu kuwa kwenye haya mambo ya kipuuzi ya sherehe zisizo na maana watu wanatumia milioni kumi kwa siku kwa kula na kunywa hawataniona kamwe na nipo tayari kulaumiwa na hata kutengwa maana ninajua kuwa watakaonifaa si hawa ninaowadhania bali Mwenyezi MUNGU ataniletea watu nisiowajua na hata kunizika watanizika. Napenda sana niwapate ndugu wa kiroho kama wewe wawe jirani zangu katika maisha yangu maana hata ktk nyakati za huzuni watanipa faraja ambayo pengine singeipata mahali pengine popote.
Kuchangia harusi hulaziishwi. Kuna watu wanapenda kuchangia harusi na usipowachangisha hawaji kwenye harusi yako. Hapo vipi?Habari ya leo wadau,
Hivi hii issue ya kuchangishana hela ili watu wafanye sherehe kuuuuuubwa ya harusi itaisha lini? Jamani zama zimebadilika hivyo yatupasa hata na sisi tubadilike pia, hali sasa hivi ni ngumu jamani si utani, mbaya zaidi unapangiwa kabisa kuwa kima cha chini ni kiasi flani cha fedha, tunatafutana ubaya ujue, ifike mahali furaha yako isiwaumize wengine.
Kama issue ni kufunga ndoa wewe nenda kwa Mchungaji/Paroko mueleza azma yako ya kufunga ndoa hivyo andaa fungu lako kodisha mapaparazi/wapiga picha tafuta sehemu tulivu ambayo mtaenjoy na baadhi ya mashuhuda, maliza mchongo bila kuwapa watu stress, kwa kufanya hivyo utakuwa umeepusha ndoa yako na manung'uniko ya watu, maana kama mjuavyo binaadam hawariziki utasikia mara oooh! pamoja na kuchangishwa fedha nyingi sherehe yenyewe ilikuwa na mapungufu kibao.
Hapa sasahivi tayari nina kadi za mchango 8 mpaka wengine hata siwafahamu, sasa najiuliza nitamchangia yupi nitamuacha yupi.
Nawasilisha.
Kwani ili uwe umefunga harusi lazima wao wawepo??? What if wamechangia halafu siku moja kabla ya harusi akafa je harusi yako haitafungwa kwasababu yy hayupo? Ishi unavoona inafaa, usiishi vile watu wanaona inafaa.Kuchangia harusi hulaziishwi. Kuna watu wanapenda kuchangia harusi na usipowachangisha hawaji kwenye harusi yako. Hapo vipi?
yani siwamalizi nikikumbuka najiuliza mengi jibu sipati..Hahahaah hao wametisha aisee....
Sahihi kabisa ni bora ufanye harusi uliyo na uwezo nayo,kuliko kutegemea michangoMi kwasasa wanosahau kabisaaaaaa. Nachangia ndugu yangu, na mtu ninaefanya nae kazi Idara yangu tu. Aidha, harusi yenye pombe sichangii kabisa, siwezi kuchangia pesa yangu watu wakanywe pombe, ila kama mtu ni wa karibu sana na mimi nitampa zawadi baada ya harusi ambayo ni equivalent to mchango ambao ningeutoa.
Vilevile nawahusia vijana, msipende kuchangiwa harusi, kumbukeni kuwa hayo ni madeni!!! Zitakavoanza kujia kadi mfululizo usilalamike kama na ww ulichangisha watu
Kwa kusisitiza ni kuwa, mimi pia watoto wangu nitawafanyia sherehe kwa kuangalia uwezo wangu, sio kusumbua watu michango isiyo na tija. Nitawakaribisha ndugu na rafiki wa familia yangu, sio kuita watu weengi hata ambao hawana hata uhusiano na familia. Ni upuuzi usio na maana.
Hatuishi ndani ya box tunaishi na jamii. Mchango kama watu wanajitolea kuna ubaya gani? Wapo watu wakiambiwa wachange wanakataa hamna kosa ni ombi, kuna wengine wanapenda kuchangia tu utakataa uwaambie sitaki michango yenu?Kwani ili uwe umefunga harusi lazima wao wawepo??? What if wamechangia halafu siku moja kabla ya harusi akafa je harusi yako haitafungwa kwasababu yy hayupo? Ishi unavoona inafaa, usiishi vile watu wanaona inafaa.
Thank you.....@Madam Mwajuma umefungukabado hizo mambo zinawaendesha?? can't you have your own stand econimically! changia issue za muhimu na sio misherehe ya watu siju alipokuwa jirani wa binadam wa mdogo wa rafiki wa mpangaji mwenzako ukiwa chuo ambaye ni mke mdogo wa mkewe wakufijia[emoji3] [emoji3]
Thank you.....@Madam Mwajuma umefunguka
Haaaaaa mbavu zangu mimi [emoji106]bado hizo mambo zinawaendesha?? can't you have your own stand econimically! changia issue za muhimu na sio misherehe ya watu siju alipokuwa jirani wa binadam wa mdogo wa rafiki wa mpangaji mwenzako ukiwa chuo ambaye ni mke mdogo wa mkewe wakufijia[emoji3] [emoji3]
Haaaaaa mbavu zangu mimi [emoji106]
Mkuu vp na ww ushagoma kuchangia hiyo mambo sio?Haaaaaa mbavu zangu mimi [emoji106]
Kweli kwa hali ya sasaivi kila kukicha mahitaji yanaongezeka na mishahara ipo pale pale,mimi nililetewa card ya harusi mchango laki5 au kuna list ya vitu uchague ukanunue ulete,fridge,cooker,kuweka mapazia,Sofa tena wamekwambia
ukisha chagua watakuelekeza wapi ukanunue,na hao watu hata wenyewe hawapikii gas wanapika na mkaa
nikasema wanatukomoa kila aliepewa card ya mchango wa hiyo harusi walisema mie ntakua nje ya nchi,wengine
sijui watakua makazini,nikasema ivi mtu unampa kiwango cha mchango atoe kwani ni harusi yake?
Ningekuwa m/kiti wa kamati hlf michango ikafikia mil 20 nawashauri tu wanakamati tuandae shughuli ya mil 2 hlf fedha iliyobaki mil 18 tunamnunulia bwana harusi kiwanja cha mil 5 na material ya ujenzi akaanze maisha.eeehhh watu wanalazimishaga utafikir wanajua unazalisha kiqsi gani changia kwa hesabu nawe ukifanya yako fanya inayoendana na uwezo wako nikujikomoa tu unaishi nyumba yakupanga unafanya sherehe ya mil 20? foolish baadae eti Magufuli kabana umeshindwa kujenga[emoji15]