Habari ya leo wadau,
Hivi hii issue ya kuchangishana hela ili watu wafanye sherehe kuuuuuubwa ya harusi itaisha lini? Jamani zama zimebadilika hivyo yatupasa hata na sisi tubadilike pia, hali sasa hivi ni ngumu jamani si utani, mbaya zaidi unapangiwa kabisa kuwa kima cha chini ni kiasi flani cha fedha, tunatafutana ubaya ujue, ifike mahali furaha yako isiwaumize wengine.
Kama issue ni kufunga ndoa wewe nenda kwa Mchungaji/Paroko mueleza azma yako ya kufunga ndoa hivyo andaa fungu lako kodisha mapaparazi/wapiga picha tafuta sehemu tulivu ambayo mtaenjoy na baadhi ya mashuhuda, maliza mchongo bila kuwapa watu stress, kwa kufanya hivyo utakuwa umeepusha ndoa yako na manung'uniko ya watu, maana kama mjuavyo binaadam hawariziki utasikia mara oooh! pamoja na kuchangishwa fedha nyingi sherehe yenyewe ilikuwa na mapungufu kibao.
Hapa sasahivi tayari nina kadi za mchango 8 mpaka wengine hata siwafahamu, sasa najiuliza nitamchangia yupi nitamuacha yupi.
Nawasilisha.