Kuna siku nimealikwa kwenye kikao. ..majamaa yana pleage kwa sifa sifa balaa ikantoka 1.4 ya M
Hahaha
Nime Left ma Group ya whatsup kisa hiyo michango
Aisee kweli bhana,ukiweka cha maana ujue chako hichoTena siku hizi hizo whatsap groups ni upuuzi mtupu. Hakuna hata cha maana.
-Kaveli-
Aisee kweli bhana,ukiweka cha maana ujue chako hicho
Sitoi tena mchango wa mtu.Kwa usawa huu wacha tuwe wabahili
Sijui nani aliingiza kwenye jamii yetu upuuzi huu. Kama mtu huwezi kufanya sherehe from your own resources si uache,why should you inconvenience other people,mbona sherehe sio lazima. Mimi niliacha kuchanga hovyo hovyo. Nachanga tu kwa watu wa karibu sana,but I continue educating them.Hii Kitu nilitaka kuipost hapa miezi kadhaa iliyopita sema nikasahau, leo kuna jamaa kanipigia anataka nimtumie dolali za mchango wa harusi ya binamu yake ambaye hata simjui wala sijawahi msikia.
Tuendelee:-
Wakuu hii kitu bado bongo ipo tena siku hizi ni project kubwa na za garama ya juu.
Watu wanakutana kila wiki mara moja kwenye baadhi ya bar, wanakunywa na kusaza katika hivyo vikao vya maandalizi, vikao hivyo huchukua miezi miwili hadi mitatu. Na katika vikao hivyo watu hutoa ahadi ya kiasi cha fedha watakachotoa kwa ajili ya harasi, wanaume hutoa michango ya bachela parti na harusi kuu, na kina dada hutoa michango ya sendi off, bridoshawa, kichenipati, na harusi kuu.
Kwa kifupi zoezi hili linakula hela nyingi sana, nimeambiwa sometimes you can be asked to contribute to more than 10 wedding a year, na ukitoa chini ya laki moja unaonekana mtu wa hovyo hovyo.
Jamani ndugu zangu naombeni mwongozo mimi naona kama hii ni too much.
Badala ya michango ya vikao vya harusi basi tuihamishie kwenye Elimu na Matibabu.
MJ
====================
Yaani mie nisingetoa hata 10......Wadau habari???
Hii michango ya Harusi sasa jamani ni matatizo na kuleteana umasikini tu.
Sahivi ajira hamna, wengine tumebahatisha tu vikazi kwa watu ili tutafutie mitaji ya kutafutia Pesa tuendeshe maisha ya baadae, tulipe na madeni ya wanaotudai, nk.
Sasa jamani, hapa ndo hvo nimepata KAZI ndo mwez umekatika, siku hiyo nimereport kazini kulikuwa na kikao cha harusi ya walimu wawili wanataka kuoana.
Khs michango wakapanga kila teacher atoe kuanzia elf 50 ahead kwa akili ya send off ya muolewaji ma harusi ya muoaji.
Ok, nimekubali nitatoa, hiyo sawa nitatoa.
Lililonikereketa sasa, pamoja na kwamba sijatoa hilo deni la harusi, juzi tena naletewa kadi ya mchango kwa ajili ya kitchen party ya muolewaji huyohuyo. Tena kwa msisitizo kwamba kiwango cha chini cha mchango kiwe 30 elf.
Na haka ka salary jamani, michango yote hiyo!!!!!!!!! jamani mtuhurumieni aiseee. Sio vizuri mda mwingine. Maisha haya sahivi magumu jamani kwa mwananchi ambaye kujulikana ktk nchi yako ni hadi miaka mitano.
Tuhurumieni aiseeeeee!!!!!
Yaan ndo hata sijawaza kutoaYaani mie nisingetoa hata 10......
Kwanza ukinipangia kiwango ujue hata kama nilitaka kichangia sichangii tena