Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Kuna siku nimealikwa kwenye kikao. ..majamaa yana pleage kwa sifa sifa balaa ikantoka 1.4 ya M


hahahahaa Mkuu umenichekesha sana Mkuu.

Izo swagga za 'pledging' huwa zinazuzua sana watu kwenye mikusanyiko. Kutaka sifa.

-Kaveli-
 
Tubadilike watanganyika tuweke hiyo hela kwenye vitu vya maana si kwa ajili ya kuponda kwa pombe na vyakula pamoja na muziki.
 
michango ya harusi inaelekea ukomo, japo itachukua muda. fomu au kadi za michango kwa wasio wanakamati zimetoweka, sherehe imebaki ya kamati kuu, wazazi na washehereshaji. hali ya pesa ngumu, na watu wametambua majukumu muhimu kama elimu na tiba ambayo bila pesa hayafanyiki, ndoa unaweza ikamilisha bila michango. unawahi asubuhi kanisani na mashahidi wako na mnarudi nyumbani mnatembea.
 
mimi sichangi kama anayeoa au kuolewa simfaham.juz kati jamaa mmoja tunafanya nae kibarua ofisi moja,hata yeye hatupo close lakini kanipa kadi eti kaka yake anaoa halafu harusi inafanyikia nje ya mkoa tuliopo,nilishangaa sana, kwanza kaka yake simfaham pili harusi yenyewe inafanyikia mkoa mwingine,niakamwambia siwez changa mana harusi inafanyikia mkoa mwingine akanuna hata salamu ikawa tatzo.haya mamichango yatatucost sana.
 
Hii Kitu nilitaka kuipost hapa miezi kadhaa iliyopita sema nikasahau, leo kuna jamaa kanipigia anataka nimtumie dolali za mchango wa harusi ya binamu yake ambaye hata simjui wala sijawahi msikia.

Tuendelee:-

Wakuu hii kitu bado bongo ipo tena siku hizi ni project kubwa na za garama ya juu.

Watu wanakutana kila wiki mara moja kwenye baadhi ya bar, wanakunywa na kusaza katika hivyo vikao vya maandalizi, vikao hivyo huchukua miezi miwili hadi mitatu. Na katika vikao hivyo watu hutoa ahadi ya kiasi cha fedha watakachotoa kwa ajili ya harasi, wanaume hutoa michango ya bachela parti na harusi kuu, na kina dada hutoa michango ya sendi off, bridoshawa, kichenipati, na harusi kuu.

Kwa kifupi zoezi hili linakula hela nyingi sana, nimeambiwa sometimes you can be asked to contribute to more than 10 wedding a year, na ukitoa chini ya laki moja unaonekana mtu wa hovyo hovyo.

Jamani ndugu zangu naombeni mwongozo mimi naona kama hii ni too much.

Badala ya michango ya vikao vya harusi basi tuihamishie kwenye Elimu na Matibabu.

MJ

====================
Sijui nani aliingiza kwenye jamii yetu upuuzi huu. Kama mtu huwezi kufanya sherehe from your own resources si uache,why should you inconvenience other people,mbona sherehe sio lazima. Mimi niliacha kuchanga hovyo hovyo. Nachanga tu kwa watu wa karibu sana,but I continue educating them.
 
Haya majadiliano kuhusu michango ya harusi ni mwanzo mzuri wa mwisho wa jambo hili. Ingawa nia ya kuchangiana ni kujenga mshikamano katika jamii na miongoni mwa wanajamii, hali inavyoendelea michango itachukua sura nyingine haswa pale wengio wanaochanga watakapogundua kuwa wanaokuza mila hii mpya ni wanaofaidika kibiashara na michango hii. Nionavyo mimi michango ya harusi ni chain ya business ya wale wote wanaohusika na huduma mbali mbali za harusi- wenye kumbiza harusi, wapika keki, vinywaji , washona nguo, wenye salon, magari, ma MC etc, . Hawa watapigana sana michango isiishe. Wakati mwingine nawafanansisha hawa na ngariba wa tohara kwa watoto wa kike. Wamejizatiti kuhakikisha haiachwi maana wanafadikika. Matumaini yangu ni kuwa hali ngumu ya maisha itaanza kutunyorosha tuanze kufikiri mambo yaliyo ya msingi na kuacha yasiyo ya msingi. Kikubwa vipaumbele vyetu ni vya ajabu sana. Jaribu kuomba michango ya mgonjwa hakuna watu wengi wa kujitolea omba michango ya harusi wengi watakuchangia. Hivi inaleta akili harusi za million 100 wakati kuna watoto wandugu, jamaa, jirani hawaendi shule hivi hii sio kufuru?Mbona tunaiga sana mambo mengi toka mataifa ya nje ila la harusi ndogo na gharama nafuu hatuigi? mfano kwa Australia, sherehe ya harusi ni swala la mtu binafsi na haizidi watu 20 wanaolikwa hotelini na kujilipia wenyewe. Wataliano na wagiriki wanatabia kama zetu waafrica, harusi kubwa, majumba na magari makubwa ni mawazo ya kiajabau sana. Cha ajabu watu hatuelewi kuwa mtoto mmoja wa jirani ama ndugu asipoenda shule na kukua bila kusoma na kuandika ni mzigo kwetu sisi sote na utatuumiza katika kodi maana mtoto huyu hataweza kuchangia uchumi wa taifa ipasavyo. WaTanzania tubadilike. Hata mimi sichangii harusi badala yake ninatoa elimu kwanini si lazima ingawa unakuwa very unppular na sometimes hat andugu wanakukimbia ninachangia misiba na elimu lakini harusi nimeacha sisi tulio kwenye mapambano ya kupiga vita harusi kubwa na michango ya harusi tuanze kuonyesha mfano kwa kuwa na harusi ndogo pale inapohusu watoto ama ndugu zetu. makanisa na misikiti ingiliane kati na mhamasishe harusi zifungwe kanisani/misikitini na sherehe zifanywe za jumla misikitini. yyako makanisa yameanza vipaimara vinafanywa pamojo na kwa gaharma nafuu.
 
ukitoa toa tu ilimradi usionekane mchoyo unaweza kuta unatoa nusu ya mshahara wako au kipato chako hapo bado hujaanza hata kupanga matumizi na saving na mengine
 
Wadau habari???

Hii michango ya Harusi sasa jamani ni matatizo na kuleteana umasikini tu.

Sahivi ajira hamna, wengine tumebahatisha tu vikazi kwa watu ili tutafutie mitaji ya kutafutia Pesa tuendeshe maisha ya baadae, tulipe na madeni ya wanaotudai, nk.

Sasa jamani, hapa ndo hvo nimepata KAZI ndo mwez umekatika, siku hiyo nimereport kazini kulikuwa na kikao cha harusi ya walimu wawili wanataka kuoana.
Khs michango wakapanga kila teacher atoe kuanzia elf 50 ahead kwa akili ya send off ya muolewaji ma harusi ya muoaji.

Ok, nimekubali nitatoa, hiyo sawa nitatoa.
Lililonikereketa sasa, pamoja na kwamba sijatoa hilo deni la harusi, juzi tena naletewa kadi ya mchango kwa ajili ya kitchen party ya muolewaji huyohuyo. Tena kwa msisitizo kwamba kiwango cha chini cha mchango kiwe 30 elf.

Na haka ka salary jamani, michango yote hiyo!!!!!!!!! jamani mtuhurumieni aiseee. Sio vizuri mda mwingine. Maisha haya sahivi magumu jamani kwa mwananchi ambaye kujulikana ktk nchi yako ni hadi miaka mitano.

Tuhurumieni aiseeeeee!!!!!
 
Ni nonsense kwakweli..unakuta familia inafanya harusi ya mil 20 wakati kwenye ukoo kuna watu wameshindwa kusoma kwa kukosa ada yani haileti logic kabisa..ifike wakati huu utaratibu uelekezwe kwenye mambo ya msingi..pia fanya harusi kwa uwezo wako sio unapeleka kadi ya mchango mpaka kwa bekitatu wa nyumba ya jirani
 
Huku kwetu uswahilini mtoto akizaliwa mchango, akifikisha siku 40 mchango,akifaulu mchango,akimaliza shule kwenye graduation mchango
 
Wadau habari???

Hii michango ya Harusi sasa jamani ni matatizo na kuleteana umasikini tu.

Sahivi ajira hamna, wengine tumebahatisha tu vikazi kwa watu ili tutafutie mitaji ya kutafutia Pesa tuendeshe maisha ya baadae, tulipe na madeni ya wanaotudai, nk.

Sasa jamani, hapa ndo hvo nimepata KAZI ndo mwez umekatika, siku hiyo nimereport kazini kulikuwa na kikao cha harusi ya walimu wawili wanataka kuoana.
Khs michango wakapanga kila teacher atoe kuanzia elf 50 ahead kwa akili ya send off ya muolewaji ma harusi ya muoaji.

Ok, nimekubali nitatoa, hiyo sawa nitatoa.
Lililonikereketa sasa, pamoja na kwamba sijatoa hilo deni la harusi, juzi tena naletewa kadi ya mchango kwa ajili ya kitchen party ya muolewaji huyohuyo. Tena kwa msisitizo kwamba kiwango cha chini cha mchango kiwe 30 elf.

Na haka ka salary jamani, michango yote hiyo!!!!!!!!! jamani mtuhurumieni aiseee. Sio vizuri mda mwingine. Maisha haya sahivi magumu jamani kwa mwananchi ambaye kujulikana ktk nchi yako ni hadi miaka mitano.

Tuhurumieni aiseeeeee!!!!!
Yaani mie nisingetoa hata 10......

Kwanza ukinipangia kiwango ujue hata kama nilitaka kichangia sichangii tena
 
Amani iwe kwenu waungwana

Mtu ukimwelewesha hakuelewi hadi kujenga chuki kisa mchango wa harusi, msema kweli mpenzi wa Mungu Kwa mwaka huu sitachangia mchqngo wowote wa harusi, tafadhalini hali mbaya,

Mtaniwia radhi aiseeee, mambo yamebqna mpaka kooni,
 
Da bora na wewe umeliona hapa nina kadi 4 kuanzia mwez wa sita mpaka w nane na zitaka pesa ya kutosha tu.
 
Back
Top Bottom