Jana kwangu ilikuwa siku nyingine ya kufurahia kuwa sehemu ya member wa jamii forum. Hii ilitokana mwanajamii mmoja
nzagambadume kupost link ya kitabu kilichoandikwa na mlinzi wa raisi Kagame aliyekimbilia UK kuepuka kifo kilichokuwa tayari mlangoni mwake.
KWA NINI NAMTAJA KIKWETE NA MEMBE
Kwanza ijulikane wazi kuwa Watanzania wengi tulifahamu kuwa Kikwete alikuwa raisi mpole na kufikia hatua ya tukamuita raisi dhaifu aliyezungukwa na marafiki wabaya (walio na hulka ya kujinufaisha wao na familia zao). Nakumbuka nikiwa navuka Mtukula kwenda Kampala siku hiyo sitausahau hasa baada ya kukuta kundi la raia wa Rwanda wakiwa na mizigo yao wakifurushwa kurudishwa Rwanda bila kujali walikuwa na mifugo au makazi,wameoa Watanzania au Watanzania wamewaoa walilazimishwa kurudi makwao kwa amri ya raisi Jakaya Kikwete!!.
Pale mpakani alikuwepo mama mmoja na mwanae wamelala kandoni kidogo mwa barabara huku mtoto akiwa na hali mbaya bila nguo ndipo utu wa Kitanzania niliuona pale kwani yule mama kama alitoka hapo basi hatasahau maisha yake yote kwani alichangiwa na abiria wa Kitanzania kwa kupewa vyakula, nguo na pesa na katika basi gumzo ilikuwa Kikwete ana bifu na Kagame lao binafsi lkn limesababisha hadi wasiohusika wanataabika ukweli hata mimi nilikuwa mmoja wa waliokuwa wanamshutumu raisi. Tulienda mbali kwa kusema huu ukatili si angeuelekeza kwa wezi walioko serikalini mwake lkn msimamo wa Kikwete ulikuwa palepale na hadi anatoka madarakani sikumbuki kama Kikwete alishawahi kwenda ziara Rwanda.
MEMBE ambaye alikuwa mtu wa karibu wa raisi Kikwete wengi tulijua ni usalama wa Taifa (TISS) hivyo tulifahamu kuwa linalotokea baina ya Tanzania na Rwanda basi kwa namna moja Membe alikuwa anafahamu tukizingatia kuwa alishakuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka kadhaa.
KITABU CHA NOBLE MARARA
Kitty hiki ukianza tu kukisoma sio tu utastaajabu usiyoyafahamu kuhusu Kagame ila utashangaa kwa nini tuna urafiki na mtu dizaini hii (Kagame na Rwanda). Kitabu kimemweka wazi Kagame maisha yake,tabia yake,ukatili wake,namna anavyosuka mipango ya mauaji na namna anavyoplan kujisafisha namna alivyokuwa anazini na wake za watu wake wa karibu akiwa analindwa na ma body guards wake!!
Mtu anayeandika kitabu hiki kumbuka ni mtu aliyekuwa anamlinda Kagame kuanzia asubuhi gadi asubuhi nyingine, yeye mwenyewe kashiriki mauaji akifikiria anailinda Rwanda na Kagame kumbe ni chuki na kujiimarisha tu kwa Kagame rafiki wa karibu wa Tanzania kwa sasa!! Hadi anatoroka alikuwa tayari yuko kwenye target za Kagame
Katika haya maelezo mafupi sana nimeelewa sasa kuwa Mh. raisi Mstaafu Kikwete alibaini na kujilidhisha pasipo shaka kuwa urafiki na huyu mtu sio kabisa hasa baada ya majeshi ya Tanzania kuwapa kichapo M23 jeshi katili la Kagame kipindi hicho huko DRC
Sent using
Jamii Forums mobile app