Umempa Yesu maisha baada ya huo muujiza? His concern is the salvation of your spirit hayo mengine ni incentive tu za kukupa mbegu ya Imani ila kuzaa kwa mbegu itategemea imepandwa kwenye udongo gani, some zinaangukaga njiani ndege wanaokota hao ndege nimewaona wengi hapa JF wakisha iokota utaona kidogo kidogo ile value ya huo ushuhuda inapungua as days proceed, wakati mwingine inaangukaga kwenye miiba utaanza visingizio ooh leo sitaki kusikiliza mahubiri maana ninakazi nyingi na ile ari na viapo ulivyovitoa kwa furaha ya kuona mkeo amepona inaanza ku fade away taratibu....So if you continue with your humble heart ya kusikiliza wenye habari njema zaidi ya huo mchungaji kuna package mbali mbali zaidi ya healing miracle utaendelea kupokea na ukifungua huko ndani utakuta peace, financial break through, opportunities, right people to take you to your destiny earlier than you could imagine etc ndiyo hapo inapoanguka kwenye udongo mzuri moja huzaa mia, nyingine sitini na nyingine thelathini. Cha msingi ni kuwa huyo mkeo hajapokea uponyaji wake tu kama kweli huyo ni mtumishi wa Mungu lakini pia na anointing ya kutibu wengine wenye shida kama yake so aanze kutumia hiyo karama ili kuichochea kila anapokutana na mwenye hitaji ndiyo maana Yesu akasema kama baba alivyonituma nami pia ninawatuma kupeleka hii habari njema kwa mataifa ili nao wapate kupona....
I hope umenipata na ubarikiwe sana.
matibabu anatoa kuanzia saa ngapi hadi saa ngapi; kama umati ni mkumbwa watamchosha mzee wa watu.
Nadhani mafisadi wanamtamani sana saa hii; nafikiri hadanganyiki wangesha mpora hati miliki.
Felister! Yesu ni kila kitu kwangu na kwa familia yangu. Mimi naamini na familia pia maombi ya rohoni zaidi kuliko wapayukao! Roho husema kweli zaidi kuliko mdomo. Ni wachache sana wanayoyaongea yanakuwa yanatoka katika roho ya kweli. Wengi wao ni wasanii. Roho wa kweli humwomba baba yake yaliyo ya kweli. Tunashuhudia kila uchao kuna wanaojiita mitume! wanawachanganya sana waumini wao nao kwa kupiga makelele mengi huwafanya wote wenye shida kuamini kila wasemacho mwisho hujikuta wako wenyewe.
Iaminike kuwa kila mtu anayo imani yake, kwa diini yake basi na tuwape watu uhuru wa kuamini kile waaminicho ambacho lengo lake ni kumfikisha kwa muumba wake. Usitake kila mtu aamini kile wewe uaminicho ni sahihi, la hasha ila wewe onyesha kuwa huo ni muono wako na ni ushauri tu! Tufike mahali tuheshimu dini ya Felister hali kadhalika Musa au eeka mangi aheshimu uabudi wa Felister.
Nikutakie kila la kheri katika maisha yako ya kila siku.
kwanza jina lako linanipa utata-maana lenyewe ni ugonjwa tayariKwa wale wataalamu wa magonjwa ya akili wanaweza kugundua mambo mawili muhimu hasa kwa jinsi anavyojieleza.
1.grandiose delusion-ile hali ya kujikweza ati yale majani lazima ayaombee yeye ili yaweze kukutibu.
2.hallucination-eti mungu alimuonyesha noti ya 500 na hivyo hii ndio bei ya matibabu.
Mwenye masikio na asikie,huyu mtu ni mgonjwa na anahitaji tiba haraka iwezekanavyo.
Inawezekana wewe ni yule niliekwambia hakuna mwanamke atakaye kukubali kutembea nje ya ndoa na kila uliye naye ambaye si mkeo atazua ugomvi muachane, kwa amri hii ni mpaka milele umechoka kukaa kwenye kifungo au hahaaaaaa! Kama ndiye aise siku hizi nakosa wakuchat naye hapa kwenye baridi..hamjambo huko? Wawekee huo ushuhuda basi nipate wateja wakuamini jina la Yesu......
Je hiyo dawa inatibu kweli?
kwanza jina lako linanipa utata-maana lenyewe ni ugonjwa tayari
Pili huyu mr wa loliondo kwa sasa yupo juu-watu hawawez ambiwa kitu wakaelewa-tusubiri kwanza kama kutakuwa na udanganyifu anaofanya utajulikna tu-ngoja tufanye TRIAL&ERROR
dawa gani hiyo inayotibu kisukari,ukimwi,b.p kwa pamoja
haya magonjwa ni tofauti sana na visababishi vyake ni tofauti, kamwe haiwezi kutibu yote haya.
mimi naibeza kazi yake!kama amegundua dawa afuate taratibu,aende muhimbili kuna kitengo cha traditional medicine aeleze jinsi inavyofanya kazi,dose,inaingiaje na kutokaje mwilini,madhara yake(side effects),inaingiliana vipi na dawa nyingine(interaction with other drugs),inatumikaje kwa makundi maalum mfano watoto,wazee au wajawazito.mie naamini kuwa imani inauwezo mkubwa ikiwa watu wanaamini watapona basi tuwasikilizie. tusiibeze kazi ya mtu!