Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Unajua tusimlaumu mtu yeyote kuhusu ili .Huyu marehemu Mungu alikuwa kabisa anamtaka na alijua kama akipata dawa atapona wakati siku zake zimeisha . Basi Mungu akaamua kuchelewesha na kumchukua mtu wake. Mungu akikuhitaji ni vigumu kukwepa hata kama una kila kitu.
 
title na content vinatofautiana. hata hivyo umbali toka arusha hadi kwa babu ni kama 400km na barabara ni mbaya sana sana, mazingira ya kwenda ni magumu 'one way' ni masaa 6 pia wenye magari wanafanya biashara hawawezi kutoza mia tano au elfu moja, hata hivyo wanapata super profit.
 
Picha za pilikapilika za watu wakijaribu kupata tiba za magonjwa sugu maeneo ya Loliondo:
GARI%2BLA%2BMANISPAA%2BNDANI%2BYA%2BMCHUNGAJI.JPG

magari%2Bwakinywa%2Bdawa.jpg

PICHA%2BMAGARI.JPG

Picha hisani ya Mzee wa Mshitu
 
Serikali iwasafirishe wagonjwa "kama kweli watu wanapona" kuliko kuendelea kugharamia mabilioni ya fedha kwa kununua dawa za kizungu
 
Daa inatia huruma sana kwa kweli..............
 
Naomba kujibiwa swala hili kwa mwenye ufahamu tafadhali. Huyo babu mnasema ni mchungaji/askofu and the like. Na kuwa imani ndio inaponya. Je watu wa dini zingine eg waislamu nao wanaenda? Je wanaoenda nao wanapona wakibaki na imani ya dini zao? Msaada tafadhali

Wailing, Mungu hata siku moja haangalii dini ya mtu; dini ni phylosophy ya kibinadamu zaidi kulinda self interest..Mungu anaangalia moyo uliotayari kupokea na halazimishi mtu kutenda against his will maana amempa binadamu will..ukiwa humble in heart atakufundisha taratibu kujua ukweli wa mambo..Kinyume na Mungu ni shetani yeye mambo yake ni ya kulazimisha na anataka matokeo yawe papo kwa papo ili uwongo wake usigundulike....So dont think about your dini to be a constraint kwani pengine ulijikuta uko kwenye dini kwasababu ya wazazi uliopewa na Mungu huyo huyo so he knows best why you were born in that family....Chamsingi acha moyo wako wazi mbele za mungu naye anajua jinsi ya kukusaidia pale unapoomba kupata solutions to your problems....i ahve helped many Muslims who were ready and humble in heart na hata siku moja sijafanya hivyo kuwa manipulate ili waje kwenye imani yangu najua one day they will come to know the truth; a person can be a muslim by name but full of faith in Jesus in heart and some are christians in names but empty of faith meaning they dont know that they actually are not christians for christianity if more than going to church and participating in all church time tables so let us leave God to judge the living and the dead for He is righteous!
 
Mimi naomba kuuliza huyu mganga anatibu nini maana sielewi? Kuna watu wowote wametoa ushuhuda na tiba yake au ni basi watu kujipanga. Kazi ipo kweli kweli huu mwaka ni mwaka wa matukio
 
Kuna ndugu mmoja( Askofu mstaafu wa K.K.K.T) au maarufu kama Doctor anakaa wilaya ya Loliondo mkoa wa Arusha anatibu magonjwa yote sugu kama Ukimwi,kisukari,magojwa ya moyo,mifupa,ini,figo n.k kwa muda mfupi. Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali za nchi,uarabuni,ulaya wanamimini. Binafsi kuna mzee wangu alikuwa na kisukari amepona kabisa. Bei ya dawa ni shilingi mia tano tu.

Kwa mgonjwa yeyeyote mwenye terminal illness including HIV AIDS akisikia chochote kile kinachohusiana na kunusuru maisha yake ni lazima atataka kujaribu. tufikirie kitu kimoja UKIMWI badi hauna dawa. Hata rais wa Gambia Yahya Jammeh alidai kuwa anatibu UKIMWI ila mpaka leo habari zake zimekuwa kimya kabisa, ninahisi kuwa time will tell tumpe muda huyu mchungaji ukweli utajidhihirisha mbele ya safari.

 
Last edited by a moderator:
NI Mchungaji Mstaafu siyo Askof.

mimi Bado napata shida jinsi anavyotoa huduma yake! Nakosa Imani kama ni nguvu za Kimungu kwani hayo masharti ni balaa
 
Serikali imetuma wataalamu kuchukua vielelezo (sample) vya watu wanaodaiwa kutibiwa ugonjwa wa ukimwi na Mchungaji Ambilikile, mnyakyusa huyu, kwa uthibitisho.

Hii nikufuatia mamia ya watu kumiminika kutoka sehemu mbalimbali kutoka hata nje ya nchi katika kijiji cha Loriondo kupata matibabu kwa Mchungaji huyu. Matibabu ni Tsh. 500 tu.

Leo asubuhi mtaani nimemsikia mtu akisema ndugu yake ametibiwa pia. Let us wait and see.
 
Ni vyema sana wakituma wataalam ili waweze kutoa tamko kuhusiana na ukweli wa dawa/tiba hiyo.ila wasiishie hapo ni vyema pia waweke wazi kua kua huyo bwana ni mtu wa maombi au mganga?
 
jamani huyu mzee!! ndugu zangu wamebebana huko, mie sielewi nikitu gani hiki!!!!!
 
Back
Top Bottom