Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwanza jina lako linadhihilisha wewe uko hoi, pili nina hakika wewe huna imani na ulimwengu unao ishi. Ukiambiwa hiki ni kivuli chako pia utakataa!!!!!! Sasa waulize watu lukuki waliokwenda Loliondo na mpaka sasa wanakwenda je wanapona????????? Ndg yangu watu wamejaa huko si Waarabu, Wahindi, Wazungu, matajiri ndo usiseme, PM ALIKUWA HUKO, Mkuu wa Boma kaisharudi toka huko. Sijui nikwambie vipi???????? Hayo ni maajabu ya Mungu, ni imani yako tuu. Mwamini Mungu yote yawezekana !!!!!!!!mimi naibeza kazi yake!kama amegundua dawa afuate taratibu,aende muhimbili kuna kitengo cha traditional medicine aeleze jinsi inavyofanya kazi,dose,inaingiaje na kutokaje mwilini,madhara yake(side effects),inaingiliana vipi na dawa nyingine(interaction with other drugs),inatumikaje kwa makundi maalum mfano watoto,wazee au wajawazito.
Imefanyiwa majaribio lini,wapi na kwa nani?haya ni baadhi ya maswali ambayo anatakiwa kuyatolea ufafanuzi.bila kujibu maswali haya halafu unaibuka from nowhere na kujidai unatibu!huu ni ukichaa wa aina fulani.naomba apate huduma ya psychiatry haraka iwezekanavyo.
Ni juzi tuu mkuu mmoja wa serikali alitangaza kua ugonjwa kama wa kisukari hauna dawa kabisa, leo gazeti la Mwananchi linatoa taarifa kua kuna mchungaji anatibu kisukari, ukimwi na magonjwa mengine sugu. Kinachishtusha sana ni kuona akili za waTanzania wengi namna gani zinaweza kukinaishwa maramoja.
Ugonjwa kama ukimwi kisukari nafikiri sio ugonjwa wa mtu kupewa kikombe kimoja cha dawa na kufika kwenye conclusion kua mtu ameshapona, tunaribu kua reasonable, hivi ni vitu vinahitaji muda kidogo ili kujua kua kweli dawa hiyo inatibu.
Upande mwingine ni ule wa mtu kudai kua ana mawasiliano na God hili nalo linahitaji kuangaliwa vizuri. Kinachoshtusha zaidi ni kusikia watu ambao tunawaamini kua ndio viongozi wa taifa letu kama wabunge mawaziri wanamiminika huko na mkuu wa mkoa anaiomba serikali ifacilatate mazingira ya watu kwenda. Hii ndio Tanzania yetu. Mungu ibariki dunia, Afrika na Tanzania
SIMWAMINI HUYO BABU HATA KIDOGO.Inawezekana akawa anapiga janja ya shehe YAHYAIngekuwa mzungu hapo watu wangeamini na wangeanza kutoa pongezi na kusifia, lakini mwafrika tena mtanzania hata kama kweli watu wanapona , lazima fitma ziwekwe kumzimisha babu wa watu, dawa ipatikane miradi mikubwa ife na kuna watu wanategemea miradi ya ukimwi na kansa kuishi
Am fed up!Wailing, Mungu hata siku moja haangalii dini ya mtu; dini ni phylosophy ya kibinadamu zaidi kulinda self interest..Mungu anaangalia moyo uliotayari kupokea na halazimishi mtu kutenda against his will maana amempa binadamu will..ukiwa humble in heart atakufundisha taratibu kujua ukweli wa mambo..Kinyume na Mungu ni shetani yeye mambo yake ni ya kulazimisha na anataka matokeo yawe papo kwa papo ili uwongo wake usigundulike....So dont think about your dini to be a constraint kwani pengine ulijikuta uko kwenye dini kwasababu ya wazazi uliopewa na Mungu huyo huyo so he knows best why you were born in that family....Chamsingi acha moyo wako wazi mbele za mungu naye anajua jinsi ya kukusaidia pale unapoomba kupata solutions to your problems....i ahve helped many Muslims who were ready and humble in heart na hata siku moja sijafanya hivyo kuwa manipulate ili waje kwenye imani yangu najua one day they will come to know the truth; a person can be a muslim by name but full of faith in Jesus in heart and some are christians in names but empty of faith meaning they dont know that they actually are not christians for christianity if more than going to church and participating in all church time tables so let us leave God to judge the living and the dead for He is righteous!
SIMWAMINI HUYO BABU HATA KIDOGO.Inawezekana akawa anapiga janja ya shehe YAHYA
ndugu yangu ana kansa ,kapelekwa huko leo, yaan nashindwa kuamini au kukataa ila namuombea apone tuu km kweli hiyo dawa inatibu
Hivi wewe unataka nauli ya kutoka Arusha hadi Loliondo iwe Tshs 500? Ukiweka gari mafuta hata ya Tshs 1000 haliwezi kukufikisha hata Burka kutoka mjini bila gari kuzimika. Miujiza anafanya Babu na hajamlazimisha mtu kwenda huko ila kutokana na matatizo waliyonayo watu elfu 80 inaonekana ndogo kama watu wakiamua kuwachangia wenzao wagonjwa. Mbona harusi tunachangai mamillioni tushindwe kumchangia mtu elfu 80? Pia kumbuka babu hana magari useme atafanya muujiza mafuta ya shilingi 500 yatoshe gari kutoka Ar hadi Loliondo.
Tunapotoa hu mwito pia tudadavue kdg, eti ni kweli JK naye alikwenda kunywa dawa? Maana, karibuni alikwenda Loliondo eti kufukua nyayo! Hahaha
Tukabali tusikubali watu kwa mamia wanmiminika huko Loliondo. Mahitaji ya kijamii yanazidi kuwa ni utata mtupu kwenye eneo hilo. Kama tiba inamatokeo au haina matokeo ya kuridhisha hilo aachiwe kila mtu na kwa ukweli si hoja ya kuongelea kwa sasa. Na kwa ukweli hakuna sheria yeyote ya tiba mbadala iliyokiukwa hadi sasa. Kwa hiyo serekali haiwezi kujitoa kwenye kulifanya tukio zima sehemu ya shughuli zake za jamiii.
Honestly Serekali kupitia wizara ya afya kitengo cha tiba mbadala wafanye ushirikiano na makubaliano na Babu...
.... Aje kufanyia shughuli zake Sheigh Amri Abeid ARUSHA. Hii shughuli yote iwe total official kwani itakuwa rahisi kuimanage na kuimonitor. Babu awezeshwe...
Sasa tusemeje ...? Ukweli ndio huo.The facts is WATU WANAKWENDA HUKO....Its up to the goverment kuwezesha wananchi na kumuwezesha Babu..
Hii issue hawezi kuachiwa Babu na wananchi peke yake..ni issue ya kijamii na lazima kuchukuliwa hivi kwa sasa kwa ajili ya kusimamia afya, usalama na amani ya wagonjwa wanaomininika huko na afya na usalama wa Babu mwenyewe.