Kiongozi mmoja wa kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam jana alielezea msimamo wa kanisa Katoliki kuhusu tiba ya Loliondo inayotolewa na Mchungaji Ambikile Mwaisapile kuwa kabla mtu yeyote hajapata tiba hiyo lazima ajiulize maswali manne kwanza kabla ya kuamua kuitumia.
Akihutubia katika Ibada ya Jumapili katika Kigango cha Mt. Yohane wa Msalaba Parokoa ya Mbezi Luis, Paroko wa parikoa hiyo Padre Vivian alisema, "Sina chuki wala tatizo lolote na tiba ya Loliondo, lakini kama unataka kwenda lazima ujiulize maswali manne yafuatayo.
"Kwanza, tiba inayotokana na miujiza ya Mungu lazima iwe endelevu isiwepo kwa kipindi kifupi tu," alisema.
Swali la pili alilotaka watu wajiulize ni kuwa tiba inayokuja kama muujiza kutoka kwa Mungu huwa na masharti? Swali la tatu alilolitaja Paroko huyo ambaye ni Padre wa Shirika la Wakalmeli ni kuwa, Kama tiba hiyo inafanya kazi ndani ya Loliondo, kwanini isifanyekazi Dar es Salaam na kwingineko?
Na swali lake la mwisho alilotaka watu wajiulize kuhusu tiba hiyo ya magonjwa sugu ukiwemo UKIMWI ni je, Mungu aliwaumba wanadamu na kisha kuamua kuwaangamiza? Au wanadamu wanaangamia kutokana na vitendo vyao vya ujanja ujanja?
"Ukiisha jiuliza maswali hayo na kujiridhisha kwa majibu utakayopata unawea kufanya maamuzi ya kwenda Loliondo. Hivyo ukiliona basi limeegeshwa katika stendi ya Mbezi au mahali pengine na ukasikia wapigadebe wanaita Loliondo Loliondo Loliondo, basi panda ukapate kikombe cha Babu," aliongeza kusema.
Katika siku za hivi karibuni Mchungaji Mwaisapile ameutikisa Ulimwengu baada ya kutangaza kuwa anatibu magonjwa sugu kwa kutoa dozi ya kikombe kimoja cha dawa ya kienyeji kwa gharama ya shilingi 500/ kwa Watanzania na Tsh 1,000/= kwa wageni.
Viongozi mbalimbali wa siasa na dini wakiwemo maaskofu wa madhehebu ya Kikristo wamekuwa wakitoa ushuhuda wa ukweli wa tiba hiyo na kuwashauri wananchi wenye magonjwa sugu kwenda kijijini Samonge mkoani Arusha kupata tiba.
Hata hivyo kwa upande mwingine, baadhi ya viongozi wa makanisa hayo akiwemo Askofu Zakaria Kakobe wa kanisa la FGBF na Mchungaji Christopher Mtikila wamekuwa wakiipinga vikali tiba hiyo.
Source: mbs
....lakini watu tujue pia hakuna dawa ya kuponya kifo. .
Asante kwa ushuhuda pole sana mkuu, mimi nitakuwa wa mkristu wa Mwisho TZ kumwamini huyu babu.
Pole sana ndugu;
hapo umeeleza vizuri kabisa - hakuna dawa ya kifo;
Na babu hajasema dawa anayotoa inatibu kifo; muda unafika Mungu akakupenda zaidi, basi anakuchukua!
Asante kwa ushuhuda pole sana mkuu, mimi nitakuwa wa mkristu wa Mwisho TZ kumwamini huyu babu.
Sijakuelewa mantiki ya kuleta hii thread humu,hadi sasa unaleta hii habari bado hauna imani na ndio maana unasaka watu walete ushahidi ili wajiridhishe.Babu kule yuko wazi ukichakachua unakunywa maji.Mwenyewe umelonga kuwa hakuna dawa ya kuponya kifo kwa hiyo unacholaumu ni nini!!!Unaogopa kusema ukweli kuwa huwa imani na tiba ya babu ila unatumia lugha rafiki ili usishambuliwe humu.Hakuna mtu ambae hataonja mauti hivyo kubali matokeo tu kwani hata wale waliofufuliwa na yesu(kwa imani yangu) mwishoe walikufa.na hata ambao watajitokeza kutoa ushuhuda wa babu mwisho wa siku watakufa tu.suala ni timeframe huyu kakaa siku ngapi huyu miaka mingapi.huo ndio ukweliKwa wanajamii wote, naomba kutoa ushuhuda kuwa nilimpeleka mgonjwa wangu mke wa rafiki yangu mpenzi kwa Babu wiki mbili zilizopita ili kupata dawa kutokana na maradhi ya Breast cancer ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Kama sote tunavyojua hakuna dawa ya kutibu kansa, lakini baada ya kusikia habari za Babu tulijenga imani kuwa huenda akapona. Tulimpeleka huko, na baada ya kukaa siku mbili kwenye foleni alibahatika kupata dawa na kuinywa. Lakini toka anywe hiyo dawa hali yake imekuwa sio nzuri na kudhoofu siku hadi siku hadi hii leo saa nne asubuhi amefariki dunia. Ninatoa ushuhuda huu si kwa kuwakatisha tamaa watu la hasha bali ni kutaka kuweka vitu hadharani ili watu wajue kuwa pamoja na kuwa huenda dawa hiyo ikawatibu baadhi ya watu lakini watu tujue pia hakuna dawa ya kuponya kifo. Huenda kweli babu anatibu kwa imani, lakini sidhani kama wale wote wanaoenda huko hawana imani. Namalizia kwa kuzidi kuwaomba waliotibiwa na kupona kweli wajitokeze watuthibitishie kwa ushahidi wa kitabibu.
Kwa wanajamii wote, naomba kutoa ushuhuda kuwa nilimpeleka mgonjwa wangu mke wa rafiki yangu mpenzi kwa Babu wiki mbili zilizopita ili kupata dawa kutokana na maradhi ya Breast cancer ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Kama sote tunavyojua hakuna dawa ya kutibu kansa, lakini baada ya kusikia habari za Babu tulijenga imani kuwa huenda akapona. Tulimpeleka huko, na baada ya kukaa siku mbili kwenye foleni alibahatika kupata dawa na kuinywa. Lakini toka anywe hiyo dawa hali yake imekuwa sio nzuri na kudhoofu siku hadi siku hadi hii leo saa nne asubuhi amefariki dunia. Ninatoa ushuhuda huu si kwa kuwakatisha tamaa watu la hasha bali ni kutaka kuweka vitu hadharani ili watu wajue kuwa pamoja na kuwa huenda dawa hiyo ikawatibu baadhi ya watu lakini watu tujue pia hakuna dawa ya kuponya kifo. Huenda kweli babu anatibu kwa imani, lakini sidhani kama wale wote wanaoenda huko hawana imani. Namalizia kwa kuzidi kuwaomba waliotibiwa na kupona kweli wajitokeze watuthibitishie kwa ushahidi wa kitabibu.
umeandika vizuri sana. natamani watu wasome na waelewe. kupona ugonjwa siyo kupona kifo. kama kifo chako kimepangwa kutimia kwa ugonjwa,basi hata kama dawa ya ugonjwa huo ipo na umetumia kifo kitakuja tuuu.
ni vema tukaelewa kuwa kutumia dawa ya Babu siyo kuepuka kifo, bali ni kupona ugonjwa , hata wale wote walioponywa na Kristo Yesu baadae walikufa. Tukeshe tukiomba kwakuwa hatujui saa ya hukumu yetu