Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Dah! Pole sana.
Ngoja nihairishe safari nisikilizie brekin nyuzz zingine
 
Acheni ujinga! zaidi ya kumpa pole jamaa anataka ushuhuda kwa aliyepona. sio kumtetea babu. huna ushuhuda kaa kimya!
 

Umemuelewa vizuri... sana! medically speaking cancer ina stage zake, ikishakuwa metastatic hata hospital wanashauri radiotherapy ama chemotherapy, hiyo ndio fact, anayosema babu happens only katika hollywood movies ati kikombe kimoja kina cure all kinds of disease kwa neno la mungu lililomo ndani ya mti what a joke!!?.. :lol: huyu babu angekuwa nchi zilizoendelea angeshapelekwa hopsitali i bet yeye mwenyewe hes a psychotic patient .. babu need a shrink ! what happen in loliondo ni Scam & Nonsense!

watch hii vid.kipande cha mwisho kabisa dactari anasema wale waliofika kupima ngoma "HIV" tena baada ya kupiga juice ya babu they still test + ve
 
pole sana mpendwa kwa msiba uliokupata.

najua babu hawezi kuzuia kifo, na hata kama alipona kansa bado anaweza kfa kama siku Mungu anayomhitaji imefika.lakini nina swali kidogo.

naomba utusaidie, mliwahi kuthibitisha hospitali au kwa namna yoyote nyingine kuwa marehemu alipona cancer baada ya kupata kikombe cha babu?

ukitujibu hapo utakuwa umetusaidia sana.

poleni tena na msiba na hekaheka zake.

Mungu wa rehema awafariji

Glory to God
 
pole sana kwa yaliyokukuta.nadhani ushauri wako ufuatwe na wote waliopona watoe ushahidi wa kitabibu ili ukweli ujulikane.usiku mwema,jipe moyo kwani hata dawa za hospitalini kuna wanaotumia na kupona na wengine hawaponi.:angry:
 

natanguliza pole kwa mfiwa!heshima mbele kwa wachangiaji wote!niliwahi kusema nathamini sana afya ya mtu na sipendi mtu amkatishe mgonjwa tamaa ya kupona kwani magonjwa ambayo babu anadai kuponya ni magonjwa yanayotishia maisha na walio nayo wana mahangaiko mengi sana!naomba ieleweke nawatambua na nawathamini sana wagonjwa wote!niliwahi kusema kwamba nitarudi baada ya wiki moja nikikamilisha uchunguzi wangu.nilikaa kimya baada ya hiyo wiki kwani sikuwa nimefanikiwa sana katika uchunguzi wangu!LEO NATAMKA KWAMBA KATIKA UCHUNGUZI WANGU SIJAONA HATA MMOJA ALIYEKWENDA KWA BABU AKAWA AMEPONA!naamini nimeeleweka!
 


Acha kudanganya watu wewe....kasome neno la Mungu vyema,kumbuka neno la Mungu si siasa....kama ulijui usilitumie kushawishi watu vibaya maana hatia yake ni kubwa....ole wake yeye aongezaye au apunguzaye japo nukta moja katika haya maana atakunywa katika kikombe cha hasira ya Mungu..........
 
Pole sana siku yake ilifika tu, mimi bosi wangu ameenda na sasa yuko fiti sana ameanza hadi kula vyakula alivyokataliwa na doc
Mwambie amshukuru babu kwa kumponya lakini aendelee na diet kama alivyoshauriwa na daktari.
 

Nonsense.....kwani uwezi kujiuliza tu

  1. Huo mti unazaa matunda ya aina kumi na mbili?
  2. Babu anatumia mizizi sio majani
Kwa taarifa yako huo ni unabii wa mti wa uzima kwenye edeni mpya ya mbinguni baada ya Yesu kuwachukua wateule.....USIDANGANYIKE...
 
babu alishasema kuwa kupona kwako ni imani yako zaidi, .... mbaya zaidi wenye imani za kishirikina wengi wapoteza maisha nina ushuhuda wa jirani yangu. kaka yangu tulimpeleka hadi india kwa case ya cancer hakupona ila baada ya kikombe cha babu sasa hivi kila kukicha anaendelea kuwa fit.
 
Pole sana mkuu. Unataka waliopona walete ushuda wa kitabibu ...hili ni sawa....Lakini najiuliza huu ushuhuda wa kitabibu unakuwaje? Ni kama huu ushuhuda wako (kwa bahati mbaya ni wa kifo)?
 
haya mambo ni hatari sana na serikali isipochukua hatua litakuwa janga la kitaifa hapo baadae kwani watu wanaacha dawa ambazo zilikuwa zinawapa nafuu na kutumia hizi za Mafree masoon, Wilaya ya masasi eneo la Lukuledi kuna Mdada anaitwa Rose anawapiga watu pesa balaa na anafadhiliwa na AGAPE sasa sijui inakuwaje hapo...........Mimi nazidi kuunganisha Nukta tu
 
Duh!ahsanteni sana wadau wa JF kwa michango yenu mizuri,hakika baada ya dhambi binadamu alijulishwa kuwa kifo ni hakika na kwa uhalisi wa mwanadamu hatuwezi zuia kifo kwani kwa imani ya kikristo kifo ni usingizi pale unaposubiria hukumu baada ya ufufuo,la msingi hapa ni unakufaje!ukiwa na matumaini ya uzima wa milele au lah! pole sana uliyefiwa hata mimi na wewe ipo siku yetu
 
Prof. Hiyo sentensi yako ya mwisho una maanisha nn? Dawa ya babu itaua wote walioinywa?
 
pole sana kwa msiba ila naomba ujue kwamba kuna dawa ya babu na mapenzi ya Mungu.hata ukinywa dawa ya babu kama muda wa kuitwa kurudi kwa BABA umefika ni lazima utatuacha tu.
jina la Bwana lihimidiwe

Hebu subiri kidogo. Kuna dawa ya babu na mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo dawa ya babu ni kitu kingine na Mungu ni kitu kingine. Lol!
 
Kuna watu wengi wamehoji ushahidi wa kisayansi wa kikobe cha babu, Kwao wao ili dawa itibu lazima wapate scientific explanation. Kwa wengine imani inatosha kwani Babu anasema kinachotibu si yeye bali neno la Mungu lililowekwa katika mti huo; yeye ni kiunganishi cha mgonjwa na neno hilo. Kwa wanaotibiwa kwa imani hadi sasa hakuna tatizo, ila kwa wale wanaotaka kisayansi wameonekana kutokubali.
Sasa tunaambatisha maelezo ya kisayansi na uchunguzi mbalimbali wa kisayansi wa mti huo
Shukrani nyingi kwa Rose wa WHO dsm.
 

Attachments

Kumbe basi hata scientificaly huo mti unasaidia....still God can use even a dry wood to heal...He is able
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…