Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Jamani waacheni wenye imani zao wapone.

Imani ndo inatibu sio maji wala mizizi
 
Tatizo kubwa sana la maendeleo Africa ni kuwa na tafiti nyingi ambazo hazifanyiwi kazi. Tuna taarifa ya tafiti nyingi katika fani nyingi lakini taarifa hizo zinabaki mapambo katika maktaba!.

Kwa kweli ni huzuni.

Watafiti wengi wamekimbia hiyo fani maana wamekuwa wakifanya kazi ya bure na kuishia makabatini
 
Watafiti wengi wamekimbia hiyo fani maana wamekuwa wakifanya kazi ya bure na kuishia makabatrini
. Kaka siku hizi research za promo kama redet au steadman. Ottherwise wengine Copy and paste kupata cheti tu
 
Waziri wa utalii kenya kishatangaza babu anapatikana kenya loliondo!
 
lmani chanzo chake ni KUSIKIA.
Imani ni kuwa na halika ya mambo yanayotarajiwa, lmani ni bayana ya mambo yasioonekana. Ukitaka kupona magonjwa yako ni lazima ndani mwako ijengeke imani thabiti, kama waliyokuwa nayo wana wa lsrael, wakauzunguka mji wa Yeriko nao kuta zake zikaporomoa. Unatakiwa uwe na imani ya kumshinda Petro alipotaka kumfuata Yesu kwa kutembea juu ya maji.
Soma somo la imani kikamilifu wala hutokuwa na haja ya kwenda Loliondo.
 
Nilishakuuliza kama umeokoka siku hzi...mbona hukunijibu?

mim huwa sipendi kutangaza kwa maneno kuwa nimeokoka au la,bali napenda matendo yangu ndio yatangaze kuwa Yesu yupo ndani yangu.
bahati mbaya hunifahamu,ungekua unanifahamu nadhani wala usingeuliza kama nimeokoka au sijaokoka.
hebu sikiliza huu wimbo labda utasaidia kuongeza maana ktk jibu langu.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo kwa Tanzania,
Watafiti wanatafiti na wanapomaliza na kukabidhi matokeo ya tafiti zao.. huchukuliwa na hakuna chochote kinachofanyika na ziada ni kwamba anaweza kutafiti Bahati na akapewa sifa Malimwengu!

Mfano ni yule mzee wetu aliyesema bwawa la kufua umeme lisiwekwe Kihansi, wanaume wakaliweka huko! huyo anarudia tena kutafiti?
 
imekuwa vigumu watu kumamini nguvu za Mungu kutokana na vitendo vya baadhi ya wachungaji waliopo hivi sasa, imagine kakobe anaweza muhubiria nani aliye na akili zake timamu? wizi mtupu, wao ni sadaka na kuwapokonya watu hela kwa jina la yesu wanaomjua wao. Kwa hili la Mwasapili hakika ni mtu wa Mungu
 
hivi kati ya wanaojiita waokovu pamoja na mabishop wao wasiojua hata kutafsiri neno na huyu mwasapile nani anaedhihirisha wokovu kamili? Ulokole God forbid! Total hypocrisy! let the old man do what is right for the people and God will reveal himself through miraculous healing
 
Hali ni mbaya....yule wa tarakea alisema kuwa watakuwa watatu..........naona huyo wa Mbeya ndio anatimza crew.................
 
hehehe! uniacha hoi hapa tu
Ndipo usiku huo huo kijana yule akatoweka kwa miezi mingi huku ndugu zake wakimtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio.
Sasa amerudi kutoka katika 'kozi; hiyo na ndipo ameanza rasmi kutoa tiba na kinga hiyo.

kijana alienda kupiga kozi porini! ameshagraduate sasa.. hehehe!! Afrika hakuna matata..
 
Daah yaani hata kufikiri kidogo tu kutakusaidia kubaini kuwa dawa ya BABU na andiko hilo ni vitu viwili tofauti, kwanza tukitafsiri ufunuo huo kwa akili halisi za kibinadamu na si za kiroho ni kuwa mti uliotajwa ktk ufunuo huo unatoa matunda 12 mti wa BABU hauna sifa hiyo, pili mti wa ktk ufunua umeelezewa kuwa majani yake ndio tiba wakati mti wa BABU mizizi yake ndio tiba, HADI HAPO UJABAINI TOFAUTI?

Jamani tukubaliane kimsingi kama ilivyo kuna madhehebu kibao ya KIKRISTO na yote yana mhubiri YESU na kutumia BIBLIA na kuamini kuwa kila dhehebu kuwa lipo sahihi kuliko mengine ndivyohivyo hivyo kuhusiana na tiba ya BABU kuna wanaoamini ni sahihi na yatoka kwa MUNGU na wapo wasio amini japo wote ni WAKRISTO hivyo akili kichwani mwako kama waamini kapige kikombe na kama uamini endelea kusuburi muujiza wa uponyaji toka kwa BWANA kupitia MAOMBI.
 
Sijakuelewa mantiki ya kuleta hii thread humu,hadi sasa unaleta hii habari bado hauna imani na ndio maana unasaka watu walete ushahidi ili wajiridhishe.Babu kule yuko wazi ukichakachua unakunywa maji.Mwenyewe umelonga kuwa hakuna dawa ya kuponya kifo kwa hiyo unacholaumu ni nini!!!Unaogopa kusema ukweli kuwa huwa imani na tiba ya babu ila unatumia lugha rafiki ili usishambuliwe humu.Hakuna mtu ambae hataonja mauti hivyo kubali matokeo tu kwani hata wale waliofufuliwa na yesu(kwa imani yangu) mwishoe walikufa.na hata ambao watajitokeza kutoa ushuhuda wa babu mwisho wa siku watakufa tu.suala ni timeframe huyu kakaa siku ngapi huyu miaka mingapi.huo ndio ukweli

kumshambulia mtoa ushuhuda si jambo sahihi kwa muda sasa tunahamasishana kutoa ushuhuda wa kupona au kutopona kwa wale wote walioenda kupata kikombe kwa BABU na wenzetu katoa USHUHUDA mgonjwa aliyepata tiba ya kikombe kwa BABU kafariki sasa kosa lake nini? Tatizo ni kuwa kuna watu wanamuamini BABU kama vile BABU ni MUNGU mtu akiwa na mawazo tofauti kuhusu tiba ya BABu wanamuona kama ni SHETANI, tukumbuke si lazima wote tumuamini BABU lazima wawepo wenye imani haba au wasiomuamini kabisa na si kosa kuwa ktk pande zote tatu, kumuamini, kuwa na imani haba, kutokumwamini kabisa. Tukumbuke YESU alipata kusema "kama hamniamini mimi basi mwaminini aliyenituma (MUNGU)" Yaani hata YESU aliona kutoaminiwa yeye si tatizo tatizo ni kutokumwamini MUNGU. Hivyo kutomwamini BABU wa Loliondo si kosa bali kutomwamini MUNGU ni kosa, Hivyo yatupasa kurudi ktk maandiko ili kujahakikishia kama kweli tiba ya BABU yatoka kwa MUNGU au la, Maandiko yakikuaminisha kuwa ni kweli tiba ya babu yatoka kwa MUNGU sawa na vilevile yakikuakikishia kuwa tiba ya BABU si ya kutoka kwa MUNGU sawa akili kumkichwa uamuzi utakuwa juu yako, angalizo usisome maandiko kwa lengo la kujustify maamuzi yako bali soma kwa lengo la kupata ukweli wa maandiko kama ni kweli tiba ya BABU yatoka kwa MUNGU au la.

Mwisho hata kama tuna mwamini BABU basi muwe na uvumilivu kwa USHUHUDA ambazo zinatiliashaka uhalisia wa tiba ya BABU. MAANA INASHANGAZA Kufananisha tiba ya Hospitali natiba ya MUNGU, siku zote tiba ya MUNGU ni uponyaji halisi usio tiliwa mashaka kukiwa na mashaka ktk uponyaji huo lazima watu wahoji. Hivi kweli mtu asihoji kupoteza maisha kwa mgonjwa wake aliyepelekwa kupatiwa tiba isemekanayo yatokana na maagizo na maono yaMUNGU eti kwa sababu hata Hospitali wagonjwa wanakufa? Kumbukeni wa MUNGU ni uponyaji mtu apone ndipo afe ( lakini apone kwanza maana kufa ni lazima kwa kiumbe yeyote) kwa kuwa siku zake zilifika lakini hapa tunaona mgonjwa hakupona na amefariki DUNIA. Tukumbuke ktk ushuhuda wa jamaa ajasema kama wamechakachua ktk foleni. Nami nitaleta ushuhuda wa mgonjwa aliyepata kikombe kufariki lakini una mazingira tofauti na huu ulioletwa mbele yetu tunao ujadili sasa.
 
ilishasemwa .... AFRIKA BARA LA MATUKIO!!!

hapa nasubiria tukio jipya baada ya 'KUCHAKACHULIWA MATOKEO, DOWANS.... MAANDAMANO YA AMANI... BABU WA LOLIONDO & CO....."
 
Kwa mujibu wa taarifa ya habari Tbc mchana huu inasema wizara ya afya imethibisha hilo kuwa dawa ya babu haina madhara kwa binadamu.
 
Back
Top Bottom