Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Kama ni kweli au uwongo, tunamshukuru Mungu kwa kila jambo.
 
Mimi naumwa mapenzi.
Yaani mapenzi yangu kila siku yanazidi kwa JF..
Nikilala naota jf, nikiamka nawaza jf. Nikinywa maji naiona jf kwenye glasi.
Ndugu mtoa mada, nahisi huo ni ugonjwa. Naweza nikapata dawa ya kupunguza makali?
NB: Sitaki nipone kabisa.
 
Kuna ndugu mmoja( Askofu mstaafu wa K.K.K.T) au maarufu kama Doctor anakaa wilaya ya Loliondo mkoa wa Arusha anatibu magonjwa yote sugu kama Ukimwi,kisukari,magojwa ya moyo,mifupa,ini,figo n.k kwa muda mfupi. Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali za nchi,uarabuni,ulaya wanamimini. Binafsi kuna mzee wangu alikuwa na kisukari amepona kabisa. Bei ya dawa ni shilingi mia tano tu.

Unalipwa Sh ngapi kutangaza biashara ya huyo askofu? Hawa maaskofu nao siku hizi, siasa wao hata uganga wa kienyeji, kweli tuko kwenye siku za mwisho.
 
Mimi naumwa mapenzi.
Yaani mapenzi yangu kila siku yanazidi kwa JF..
Nikilala naota jf, nikiamka nawaza jf. Nikinywa maji naiona jf kwenye glasi.
Ndugu mtoa mada, nahisi huo ni ugonjwa. Naweza nikapata dawa ya kupunguza makali?
NB: Sitaki nipone kabisa.
Nione haraka nimekufichia dozi yako :coffee:
 
Aisee hiyo ya ukimwi ndiyo ya muhimu zaidi maana mie hizi jezi za mechi zimeshaanza kunipa aleji .TFDA wakithibitisha ubora,niPM
 
hivi mpaka leo mnaogopa ukimwi,mbona kansa zaidi ya huo ukimwi:rain:
 
Kama ni kweli basi ni kheri mbona ila hiyo kitu haipo kabisa
 
Nigeria nimesharudi, ngoja niende Sumbawanga na Kigoma nikirudi tu Natibu magonjwa yote hayo na bei itapungua nipo Dar.
 
Jamani mimi nimefika hadi kwa huyo mzee. Sio askofu mstaafu kama mtoa mada anavyosema bali ni mchungaji mstaafu japokuwa bado anafanya kazi za uchungaji. Anatoa dawa aina moja tu (kikombe kimoja cha chai) kwa magonjwa yote iwe HIV, kisukari, pumu, vidonda vya tumbo na mengineyo. Sijathibitisha HIV lakini pumu na kisukari nimethibitisha watu wakipona. Naamini dawa anayotoa inaweza kuponya kwa sababu watu ni wengi sana wanaenda huko kwa siku (zaidi hata ya 100) na ni gharama kubwa kumfuata, zaidi ya km 300 kutokea Arusha mjini na barabara ni mbaya mno. Je ingekuwa watu hawaponi wangegaramika namna hiyo kumfuata huyo mchungaji ilihali hawana hata ushahidi wa mtu aliyemponya?
mkuu ww ulikwenda kutibiwa nn? ebu tujuze
 
Ni kweli anatibu wengi wamepona.Kama una matatizo ya aina hiyo au yanayofanana na hayo tafadhali nenda tu ukapokee uponyaji.
 
Ni kweli huyo jamaa anatibu magonjwa mengi ambayo mimi nimeshuhudia kwa jamaa waliokwenda wamepona kisukari, maana wengi wa rafiki zangu walikuwa wanasumbuliwa na kisukari. Si unajua tena kisukari balaa hata "mguu unaweza kushindwa kufanya kazi" vyema! Sasa ofisini kwetu kuna muathirika na amejitangaza tunataka tumpeleke kisha tuone majibu yake yatakuwaje? Akiwa negative nitakujuzeni wakuu.
Kwa wanaotaka kwenda hivi sasa kuna route kabisa ya kutoka Arusha kwenda kwa huyo mchungaji nauli ni Tshs 17,000.00 ila barabara ni mbaya kwa takribani 150km kutoka getini Ngorongoro. Hivyo inabidi kujiandaa kisaikolojia kidogo kulingana na mazingira yake.
Cha kuvutia kidogo safari inakuwa kama tours fulani maana unapita eneo la hifadhi kwa takribani 75km ndiyo inaanza mbuga ya Loliondo ambayo nayo ina mvuto lakini si kama hifadhi kushituka umefika unakula tiba na kuanza kurejea tena.
Nawashauri kwa wale wenye ndugu zao kama wana uwezo wawapeleke huku kwani jamaa nasikia hataki maswali mengi yeye anakupa tiba kulingana na tatizo uliendea na dawa ni moja kwa magonjwa yote.
Ni hayo tu.
 
mmh hizi taarifa zinahitaji umakini zaidi
kusiki mtu akisema kuwa ametibwa na kupona bila ya kujua case record yake ya zamani ni kama kucheza kombolela
na kuambiwa mtu alikuwa anaumwa na amepona HIV,Diabetis,etc bila kujua result zake baada ya kutumia hizo dawa ni sawa na kujirisha upepo.
Kuna uwezekano akawa anapunguza risk factors,symptoms or other excercerbating factors na hapo mgonjwa automatically ankuwa na hali na afya njema ,lakini sio kwamba amepona.
Jamani mtofautishe Kupona na kutoa maumivu au kuvuta siku.
Wanaoumwa inawezekana kabisa walishakata tamaa, hivyo basi wanapopata njia yeyote ya kuwa encouraged in any way kama kupunguza maumivu na magonjwa mengine nyemelezi basi watasema kuwa wamepona.
Kwa mimi kama mwanasayansi kwanza ni lazima tumchukue huyo mgonjwa tumwomne status yake kaam ni HIV tujue alikuwa vipi na kama ni Diabetis tujue alikuwa na blood level kiasi gani( bearing in mind should be between 4-6 unit) then anatumia hizo dawa na akimaliza baada ya mda fulani let say a month or 3 months tunachukua vipimo na ku-confirm.
If it works ,why not to declare to the public? and he will get more publicity ever.
 
Tunashukuru sana kwa taarifa na utayari wa wale wenzetu kutuletea anuani na habari zaidi juu ya jambo hili. Mimi pia nimeshawahi kusikia humu humu kwenye vyombo vya habari lakini sikuwa na sababu ya kuzifuatilia habari hizi kwa ukaribu. Ila tunaoamini katika miujiza na nguvu za mungu tunazidi kumshukuru mungu kwa hili la uponaji, haijali kama ni pumu, kisukari, figo nami pia ni mmoja wanaoamini kwamba hakuna kisichowezekana mbele yamungu hata huo UKIMWI unaweza kuponywa pia kama mungu atataka mbona watu wengi zaidi siku hizi wanadai wanatibu? basi tuwaruhusu waendelee kufanya hivyo na wale wenye mahitaji tuwashauri wafuatilie maana hakuna watakachopteza kwa kujaribu. Leo hii wakati nikifuatilia TV kuona kama kutakua na live broadcast ya mashujaa wetu kule mwanza nimekutana na kipindi cha UKIMWI ATN alikuwepo tabibu wa alternative medicine amejitaja kama Dr Msingi nae pia alikua akihojiwa kuhusu dawa yake na tafiti alizofanya kuthibitisha uwezo wa dawa hizo, kwa bahati nzuri contacts zake ziliwekwa kwenye screen kama 0784407322 japo sina ushahidi na anachokisema nashauri wanaotaka kufuatilia wasisite huku tukijua kwa hali ilivyo katika nchi zilizoathirika sana kama zetu we are all affected and or infected. Goodluck na mtujuze basi kama mtapata habari zaidi hatuwezi kujua siku wala saa tutakapohitaji msaada huo
 
Jamani kuna mzee mmoja huko Loliondo anatibu magonjwa mengi hadi ukimwi kwa shiiling 500 tu.....haitaji zaidi ya hapo.
 
Jamani kuna mzee mmoja huko Loliondo anatibu magonjwa mengi hadi ukimwi kwa shiiling 500 tu.....haitaji zaidi ya hapo.

Yo Yo hii habari nimeisikia leo mchana, wafanyakazi wenzangu walikuwa wanaongea,hivi ni kweli?
 
Jamani kuna mzee mmoja huko Loliondo anatibu magonjwa mengi hadi ukimwi kwa shiiling 500 tu.....haitaji zaidi ya hapo.

hii ni kweli kabisa niliambiwa na jirani yake wa huko loliondo na dose is taken only once.
 
Back
Top Bottom