Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

kwa nini mnaondoka usiku,
na mie napenda kujiunga na huo msafara ila nimechelewa kuzisoma taarifa.
kama pangeni tena next week ili tupange sawa mambo ya ofisi then tuanze safari.
nasubiri mengi toka kwenu.
BIG UP PJ

during the period of lent ( kwaresima - 40 days) he will not practice ritual healing which starts next week wednesday
 
Kila la heri jamani ....tuendelee kumuomba mungu anyooshe mkono wake hii ni habari njema kwa wote
 
hizi ni nyakati za mwisho maandiko yanatimia.

mie hata siamni ni bora niwe tomaso, nilipokuwa kinda kuna mtoto maeneo ya Kibosho naye alikuwa anaponya watu kwa minajiri alitokewa na Bikira Maria, kwa sasa sijui hata yuko wapi.
 
Si PJ umesema huyo mganga huenda atakuwa na mafungo kuanzia jumatatu? Kama ni kwaresma si ni siku 40? Hebu tujuze tusijeanza safari tukakuta mzee kafunga!
 
Kuna uwezekano wakufanya hivyo yaani kutafuta kiwanja
Inabidi uende ndo utajua kuwa anakuwa na mda gani wa kuzalisha dawa kiasi hicho
Hiyo dawa ni ya miti shamba ila imeombewa
Huo uwezo kapewa yeye na Mwenyezi Mungu hivyo haurithishwi!
Watafiti wetu hawana mpango watatupotezea muda tu
Nauli ni kubwa kwa kuwa Loliondo ni mbalisana! almost 350 Kilometers from Arusha City!
 
Mungu ni Mkubwa na kweli ni maajabu. Jamaa zangu wengi tu waliougua sukari zaidi ya miaka hata kumi wamepona . Waliosahau lager wengine jana tulikuwa nao maeneo ya Mbauda tukipata ulabu na kusakakata rumba ile mbaua. Huwezi amini

Watahadharishe sana huyo Mungu anaetibu kwa Jina lake Linaloitwa Yesu nguvu zake hazipatani sana na hayo wanayoyafanya na usije shangaa hali yao ya baadaye ikawa mbaya kuliko ile ya kwanza....
 
Mchungaji adaiwa kutibu ukimwi Send to a friend Thursday, 03 March 2011 20:49

Daniel Mjema, Moshi
KWA takribani wiki moja sasa, mji wa Moshi na vitongoji vyake, umekuwa ukizizima kufuatia taarifa za kuwapo kwa mchungaji mstaafu anayetoa dawa zinazotibu magonjwa makuu manne ukiwamo ukimwi, kwa gharama za Sh500 tu.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa makundi ya watu wakiwamo Watanzania wenye asili ya kiasia, yamekuwa yakisafiri kwenda Loliondo, ili kupata tiba kutoka kwa mchungaji huyo.

Habari zilizozagaa katika mji wa Moshi na vitongoji, zinadai kuwa mchungaji huyo amekuwa akitibu magonjwa ya kisukari, ukimwi, shinikizo la damu na ugonjwa wa saratani.


Juzi mchana, nusu ya abiria waliokuwa katika basi moja la abiria lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha, walikuwa ni wale waliokuwa wakienda Loliondo lakini wakipanga kuanzia safari zao Arusha.

Wakili mmoja wa kujitegemea ambaye alikuwa ndani ya basi hilo, akitokea Moshi kwenda Arusha, aliliambia Mwananchi kuwa nusu ya abiria hao, walikuwa wanaelekea Loliondo.

Magari yanayokwenda eneo anakopatikana mchungaji huyo ni yale yenye nguvu (4WD) na nauli ya kwenda na kurudi kutoka Moshi ni kati ya Sh70,000 na Sh80,000 ingawa wenye uwezo wamekuwa wakitozwa hadi Sh100,000.

Dereva mmoja Haji Sadiki, juzi usiku alionekana akiondoka na kundi la watu nane kuelekea Loliondo na inadaiwa kuwa kila mmoja alilipa Sh70,000 kwa ajili ya nauli ya kwenda na kurudi.

Mkazi mmoja wa Mwanga, Rodgers Msangi, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM aliitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kutoa tamko kuhusu uhakika wa tiba inayotolewa na mchungaji huyo.

"Watu wanasema unapewa dawa kwenye kikombe kimoja cha chai na hata kama una ngoma (ukimwi) unapona na wala hataki pesa yako zaidi ya Sh500 tu. Watu makundi kwa makundi wanakwenda huko kila siku," alidai Msangi.

Habari zilizozagaa mkoani Kilimanjaro zinadai kuwa hata baadhi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini,wabunge na viongozi wastaafu wamekwishakwenda na kupewa dawa hiyo, ingawa hakuna uthibitisho wa kimaabara unaothibitisha nguvu ya dawa hiyo.

Tangu kuzagaa kwa taarifa ya mchungaji huyo, watu wamekuwa wakikusanyika katika vikundi kujadili suala hilo.
 
impresses me as witchcraft mingled with falsified Christianity........................

Kuna watu walenda huko na hali zao hivi sasa ni mbaya zaidi.........................ninaowafahamu wako wawili............................siyo statistically significant lakini kuna uhaja wa seriakli kuchunguza huu utapeli ndani ya kisingizio cha Kristu.....................
 
Guys kama mnasikia si mfike huko alafu mje kutuletea majibu kamili hapa??maana wote mnasikia tu na wengine mnalalamika fikeni huko na mtuletee proof hapa na sio maneno tu........
 
Alafu Felister wewe unatibu ukimwi au unatibu watu kuacha ngono haha.....
 
Ni nani ameenda huko akasema amepewa hiyo dawa na ameitumia akapona hayo maradhi??? Kila mtu ana sema "INASEMEKANA..JAMAA WANASEMA etc" Tupeni evidence..otherwise bado kwangu ni KUSADIKIKA.
 
Hii bado inahitaji utafiti wa kina

Wakati unasubiri utafiti ufanyike watu kibao wanapona. Hivi kama unachohiji wewe ni kupona utafiti unanisaidiaje?. Kila kona hapa Arusha kuna watu wanaelekea huko wengi wakipeleka ndugu zao baada ya wao kupona.
 
Ama kweli hizi ni siku za mwisho,mini nadhani huyu ni mganga wa mitishamba kama walivyo wengine.Hapo Bwana Yesu msimtaje,kwenye biblia hatujawahi kusikia huduma ya dawa na kuacha mia tano kwa hiyo huduma hiyo tafadhali msiihusishe na Bwana Yesu. nimeambiwa wagonjwa wanasubiri maji yachemke halafu kinawekwa kipande cha mti mpaka maji yageuke rangi nakuwa kama chai,halafu watu wanaketishwa wanapewa vikombe wanakunywa.
 
mbona kila mtu anasema "KUNA MTU KAENDA....KUNA MTU KAENDA".......mi nataka kumsikia huyo MTU KAENDA aje hapa aseme mwenyewe.....acheni uzushi.

Well ndugu baada ya taarifa za hapa JF juzi jumatano tuliondoka kama gari 8 zote zilikuwa zimejaa! Tuliondoka Moshi kiasi cha saa 3.50 hivi usiku tlifika alhamisi ya tarehe 3/3 saa mbili asubuhi. Umati tulikuta sijapata kuona maishani mwangu. Nauli ilikuwa shilingi laki moja kwenda na kurudi. Ilibidi tutumie ujanja wa kimjini tuweze kupata dawa. Asikwambie mtu kuna watu toka sehemu malimbali hapa Tanzania na jirani pia bila kusahau ndugu zetu suche! Kuna watu ambao waliletwa wakiwa wamebebwa kwenye magodoro. Siwezi kutoa ushahidi hapa kuwa namshuhudia nani kuwa ni nani kaweza kupona maana wanasema kuwa majibu baada ya siku saba. Nitarudi kuwapa taarifa za ni wangapi wamepona baada ya kupata taarfa kamili toka kwa wale niliosafiri nao. Binafsi nilimpeleka mke wangu kwa matatizo ya kuumwa kichwa. Niapoandika ujumbe huu yuko fit kabisa ni uchovu tu maana barabara ni mbaya kabisa. Jana wakati narudi mida ya saa 5 usiku nilikuta msafara wa magari yasiyopungua 50 wakielekea huko. Km 175 toka njia panda ya Kigongoni karibu na Mto wa Mbu kupitia Engaruka, Lake natron hadi Kwa Mchungaji ni mwendo wa masaa 6 hadi 7 kutegemea ni aina gani ya gari uko nayo. Sikushauri utumie gari ndogo, landcruiser ama Landrover is ideal though some 4WD of any type can do.
Nitarudi tena siku zijazo ka ushuhuda zaidi. Kwa sasa mnaweza kuniuliza maswali na nitajitahidi kujibu kwa kile nilichokiona.
Mbarikiwe sana.
 
hizi ni nyakati za mwisho maandiko yanatimia.

mie hata siamni ni bora niwe tomaso, nilipokuwa kinda kuna mtoto maeneo ya Kibosho naye alikuwa anaponya watu kwa minajiri alitokewa na Bikira Maria, kwa sasa sijui hata yuko wapi.

Yuko pale King'ori kwenye kituo cha watoto yatima mkuu
 
Back
Top Bottom