Je anatibu magonjwa tuau anatoa na dawa kwa wenye shida yakupata mtoto? Plz nijuzen jaman nina ndugu yangu anashida hiyo. Na je wenye HIV walioanza kutumia dawa nao wanapona?
Kwanza kabisa mimi binafsi nawasibitishia kuwa naendelea vizuri mpaka sasa japo sijafikisha 7 days,nilikuwa huko kwa ajili ya kale kaugonjwa kangu kama nilivyowahi kuwauliza mtu mwenye kisukari chakula chake ni nini katika moja ya POST zangu na ninashukuru wana JF walinipa miongozo mingi na nilikuwa naifuata sana ila vingine nimeacha.baada ya kumsiki rafiki yangu alinichukua tarehe 27.02.2011 tulindoka arusha mjini yapata saa 10.00 alfajili,ni mwendo mrefu sana ni zaidi ya kilomita 330 kwenda tulifika saa 5 asubuhi,barabara ni mbaya gari inayoweza kuvumili ni yale yanayobeba watalii cruser na landrover nazo zikirudi ni matengenezo makubwa, ubebaji kidogo ni abiria 15 na kuendelea kila kichwa 70'000 mpaka 100,000.00,siku hiyo gari zilikuwa zaidi ya 150 na tarehe 26 rekodi tuliyoikuta kenye mpaka wa monduli na loliondo ilikuwa zaidi ya gari 300,kwa kweli nishagaa sana kwani ni umati mkubwa sana.Cha kwanza kabisa tuliorodhesha majiana na kumkabidhi alitupatia tiba ya dharura kwani alisema jumapili ni siku ya kupunzika baada ya kutoka kwenye ibada hivyo tulianza kutibiwa saa 8 mchana ilikuwa shughuli kila mtu anataka kuwa wa kwanza kupona.
Kuhusu TIBA ni kikombe kimoja tu kwakila mgonjwa,nilikuta wahindi,waarabu na hata wenzetu wa jirani afrika mashariki,kabla hujanywa dawa ni lazima akueleza dawa hiyo imepatikana vipi na ni ndoto toka wa mungu,mti wenyewe unasemekana ukiutumia wewe ni sumu.anachimba mizizi na kuchemshwa niliokwenda nao wamekwisha tupa sindano za insulin na wenye HIV/AIDS waliokuwa wanatumia ARV wameacha na wanaendelea vizuri,mchungaji anashauri uende na mkeo au mumeo kwani ilimpate tiba wote kuondoa maambukizi mapya,kwa wagonjwa wa ukimwi nimepata ushuhuda kwa watu watatu tofauti ambao ndugu zao wanaendelea vizuri mmoja kapona kabisa nilisahau kuchukua namba yake ya simu maana anagawa ili awape watu ushuhuda
Dawa hii inafanyakazi ifuatavyo kama alivyoeleza muinjilisti,baada ya kunywa unakaa siku saba ndio ukapime hospitali yawezekana ukapata matokeo mazuri katika muda huo au la kama la ongeza tena siku saba kwa dozi ileile maana kwa ukimwi anasema ukinywa tu ile dawa inazuia kabisa virus kushambulia kinga za mwili na wanabakia kuhangaika na kufa taratibu mpaka wanakwisha,kwa nini anasema uende na mwenzi wako ni kwa vile kama wote mmeathirika na mmoja amekunywa dawa ukilala na mwenzako atakuambukiza tena na utasema dawa haikukusaidia.
Imenibidi nichangie kidogo na niwape mwanga nini kilitokea huko ila ni kweli ninawajua niliokwenda nao walikuwa wagonjwa sana wa vidonda vya tumbo baada ya siku tatu tu wameanza kunywa pombe kwa sana na hawajadhurika kama awali
magonjwa anayotibu ni wakwanza kuoteshwa ni
ukimwi,2.kisukari na viambata vyake kama presha na kadhalika,3vidonda vya tumbo na viambata vyake,4.Kansa,baada ya hapo akapewa magonjwa mengine
pumu,kifafa mengine hajui ila kwa kumuamini mungu wako unaweza kuomba akuondolee na magonjwa mengine ambayo wewe unaumwa lakini yeye hakuoteshwa inawezeka ukapona yeye hawezi kuyasemea
Hakuna kusema wala kumwambia kuwa wewe unaumwa nini.Baada ya kupewa historia fupi ndio anawaelekeza kupanga foleni kuelekea kwenye nyumba yake ambayo ni ndogo kwa kweli na yeye mwenyewe ndio ankumiminia hiyo dawa katika kikombe ulichopewa baada ya hapo unasogea mbele kuna watu wanapokea TZS 500 yako naunasogea hatua nyingine na kunywa hiyo dawa,haina uchungu kabisa.
mimi naendelea kufuatilia watu wengi waliokunywa nijue uponaji wao japo na mimi naendelea vizuri wenye kisukari tunakaa 2 weeks baada ya hapo tukula kila kitu bila shida,bado sijamaliza nikimaliza nitawapa taarifa.
Taarifa nilizopata wa jamaa zangu wa Atown wanasema leo hii kuna watu wasiopungua 5,000 huko na kama ni hivyo basi ni hatari kubwa,nimejaribu kufanya utafiti pia idadi kubwa ya watu wanasafiri kwa mabasi toka sehemu mbalili kuelekea huko,hata ndege ni shida sasa hivi,matajiri kwa masikini wanakwenda huko.Magari ya kutembeza watalii wamepata high season ya wagonjwa