Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Inaelekea kuna usanii katika hili swala, kwa maana nime note kuna contradiction ya mahali alipo huyu mchungaji wengine wanasema yupo arumeru, wengine wanasema yupo loliondo, wengine engaruka wengine karatu, wengine mto wa mbu (?sijui labda ana hama hama)

Yuko loliondo, wanaosema engaruka, m/mbu, karatu nk wanashindwa kutofautisha hizo sehemu.

Kama tatizo ni HIV unatakiwa kupima baada ya 7days ukishatumia dawa, wenye sukari anakwambia ukishatumia dawa unaweza kuburudika na coca cola ukiwa njiani unarudi!

Ukipenda anakuonesha mti anaoutumia ila ukiuchukua wewe sio dawa, ukichukua dawa kwake ukampelekea mgonjwa home haifanyi kazi ni mpaka uende mwenyewe akupe dawa unywe ndipo unapona!

Habari ndio hiyo, ukiambukizwa mara ya pili (HIV) NO tiba!
 
Kwa wale wanalikuwa Bukoba miaka ya 2000, kuibuka kwa wagaganga wa namna hii haitakuwa jambo geni kwao. Nakumbuka yule wa Bukoba alitokea sehemu za LUKURUNGO. Naye alikuwa anatoa DAWA YA UKIMWI BURE.

Habari ikaenea, watu maelfu kwa maelfu wakaanza kujazana huko, gari zikapata ruti mpya, biashara za usafiri, maji, chakula na mengine zikashamiri. Utalii wa ndani kuzuru kijiji cha LUKURUNGO ukashamiri. Mwisho wa mambo hakuna aliyepona na mgaga alipata promo ya mdomo-kwa-mdomo (Word of Mouth) na habari zake kusambaa kama moto wa kifuu akapotea ghafla na zisifahamike tena nyendo zake.

Sisemi huyo wa Loliondo naye atakuwa kama huyu; bali nawashirikisheni tukio/uzoefu ili muamue. Ili kama ni historia/hadithi mpya inatokea basi isituache tumeduwaa na matumaini feki kama DECI
 
Nimempeleka mzee wangu jtano,leo asubuhi kaenda kuchek sukari ipo normal..na kidonda cha mguu maji yamekauka.cna mengi.
 
mbona kila mtu anasema "KUNA MTU KAENDA....KUNA MTU KAENDA".......mi nataka kumsikia huyo MTU KAENDA aje hapa aseme mwenyewe.....acheni uzushi.

Ha haaa!
Yani ukiona mtu anakuaminisha kuwa kuna jamaa au rafiki au ndugu yake nk kuwa ameenda huko ujue kaenda mwenyewe (japo si wote). Soma alama za nyakati mkuu. Na hii inatokana na HIV kuwepo kwenye orodha, anaogopa asije kuwa marked.
 
WiseLady, hii habari ina ukweli lakini wasije watu wakafunga safari kutoka mbali mpaka arumeru wakakuta patupu!!!:A S 13:

ni LOLIONDO MKUU,SIO ARUMERU ABOUT 400KM FROM ARUSHA TOWN....NAURI NI 50.000-70,000Tsh
 
Kuna mtu kaenda mwanzo mwanzo kabla hajavuma huyo mzee, kapima bado ni hiv positive, huenda imani yake haijamponya... Ukienda uwe na imani
 
Kwa wale wanalikuwa Bukoba miaka ya 2000, kuibuka kwa wagaganga wa namna hii haitakuwa jambo geni kwao. Nakumbuka yule wa Bukoba alitokea sehemu za LUKURUNGO. Naye alikuwa anatoa DAWA YA UKIMWI BURE.

Habari ikaenea, watu maelfu kwa maelfu wakaanza kujazana huko, gari zikapata ruti mpya, biashara za usafiri, maji, chakula na mengine zikashamiri. Utalii wa ndani kuzuru kijiji cha LUKURUNGO ukashamiri. Mwisho wa mambo hakuna aliyepona na mgaga alipata promo ya mdomo-kwa-mdomo (Word of Mouth) na habari zake kusambaa kama moto wa kifuu akapotea ghafla na zisifahamike tena nyendo zake.

Sisemi huyo wa Loliondo naye atakuwa kama huyu; bali nawashirikisheni tukio/uzoefu ili muamue. Ili kama ni historia/hadithi mpya inatokea basi isituache tumeduwaa na matumaini feki kama DECI

sure!kati ya 1996 na 1997,pale Ihungo pia alikuwepo padri mmoja aliyedai ametokewa na ameonyweshwa dawa ya kutibu ukimwi.Watu walimiminika sana,lakini kwa habari zisizo za uhakika inasemekana alizuiwa kuendelea kutibu na uongozi wa kanisa kwa kudai kuwa lazima apate kibali toka Roma. Wengi wametokea ,Hata Karagwe yupo mama mmoja alitokea miaka ya 1988-1990.
 
We got a letter from Loliondo:

MAFISADI WANAPORA ARDHI YA WANANCHI LOLIONDO;

Loliondo ni makao makuu ya wilaya ya Ngorongoro ambapo kumekuwa na migogoro mingi ya ardhi baina ya wawekezaji na wananchi. katika migogoro hizi serikali imeshindwa kusuluhisha kwa kuwa kumekuwa na tuhuma nyingi dhidi yake za kutetea wawekezaji huko wananchi wakipata unyanyasanyi ya kila aina. Wawekezaji hawa ni Kampuni ya Ortelo Business Coorperation(OBC), ambayo Mmiliki ni mwarabu wa dubai na inayofanya biashara ya Uwindaji wa wanyama pori.

Katika gazeti la RAi la jana, kuna mwandishi moja ambaye ameandika makala mengi juu ya mgogoro huo akiisifu kampuni kwamba imewasaidia wananchi kwa kusomesha wanafunzi Vyuo vikuu na sekondari kwa gharama isiopungua Tzsh 38,milioni, huu ni uzushi usiokuwa na ukweli wowote; na kwa kukanusha hili naomba naomba niweke bayana mabo yafuatayo;

1.Shule ya sekondari ya Loliondo, ukarabati ya hospitali ya wasso anazodai mwandishi wa gazeti hilo hilo kuwa zimefanywa na Kampuni hiyo sio kweli badala yake yalifanywa na msamaria moja anaefahamika kwa jina la MALALA wa Kampuni ya ABUDHABI. Pia hakuna katika recodi za vijiji wanafunzi wanaosomeshwa na Kampuni hiyo.

2.Mwaka 2009 Kampuni hii kwa kushirikiana na serikali ilipitisha operesheni ya FFU ambayo iliwaondoa wafugaji wa kimaasai ktk eneo hilo ambalo wamekaa miaka nenda rudi, na kuchoma makazi yao (maboma), maghala ya mahindi, mali zenye dhamani kubwa sana, watu kupigwa na wanawake kudhalilishwa, kupotea kwa maefu ya mifugo, hivyo kusabisha ufukara wa kutisha kwa wafugaji hao.

3. Kitalu hiki kimepakana na hifadhi ya taifa ya Serengeti ampapo wanyama wanaowindwa ni wale wanaotoka ndani ya hifadhi hiyo.

4. Imejenga majengo makubwa na ya kudumu katika chanzo cha maji(mto alasai) ambayo ndiyo uhai wa Ekologia ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti na watu wa vijiji husika.

5. Eneo hilohilo ndilo korido la wanyamapori wanapokuwa wanahama kutoka serengeti-Maasai mara kenya na ambapo wamejenga uwanja kubwa wa ndege ambayo ni kikwazo kikubwa kwa wanyama pori na ekologia ya serengeti kwa ujumla.

6.Eneo hilo lina mawsiliano ya aina yake ambapo uukifika inakuandikia kwa sms "wecome tu united Arabs Emirates.........." sasa tunashindwa kuelewa ni Nchi ndani ya nchi ama ni nini? na pia kabla ya kuanikwa kwa ripoti ya CSOs ijulikanayo kama FEMAct ya 2009, magari ya kampuni hiyo yalikuwa na number za usajili za Dubai, sasa kama sio kuujumu uchumi wa nchi ni nini?

''Nawaomba wazalendo na wanaharakati wa haki za binadamu tusaidiane katika hili.
''
 
JK ofa hii itampita manake yupo safarini kila siku wakati afya mgogoro.

Kwa habari zisizo rasmi Mkwere na mkewe wameshapata tiba kwake kabla ya kusafiri. EL nae alienda na mkwara wa kutoshuka kutoka kwenye gari eti apelekewe huko, Dr kamgomea kuwa watu wote lazima wafike kwa Dr na kupewa na Dr sio kuagiziwa.

Wengine niliosikia wamesharipoti huko ni Dr Magufuli, ila wote hao sijui walikuwa na shida gani.
 
Imenibidi nitoke Dar leo asubuhi to Arusha. My mother had visited the pastor last week, she was suffering heart and pressure for 3 years nimemkuta 2 hours ago anadunda kaa demu somebody of 60 yrs siamini. Kesho kutwa baba yangu mdogo mwenye shida ya kisukari anaondoka pia kuelekea huko. Sasa sijui niamini au nisubiri kwanza????
 
Alafu Felister wewe unatibu ukimwi au unatibu watu kuacha ngono haha.....

Inawezekana wewe ni yule niliekwambia hakuna mwanamke atakaye kukubali kutembea nje ya ndoa na kila uliye naye ambaye si mkeo atazua ugomvi muachane, kwa amri hii ni mpaka milele umechoka kukaa kwenye kifungo au hahaaaaaa! Kama ndiye aise siku hizi nakosa wakuchat naye hapa kwenye baridi..hamjambo huko? Wawekee huo ushuhuda basi nipate wateja wakuamini jina la Yesu......
 
Je anatibu magonjwa tuau anatoa na dawa kwa wenye shida yakupata mtoto? Plz nijuzen jaman nina ndugu yangu anashida hiyo. Na je wenye HIV walioanza kutumia dawa nao wanapona?
Kwanza kabisa mimi binafsi nawasibitishia kuwa naendelea vizuri mpaka sasa japo sijafikisha 7 days,nilikuwa huko kwa ajili ya kale kaugonjwa kangu kama nilivyowahi kuwauliza mtu mwenye kisukari chakula chake ni nini katika moja ya POST zangu na ninashukuru wana JF walinipa miongozo mingi na nilikuwa naifuata sana ila vingine nimeacha.baada ya kumsiki rafiki yangu alinichukua tarehe 27.02.2011 tulindoka arusha mjini yapata saa 10.00 alfajili,ni mwendo mrefu sana ni zaidi ya kilomita 330 kwenda tulifika saa 5 asubuhi,barabara ni mbaya gari inayoweza kuvumili ni yale yanayobeba watalii cruser na landrover nazo zikirudi ni matengenezo makubwa, ubebaji kidogo ni abiria 15 na kuendelea kila kichwa 70'000 mpaka 100,000.00,siku hiyo gari zilikuwa zaidi ya 150 na tarehe 26 rekodi tuliyoikuta kenye mpaka wa monduli na loliondo ilikuwa zaidi ya gari 300,kwa kweli nishagaa sana kwani ni umati mkubwa sana.Cha kwanza kabisa tuliorodhesha majiana na kumkabidhi alitupatia tiba ya dharura kwani alisema jumapili ni siku ya kupunzika baada ya kutoka kwenye ibada hivyo tulianza kutibiwa saa 8 mchana ilikuwa shughuli kila mtu anataka kuwa wa kwanza kupona.
Kuhusu TIBA ni kikombe kimoja tu kwakila mgonjwa,nilikuta wahindi,waarabu na hata wenzetu wa jirani afrika mashariki,kabla hujanywa dawa ni lazima akueleza dawa hiyo imepatikana vipi na ni ndoto toka wa mungu,mti wenyewe unasemekana ukiutumia wewe ni sumu.anachimba mizizi na kuchemshwa niliokwenda nao wamekwisha tupa sindano za insulin na wenye HIV/AIDS waliokuwa wanatumia ARV wameacha na wanaendelea vizuri,mchungaji anashauri uende na mkeo au mumeo kwani ilimpate tiba wote kuondoa maambukizi mapya,kwa wagonjwa wa ukimwi nimepata ushuhuda kwa watu watatu tofauti ambao ndugu zao wanaendelea vizuri mmoja kapona kabisa nilisahau kuchukua namba yake ya simu maana anagawa ili awape watu ushuhuda
Dawa hii inafanyakazi ifuatavyo kama alivyoeleza muinjilisti,baada ya kunywa unakaa siku saba ndio ukapime hospitali yawezekana ukapata matokeo mazuri katika muda huo au la kama la ongeza tena siku saba kwa dozi ileile maana kwa ukimwi anasema ukinywa tu ile dawa inazuia kabisa virus kushambulia kinga za mwili na wanabakia kuhangaika na kufa taratibu mpaka wanakwisha,kwa nini anasema uende na mwenzi wako ni kwa vile kama wote mmeathirika na mmoja amekunywa dawa ukilala na mwenzako atakuambukiza tena na utasema dawa haikukusaidia.
Imenibidi nichangie kidogo na niwape mwanga nini kilitokea huko ila ni kweli ninawajua niliokwenda nao walikuwa wagonjwa sana wa vidonda vya tumbo baada ya siku tatu tu wameanza kunywa pombe kwa sana na hawajadhurika kama awali
magonjwa anayotibu ni wakwanza kuoteshwa ni ukimwi,2.kisukari na viambata vyake kama presha na kadhalika,3vidonda vya tumbo na viambata vyake,4.Kansa,baada ya hapo akapewa magonjwa mengine pumu,kifafa mengine hajui ila kwa kumuamini mungu wako unaweza kuomba akuondolee na magonjwa mengine ambayo wewe unaumwa lakini yeye hakuoteshwa inawezeka ukapona yeye hawezi kuyasemea
Hakuna kusema wala kumwambia kuwa wewe unaumwa nini.Baada ya kupewa historia fupi ndio anawaelekeza kupanga foleni kuelekea kwenye nyumba yake ambayo ni ndogo kwa kweli na yeye mwenyewe ndio ankumiminia hiyo dawa katika kikombe ulichopewa baada ya hapo unasogea mbele kuna watu wanapokea TZS 500 yako naunasogea hatua nyingine na kunywa hiyo dawa,haina uchungu kabisa.
mimi naendelea kufuatilia watu wengi waliokunywa nijue uponaji wao japo na mimi naendelea vizuri wenye kisukari tunakaa 2 weeks baada ya hapo tukula kila kitu bila shida,bado sijamaliza nikimaliza nitawapa taarifa.
Taarifa nilizopata wa jamaa zangu wa Atown wanasema leo hii kuna watu wasiopungua 5,000 huko na kama ni hivyo basi ni hatari kubwa,nimejaribu kufanya utafiti pia idadi kubwa ya watu wanasafiri kwa mabasi toka sehemu mbalili kuelekea huko,hata ndege ni shida sasa hivi,matajiri kwa masikini wanakwenda huko.Magari ya kutembeza watalii wamepata high season ya wagonjwa
 
Au jamani huu ndio utabiri ya shekhe yahaya husein, kwamba dawa za magonjwa sugu zitagunduliwa
 
Well ndugu baada ya taarifa za hapa JF juzi jumatano tuliondoka kama gari 8 zote zilikuwa zimejaa! Tuliondoka Moshi kiasi cha saa 3.50 hivi usiku tlifika alhamisi ya tarehe 3/3 saa mbili asubuhi. Umati tulikuta sijapata kuona maishani mwangu. Nauli ilikuwa shilingi laki moja kwenda na kurudi. Ilibidi tutumie ujanja wa kimjini tuweze kupata dawa. Asikwambie mtu kuna watu toka sehemu malimbali hapa Tanzania na jirani pia bila kusahau ndugu zetu suche! Kuna watu ambao waliletwa wakiwa wamebebwa kwenye magodoro. Siwezi kutoa ushahidi hapa kuwa namshuhudia nani kuwa ni nani kaweza kupona maana wanasema kuwa majibu baada ya siku saba. Nitarudi kuwapa taarifa za ni wangapi wamepona baada ya kupata taarfa kamili toka kwa wale niliosafiri nao. Binafsi nilimpeleka mke wangu kwa matatizo ya kuumwa kichwa. Niapoandika ujumbe huu yuko fit kabisa ni uchovu tu maana barabara ni mbaya kabisa. Jana wakati narudi mida ya saa 5 usiku nilikuta msafara wa magari yasiyopungua 50 wakielekea huko. Km 175 toka njia panda ya Kigongoni karibu na Mto wa Mbu kupitia Engaruka, Lake natron hadi Kwa Mchungaji ni mwendo wa masaa 6 hadi 7 kutegemea ni aina gani ya gari uko nayo. Sikushauri utumie gari ndogo, landcruiser ama Landrover is ideal though some 4WD of any type can do.
Nitarudi tena siku zijazo ka ushuhuda zaidi. Kwa sasa mnaweza kuniuliza maswali na nitajitahidi kujibu kwa kile nilichokiona.
Mbarikiwe sana.

Umempa Yesu maisha baada ya huo muujiza? His concern is the salvation of your spirit hayo mengine ni incentive tu za kukupa mbegu ya Imani ila kuzaa kwa mbegu itategemea imepandwa kwenye udongo gani, some zinaangukaga njiani ndege wanaokota hao ndege nimewaona wengi hapa JF wakisha iokota utaona kidogo kidogo ile value ya huo ushuhuda inapungua as days proceed, wakati mwingine inaangukaga kwenye miiba utaanza visingizio ooh leo sitaki kusikiliza mahubiri maana ninakazi nyingi na ile ari na viapo ulivyovitoa kwa furaha ya kuona mkeo amepona inaanza ku fade away taratibu....So if you continue with your humble heart ya kusikiliza wenye habari njema zaidi ya huo mchungaji kuna package mbali mbali zaidi ya healing miracle utaendelea kupokea na ukifungua huko ndani utakuta peace, financial break through, opportunities, right people to take you to your destiny earlier than you could imagine etc ndiyo hapo inapoanguka kwenye udongo mzuri moja huzaa mia, nyingine sitini na nyingine thelathini. Cha msingi ni kuwa huyo mkeo hajapokea uponyaji wake tu kama kweli huyo ni mtumishi wa Mungu lakini pia na anointing ya kutibu wengine wenye shida kama yake so aanze kutumia hiyo karama ili kuichochea kila anapokutana na mwenye hitaji ndiyo maana Yesu akasema kama baba alivyonituma nami pia ninawatuma kupeleka hii habari njema kwa mataifa ili nao wapate kupona....

I hope umenipata na ubarikiwe sana.
 
Kwanza kabisa mimi binafsi nawasibitishia kuwa naendelea vizuri mpaka sasa japo sijafikisha 7 days,nilikuwa huko kwa ajili ya kale kaugonjwa kangu kama nilivyowahi kuwauliza mtu mwenye kisukari chakula chake ni nini katika moja ya POST zangu na ninashukuru wana JF walinipa miongozo mingi na nilikuwa naifuata sana ila vingine nimeacha.baada ya kumsiki rafiki yangu alinichukua tarehe 27.02.2011 tulindoka arusha mjini yapata saa 10.00 alfajili,ni mwendo mrefu sana ni zaidi ya kilomita 330 kwenda tulifika saa 5 asubuhi,barabara ni mbaya gari inayoweza kuvumili ni yale yanayobeba watalii cruser na landrover nazo zikirudi ni matengenezo makubwa, ubebaji kidogo ni abiria 15 na kuendelea kila kichwa 70'000 mpaka 100,000.00,siku hiyo gari zilikuwa zaidi ya 150 na tarehe 26 rekodi tuliyoikuta kenye mpaka wa monduli na loliondo ilikuwa zaidi ya gari 300,kwa kweli nishagaa sana kwani ni umati mkubwa sana.Cha kwanza kabisa tuliorodhesha majiana na kumkabidhi alitupatia tiba ya dharura kwani alisema jumapili ni siku ya kupunzika baada ya kutoka kwenye ibada hivyo tulianza kutibiwa saa 8 mchana ilikuwa shughuli kila mtu anataka kuwa wa kwanza kupona.
Kuhusu TIBA ni kikombe kimoja tu kwakila mgonjwa,nilikuta wahindi,waarabu na hata wenzetu wa jirani afrika mashariki,kabla hujanywa dawa ni lazima akueleza dawa hiyo imepatikana vipi na ni ndoto toka wa mungu,mti wenyewe unasemekana ukiutumia wewe ni sumu.anachimba mizizi na kuchemshwa niliokwenda nao wamekwisha tupa sindano za insulin na wenye HIV/AIDS waliokuwa wanatumia ARV wameacha na wanaendelea vizuri,mchungaji anashauri uende na mkeo au mumeo kwani ilimpate tiba wote kuondoa maambukizi mapya,kwa wagonjwa wa ukimwi nimepata ushuhuda kwa watu watatu tofauti ambao ndugu zao wanaendelea vizuri mmoja kapona kabisa nilisahau kuchukua namba yake ya simu maana anagawa ili awape watu ushuhuda
Dawa hii inafanyakazi ifuatavyo kama alivyoeleza muinjilisti,baada ya kunywa unakaa siku saba ndio ukapime hospitali yawezekana ukapata matokeo mazuri katika muda huo au la kama la ongeza tena siku saba kwa dozi ileile maana kwa ukimwi anasema ukinywa tu ile dawa inazuia kabisa virus kushambulia kinga za mwili na wanabakia kuhangaika na kufa taratibu mpaka wanakwisha,kwa nini anasema uende na mwenzi wako ni kwa vile kama wote mmeathirika na mmoja amekunywa dawa ukilala na mwenzako atakuambukiza tena na utasema dawa haikukusaidia.
Imenibidi nichangie kidogo na niwape mwanga nini kilitokea huko ila ni kweli ninawajua niliokwenda nao walikuwa wagonjwa sana wa vidonda vya tumbo baada ya siku tatu tu wameanza kunywa pombe kwa sana na hawajadhurika kama awali
magonjwa anayotibu ni wakwanza kuoteshwa ni ukimwi,2.kisukari na viambata vyake kama presha na kadhalika,3vidonda vya tumbo na viambata vyake,4.Kansa,baada ya hapo akapewa magonjwa mengine pumu,kifafa mengine hajui ila kwa kumuamini mungu wako unaweza kuomba akuondolee na magonjwa mengine ambayo wewe unaumwa lakini yeye hakuoteshwa inawezeka ukapona yeye hawezi kuyasemea
Hakuna kusema wala kumwambia kuwa wewe unaumwa nini.Baada ya kupewa historia fupi ndio anawaelekeza kupanga foleni kuelekea kwenye nyumba yake ambayo ni ndogo kwa kweli na yeye mwenyewe ndio ankumiminia hiyo dawa katika kikombe ulichopewa baada ya hapo unasogea mbele kuna watu wanapokea TZS 500 yako naunasogea hatua nyingine na kunywa hiyo dawa,haina uchungu kabisa.
mimi naendelea kufuatilia watu wengi waliokunywa nijue uponaji wao japo na mimi naendelea vizuri wenye kisukari tunakaa 2 weeks baada ya hapo tukula kila kitu bila shida,bado sijamaliza nikimaliza nitawapa taarifa.
Taarifa nilizopata wa jamaa zangu wa Atown wanasema leo hii kuna watu wasiopungua 5,000 huko na kama ni hivyo basi ni hatari kubwa,nimejaribu kufanya utafiti pia idadi kubwa ya watu wanasafiri kwa mabasi toka sehemu mbalili kuelekea huko,hata ndege ni shida sasa hivi,matajiri kwa masikini wanakwenda huko.Magari ya kutembeza watalii wamepata high season ya wagonjwa

Habari nilizo zipata toka huko kuna magari zaidi ya 1000 na kazi hiyo inasimamiwa FFU,ilitokea fujo na hii inatokana na idadi kubwa ya watu,ukichukua average ya watu 10 kila gari inamaana kuna watu wanaozidi 15,000.
 
Jamani kutokana na umati uliopo nawashauri kubeba vyakula vya kutosha watu wanaongezeka kila dakika.
 
Back
Top Bottom