Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Tunatoa wito tena tukimaanisha: Babu alazimishwe ahamishie kituo Arusha!!

https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/115672-wito-mganga-wa-loliondo-afanyie-shughuli-zake-arusha.html

Kuna taarifa kuwa mgonjwa mmoja mwenye asili ya ki-asia amepoteza maisha baada ya kuzidiwa kwenye foleni ya kusubiri tiba ya mchungaji wa loliondo.
Inasemekana viongozi wa kiserikali na matajiri wakubwa wanatumia nyadhifa zao 'kuchakachua' na kuwaacha walalahoi wakisubiri foleni.
USHAURI:Chonde chonde wagonjwa mnaoenda huko chukueni dawa zenu za kawaida kwani huduma inachelewa sana.

Tunatoa wito Mganga ahamishie shughuli zake arusha...anafanya nini huko porini????

https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/115672-wito-mganga-wa-loliondo-afanyie-shughuli-zake-arusha.html
 
Mimi naamini ni neema za m.mungu kwani katika vitabu vya dini mungu anasema kila ugonjea una dawa yake.tatizo wabongo wenye usafiri ndo tumeona tunufaikie hapo ila si vyema.wekeni nauli ya kawaida tu
 
RIP ila halazimishwi mtu kwenda ni suala la ubinadamu kama alikuwa kazidiwa angewaomba wa mbele wampeleke au njaa kwani wengi vyakula vimewaishia
 
wakati tunatoka huku kumchukua shemeji magari yalikuwa mengi sana kwa kukadiria ni kama 2000.... na yamepaki barabarani....ile nageuza gari nikapishana na makamba nae....nimemwacha huko.

Haina mantiki yeyote. Kwanini mtu mmoja awafanye watanzania wote wamfuate huko porini?
Cha ajabu viongozi nao wanunga msafara .... Kwani ni ushirikina????

Huyu mtu alazimishwe ahimishie kituo mahali ambapo ni rahisi kijamii kufikiwa na kumonitor kazi zake na wagonjwa wanomfuata.
 
Mimi nafkiri ni muujiza wa mungu na hivyo serikali iwasaidie wale waliopo hospitali wenye cancer wasafirishwe wapate tiba hiyo ya babu ili wapone turudishe nguvu kazi.
 
Tunamuombea kwa mungu alale pema huyo aliyefariki,kwakweli alikuwa anajitahidi kuokoa maisha yake angalau kwa huyo babu wa loliondo
 
Hii isiwe ni dogma ... alternative medicine ziko dunia nzima..
..ziko chinese medicine...ziko indian medicine... ziko German medicine... NA ZOTE ZINAHAKISHIKA

Kama ni spiritual healing..Wako Spiritual leaders wangapi wanasafiri nchi nzima...

Inakuwaje yeye awe tofauti na wengine wote?

TUNASISITIZA ATOKE HUKO ALIPO AJE ARUSHA ...
NA TIBA YAKE IWE OFFICIAL TO MEET INTERNATIONAL STANDARDS...za tiba mbadala! What is the big issue on here?

Ni simple. Ukiitaka dawa nenda loliondo. Hutaki Acha. Mambo ya international standards, official, uduni wa huduma za kijamii katika eneo la kutolea huduma yeye hayamhusu. Anachosema ni kwamba, unataka dawa nenda, ila hakuiti wala hakulazimishi. utajua mwenyewe namna ya kukabiliana na changamoto utakazozikuta. as simple as that.
 
Typical supersticious mind set!!!!!
 
Wa TZ tunapenda majibu rahisi kwa matatizo makubwa, na tunapenda sana shortcuts, hapo ndyo jamaa wana-take advantage ya kutengeza feza. yule mganga alionekana kuwa terrified kwa sababu hakutegemea kama watu wangejitokeza kwa wingi vile, yeye alikuwa anafanya majaribio yake kijijini, sasa imekuwa balaaa.
 
jamani kuna tetesi eti babu anasitisha huduma coz ya kwaresma.hii iko vp,maana nilijiandaa ku mvisit this week.
 
Hii ndio inatupa hali halisi ya Ugonjwa kwamba kumbe hali ni mbaya kuliko tunavyodhania!
 
Haina mantiki yeyote. Kwanini mtu mmoja awafanye watanzania wote wamfuate huko porini?
Cha ajabu viongozi nao wanunga msafara .... Kwani ni ushirikina????

Huyu mtu alazimishwe ahimishie kituo mahali ambapo ni rahisi kijamii kufikiwa na kumonitor kazi zake na wagonjwa wanomfuata.

kwani ni lazima atoe huduma?
Atatoa kwa watakaoenda kwake.
Kama hutaki usiende huko.
Btw. Kuna haja ya kufanya dharura kuweka mazingira safi na salama kwa wahitaji wa huduma hiyo.
Kama ni ushirikina au la nadhani wanopata tiba hiyo na kupona hawatakuelewa, kwao kupona ni muhimu zaidi.
 
Typical supersticious mind set!!!!!

Take it the way u like, but habari ndo hiyo na watu wamepona. Iwe ni uchawi, Mungu, Mashetani nk...... Ndo huduma anayoitoa babu na watu wameipenda na wanaihitaji sana, na yeye kaweka terms and conditions .."Anaetaka aje Loliondo na sh 500." We ukiona haiko kwenye standards na mazingira ya kule huwezi kukabiliana nayo, potezea. Mbona hospitali zipo kibao tu na wataalam tena maprofesa wapo kibao tuu? Anaeenda kule lazima ajue in advance mazingira anayoenda kukumbana nayo na ajue jinsi ya kuyakabili.
 
Nasikia hata JK ana mpango wa kwenda ili aiwahi j5.

kaka tayari amekunywa juice ya babu.......makamba nimepishana nae wakati sisi tunatoka huko...shemeji yangu amepona kisukari kabisa
 
Back
Top Bottom