Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

kwani ni lazima atoe huduma?
Atatoa kwa watakaoenda kwake.
Kama hutaki usiende huko.
Btw. Kuna haja ya kufanya dharura kuweka mazingira safi na salama kwa wahitaji wa huduma hiyo.
Kama ni ushirikina au la nadhani wanopata tiba hiyo na kupona hawatakuelewa, kwao kupona ni muhimu zaidi.

Get It very clear ..!!!

Sijasema tiba wala huduma ni superstious..

LAKINI

Nimesema .....KAMA HAIHAMISHIKI ......

Tuelezwe ni kwa nini? Kama haina maelezo ..ndio nikauuliza ..Is it Superstisous?

Kama sio...Ihamishwe kurahisisha huduma yenyewe..sijaipinga!

Huduma itolewe ..lakini irahisishwe...kwanini Tanzania yote ..ifuate mtu mmoja katikati porini huko??
 
Dawa zake hazitakiwi kuhamishwa katika eneo lake!Waimalishe infrastructure huko huko!
nakubaliaana na wewe, mgeni njoo mwenyeji apone, watengeneze basi,si wameona miundombinu ilivyo mibovu, kama walikuwa hawajui, sasa wanajua
 
jana nawapigia simu ndugu zangu niende kuwasalim wk end!! eti wananiambia wako safarini loliondo

mmmhh haya sasa!!
 
nakubaliaana na wewe, mgeni njoo mwenyeji apone, watengeneze basi,si wameona miundombinu ilivyo mibovu, kama walikuwa hawajui, sasa wanajua

Kama hao watu wanao teseka wakisubiri huduma kwenye foleni usiku na mchana hadi siku tatu nk..wangekuwa sio wagonjwa...tena wagonjwa ... wa magonjwa sugu ningekubaliana wewe!
Vinginevyo NO!

Babu ahamie sehemu ambayo itarahisisha Watanzania kupata huduma!
 
If you are out to describe the truth, leave elegance to the tailor.
 
RIP

Kusipoanzishwa management nzuri ya hilo kusanyiko linalozidi kukua maafa zaidi yatatokea.
 
SIMWAMINI HUYO BABU HATA KIDOGO.Inawezekana akawa anapiga janja ya shehe YAHYA

umeshaambiwa hapigi ramli, wala haangalii kiganja, unafika kikombe chako unamiminiwa dawa unaondoka, tatizo watu mko kama Tomaso bila kugusa hamuamini.
 
Amezua vita na Makanisa ya uponyaji waumini wamepungua leo nimesoma Askofu Zachary Kakobe akimponda babu na kusema atazivunja nguvu zake za giza kama alivyozivunja za Babu wa Tegeta...brief huyu wa Tegeta alikuwa kijana na alidai kuponya magonjwa sugu kama vile Ukimwi. Ila nilichobaini makanisa yaliyoathirika ni haya yanayojijenga kwa njia ya uponyaji na yameaanza kupoteza waumini aka wateja wao wanaokimbilia huko Loliondo.
 
Jamani mbona hamuongelei ishu ya kusimama kwaresima huduma?
 
WanaJF nakwenda Loliondo kwa babu siku ya Jumatano nitawaletea salamu
 
Sawa bandugu! Kila la kheri. Ila jiandae vilivyo nasikia watu ni wengi saaaana kiasi kwamba itakuchukua wiki kadhaa kupata huduma. Anyway wish you luck
 
Du ! kama watendaji wa serikali yetu pamoja na jamaa zao wa karibu wamepata tiba hawaoni kama kuna sababu ya kuwawezesha watanzania wa kawaida kufika huko,je ni mlalahoi gani anayeweza kukodi landcruiser kwenda huko ? wao wantumia ma VX na MAPATROL ya SU,STK,STJ,DFP nk. Hawa ni wa binafsi mno,hakuna hata mmoja aliyetoa mwito wa kuboresha miundo mbinu kule !
 
Kweli watu wanamatatizo!! Pole mkuu...
 
Mkuu ona hii thread! https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/115561-apoteza-maisha-akisubiri-tiba-loliondo.html

Apoteza maisha akisubiri tiba loliondo.
Kuna taarifa kuwa mgonjwa mmoja mwenye asili ya ki-asia amepoteza maisha baada ya kuzidiwa kwenye foleni ya kusubiri tiba ya mchungaji wa loliondo.
Inasemekana viongozi wa kiserikali na matajiri wakubwa wanatumia nyadhifa zao 'kuchakachua' na kuwaacha walalahoi wakisubiri foleni.
USHAURI:Chonde chonde wagonjwa mnaoenda huko chukueni dawa zenu za kawaida kwani huduma inachelewa sana.
Yaani hapa sio kwanini babu analaumiwa labda serikali iweke mfumo wa watu kupanga foleni,maana babu anajitahidi kusaidia watu ila tatizo la watz hatupendi foleni tumezoea vitu vya fasta.

 
Umejiandaa?? Kwa chakula, maradhi, na kila kitu ndugu hakuendeki huko.

Uwe umeomba ruhusa wiki mbili wenzio wamekwenda na kurudi kapa wanawahi kazini
 
Back
Top Bottom