Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Awataka wakazi wa Loliondo, Simanjiro, Mto wa Mbu, Mererani na Arusha yote kufurika kwa wingi siku ya Alhamis hii, atakapotia timu kutoa uponyaji. Atumia mda mwingi kutaja na kurudia rudia namba zake lukuki za simu.

Tofauti ni kuwa BABU hatumii uchawi wowote kama ilivyo kwa NDOI, Halafu babu si mganga wa kienyeji ni ametumwa na mungu naona shetani anataka kuingilia kati kuharibu akili za watu " ASHINDWEEE NA ALEGEEEE NA KUNYONG'ONYEA KABISA"
 
Akina Ndodi wafungiwe hawawasaidii Watu wa kawaida zaidi zaidi wanajinufaisha wao.
Ni wezi
 
wathibitishe dawa ya ukimwi si waseme tu wanakwenda kwa babu kunywa dawa
 
mkuu mlachake tuwauklize wale ndugu zetu sabato masalia waliotuambia-ga watapaa kuelekea ughaibuni bila document yoyote!!!! Naskia walikuwa wanamtaja mtu mmoja wanamwita yesu kuwa ndiye wanaenda kwa nguvu zake wala hawahitaji hata passoprt wala tikit.

Naona na wewee unasema unamwamini huyu yesu, sawa kaka hamna shida amini tu unachotaka mradi usiwabugudhi wenzako kwa imani yako wala usilazimishe kila mtu aamini unachoamini wewe. Mimi mbudha (naskia hata wahindu) hawaamini huyo yesu wako. Naskia waislamu wao wanamwamini allah na mtume mohamed na marastafar wanamwamini jah never die. Kila mtu na imani yake mkuu, tatizo linakukuja pale unapotaka kutumia imani yako kuwadanganya watu waseme "majiiii" ili eti risasi ya jerumani isiingie na badala yake igeuke kuwa maji

we ungekuwa unaumwa then ungeongea haya sikuombei upatwe kansa, but natamani uipate then uambiwe kuna dawa mahali uone kama utaacha, kwani kuwa mhindu sio binadamu wewe? Au unaleta udini hapa? Mbona sheikh yakha ukienda kwake anasemaga na aya z quran kwa yeyote na halalamiki mtu? Kutajwa yesu hapo ni kwa imani ya mkristo, na tunaamini yupo na anatusaidia! Km huamni nakutaminia upate ugonjwa sugu kwani utakuwa wa kwanza kuja kutoa shuhuda hapa jf!
 
teh teh teh..dua la kuku hilo, kwa jina la budha na hindu na sidhuriki ng'o. hindu na budha wakishindwa kunilinda narudi kwa wahenga wangu nachinja mbuzi, namimina mbege na maziwa wazee wakiyapokea natoka gado. kansa zitakuandama wewe unayeombea wenzako ili upate sababu ya kuwalazimishia imani yako.

shekke yahya mwache aendelee coz yeye ana kiti, ndo maana anamlinda mkwere. sasa wewe una kiti?. kama unae njoo tumtoe.....

By the way kama umeumia pole mkuu, najua religion is an opium of the people, hakuna kitu humfanya mtu zuzu kama imani ya dini, ndo maana waskia kuna wajinga wanadanganywa kwa dini wanakuwa radicalised hadi wanakubali kuvaa bomu liwalipukie ili tu eti kuuwa makafiri. na nyie mnaosemasema-ga yesu yesu naskia mishahara yenu mnawapelekea wachungaji wao ndo wanawapangia...lol

sina nia ya kukukashifu kaka ila nina nia ya kuku-free from mental slavery na katika kufanya hivo lazima utaskia uchungu kweli lakn ndo ukweli sasa tufanyeje, japo ni ukweli mgumu kuujua kwa simpo minds.

mkoloni(mzungu na mwarabu) alipokuja afrika alikuja na biblia/quran mkononi akamwabia mwafirika funga macho tusali, mwafirika alipofungua macho akakuta ardhi yote kwishnei.....pole kaka, usiache imani yako ila taratibu taratibu tunakupa na dozi ya upande wa pili, tukiamini utaweza kuipokea na kui-criticalise ili usifuate kama zuzu tu. kwani wewe kaka pia si ni great thinker au? usijekuta nimekutana na .....thinker!!!?
 
ANAYE AMINI NAAMINI ASIYEAMINI NA AGONGE MAMBO ALIYOJIPANGIA KATIKA MAISHA YAKE HAINA HAJA YA KUELEZA SAAAANA :blah:
 
uelewa wako wa mambo finyu sana naona, na unapenda ligi, well and good wewe uamuzi wako kuamua unachotaka haku;alzimishi mtu, about jesus nampenda na ntakufa na imani hiyo maneno yako hayawezi nichange kabisa! pia i dont expect to change u either! but unapenda ligi tu kuwaza ktk thin bw!
 
Mmmh na mimi ngoja niende huko Loliondo kabla wazungu hawajamtwaa babu.
 
Maaskofu: Dawa ya Mwasapile inaponya

  • Ni maaskofu wa KKKT Laizer, Shao na Akyoo

  • Wathibitisha kuwa waliinywa na wameponywa
Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile akiongea na wageni wake waliofuata huduma yake ya tiba nyumbani kwake Loliondo.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limesema linatambua na kubariki dawa inayotolewa na Mchungaji wake mstaafu anayefanyia shughuli zake Loliondo, Ambilikile Mwasapile, huku baadhi ya maaskofu wa kanisa hilo wakithibitisha kwamba wamekunywa dawa hiyo na kuponywa.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kwa njia ya simu, Maaskofu wa kanisa hilo Thomas Laizer wa Dayosisi ya Mkoani Arusha, Dk. Martin Shao wa Dayosisi ya Kaskazini, walisema huduma inayotolewa na Mchungaji Mwasapile ni sahihi na imeanza siku nyingi na kwamba wao ni miongoni mwa watu wa mwanzoni waliowahi kunywa dawa hiyo na kupona.
Askafu Laizer alisema kwa mujibu wa imani na taratibu za KKKT, mchungaji huyo yupo sahihi na Kanisa halina mgogoro naye.

“Ifahamike kwamba kazi ya utoaji dawa haikuanza jana, ilianza siku nyingi na mimi kama Askofu niliyembariki Mchungaji Mwasapile, nililetewa taarifa na wachungaji wengine pamoja na wakuu wangu wa majimbo juu ya mafunuo ya Mchungaji na ndipo tulipoanza kufuatilia na kufanya mahojiano naye na Kanisa likagundua kwamba tiba yake ipo sahihi,” alisema Askofu Laizer.

Askofu Laizer alisema binafsi alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na shinikizo la damu kwa muda mrefu, lakini baada ya kupewa dawa ya mchungaji huyo amepona na hajapata kunywa dawa nyingine.

“Unajua kuna watu wanashangaa kinachofanyika pale, ni kwamba dawa ile inaambatana na sala pamoja na imani,” alisema.

Alisema akiwa kiongozi wa kanisa alipopata habari hizo aliunda jopo la wachungaji kufuatilia kwa kina ufunuo na uwezo wa kuponya wa mchungaji huyo na ikagundulika kwamba hajaenda kinyume cha imani ya KKKT.

Alisema hata mti ambao mchungaji huyo anautumia kuchemsha na kuwapa watu, unajulikana na kila mtu, hivyo hakuna kukengeuka kunakofanywa naye.

“Zaidi sana kinachofanyika pale ni sala na imani, hakuna kitu kibaya tulichokiona sisi kama viongozi wa Kanisa,” alisema.

Pamoja naye aliwataka maaskofu wenzake, ambao walikwenda kumtembelea mchungaji huyo mstaafu kwamba ni Paul Akyoo wa Dayosisi ya Meru aliyefuatana na mkewe, pamoja na Dk. Martin Shao wa Dayosisi ya Kaskazini.

“Mke wa Askofu mwenzangu Akyoo alikuwa hawezi kutoka alikuwa akisumbuliwa na kisukari, lakini baada ya kupewa dawa hiyo juzi nilipompigia simu, akasema amepona na yupo kwenye harusi,” alisema.

Askofu Laizer alisema pamoja na jambo jema linalofanywa na mchungaji huyo, kuna watu wameshaanza kutia fitina kutokana na wivu tu.

Akizungumzia historia ya mchungaji huyo, alisema tangu aanze kazi ya kuchunga kondoo alikuwa mtiifu na mnyenyekevu.

Alisema alimbariki Mwasapile kuwa Mchungaji mwaka 1980 mjini Babati na alikaa eneo hilo kwa miaka saba.
Alisema baada ya hapo alihamia eneo la Sombe ambako alikaa kwa miaka 12.

Kwa upande wake Askofu Dk. Shao alisema anamshukuru Askofu mwenzake Laizer aliyemshirikisha katika msafara huo, pamoja na Akyoo.

Alisema baada ya kufika na kuzungumza na Mchungaji huyo waligundua kwamba hakuna dalili yoyote ya ushirikina katika utoaji wa dawa hiyo wala hakuna udanganyifu wa aina yoyote.

Alisema baada ya kufika huko na kukuta umati wa watu, waliwatoa hufu wagonjwa wote kwamba mtu aliyekuwa akiwapa tiba wanamfahamu na ni mtumishi mwenzao wa muda mrefu.

Alipoulizwa kama na yeye alikunywa dawa hiyo, Askofu Shao alisema: “Nilikunywa, ukishasema kwamba kitu fulani ni halali, basi unatakiwa ushiriki, mimi nilikunywa dawa hiyo, hasa ikizingatiwa kwamba inatibu magonjwa mengi.”

Alisema watu wanaopuuza dawa ya Mchungaji huyo ni wale ambao hawajui njia anazotumia Mwenyezi Mungu kuwaponya watu wake.

Alisema walijadiliana na wagonjwa wote, na kumuuliza maswali kadhaa mchungaji huyo na kubaini kwamba maono aliyopewa na Mungu ni sahihi.

“Mungu ana njia nyingi sana za kugawa vipaji kwa watu wake,”alisema Askofu Shao.
Aliwataka wananchi wote kumuomba Mchungji huyo ili aendelee kuwa na afya, hasa ikizingatiwa kwamba ana majukumu makubwa ya kuhudumia watu kuanzia alfajiri hadi usiku.

“Kwa hiyo sasa tunachojadili ni kumsaidia ili aendelee vema na pia kuhakikisha utaratibu mzuri unakuwepo katika kutoa huduma zake, pia tunaangalia suala zima la mazingira ili mti unaotumika kutibu usitoweke,”alisema.

Source: IPP MEDIA
 
hII HABARI KAMA IKITUMIKA VIZURI UCHUMI WA TANZANIA UTAINUKA NA KUZIPIKU NCHI JIRANI KWANI WAGENI NI WENGI MNO NA BADO KIDOGO TUTAANZA KUPOKEA WAGONJWA KUTOKA ULAYA NA ASIA.

Kikwete, si na wewe ulikunywa? Nenda kawashuhudie wenzako huko Ulaya jinsi uluvyopona ili maraisi wafurike kwetu na kujaza mahoteli yetu. Kawaambie na wwafanyabiashara kuwa tuna dawa ya magonwa sugu na tunagawa kwa senti ya dola.
Magufuli - nadhani na wewe unanisikia, Mahita nawe unanipata, fanyen kama mwenzenu nilvyomuamuru.
 
Aaaah, imani yetu itatuponya.

Ni vema wote waliotumia dawa ya BABU na kupata nafuu watoe ushuhuda ili wengi wapate kutibiwa kwa imani thabiti.

BABU apewe moyo na msaada kuboresha tiba hii kama inasaidia wagonjwa
 
hII HABARI KAMA IKITUMIKA VIZURI UCHUMI WA TANZANIA UTAINUKA NA KUZIPIKU NCHI JIRANI KWANI WAGENI NI WENGI MNO NA BADO KIDOGO TUTAANZA KUPOKEA WAGONJWA KUTOKA ULAYA NA ASIA.

Kikwete, si na wewe ulikunywa? Nenda kawashuhudie wenzako huko Ulaya jinsi uluvyopona ili maraisi wafurike kwetu na kujaza mahoteli yetu. Kawaambie na wwafanyabiashara kuwa tuna dawa ya magonwa sugu na tunagawa kwa senti ya dola.
Magufuli - nadhani na wewe unanisikia, Mahita nawe unanipata, fanyen kama mwenzenu nilvyomuamuru.

Hamna kitu, naskia Babu kapigwa stop na wizara hadi utafiti ufanyike na ajiandikishe kama tabibu mbadala.
Ingekuwa mradi wa mafisadi usingepigwa stop kwa muda.
 
Mgonjwa wa kisukari atoa ushuhuda wa dawa:

656%20loliondo%20pic.jpg

656%20mchungaji%2013.jpg

Some of the patients who thronged Mzee Masapila's compound seeking treatment. http://www.arushatimes.co.tz/front_page_1.htm

Waziri atoa msimamo wa huduma ya Mchg. Loliondo:

Habari za ziada:
"Sitaki kupigwa picha hapa. Unajua hii ni sehemu ya tiba kwa hiyo lazima uheshimu ‘praivesi' zetu (faragha). Tuko hapa kwa sababu tuna matatizo. Si kwa kupenda", alisema ofisa moja wa Serikali mwenye cheo cha juu.

Sababu za vurugu, naelezwa kuwa ni Mchungaji huyo kusitisha kutoa huduma ya kugawa dawa kwa wagonjwa baada ya baadhi ya wagonjwa hao kuvuruga utaratibu uliokwepo wa kupanga foleni ili kupata "kikombe cha dawa ya maajabu".

Nje ya nyumba hiyo na barabara inayopita mbele ya nyumba ya Mchungaji, kuna msururu wa magari na kwa haraka nakadiria kuwa msururu huo una urefu wa Kilomita kama tano na magari yanayozidi 1000 huku magari yenye usaji wa namba za serikali za STK, Mashirika ya Umma (SU) na namba za ubalozi yakitamalaki.

"Kama unavyoona idadi ya watu imeongezeka sana leo. Sasa kuna watu wanataka wapatiwe dawa bila ya kupanga foleni na hiyo tunaona ni ukiukwaji wa taratibu zetu kwasababu kuna watu wengi ambao wako hapa tangu juzi, na bado hawajapata huduma", anaeleza mtumishi huyo.

Mtumishi huyo anaongeza:"Na watu hapa wanaofanya vurugu ni wale ambao wanatoka Arusha. Wengi wanataka kupata huduma wakidhani hapa tunajali umaarufu wao….hapana hapa hakuna mfanyabiashara maarufu, afisa wala kiongozi wa serikali. Watu wanatakiwa kupanga foleni kulingana na muda kila moja aliowasili".

Ana kwa ana na Mchungaji Ambilikile

"Kijana wangu, kama unavyoona, nimezungukwa na idadi kubwa ya watu wanaohitaji huduma; hivyo utanisamehe sana sitakuwa na muda wa kutosha wa kuzungumza na wewe. Nakuomba uniulize kwa kifupi mambo ya msingi kuhusu dawa yangu, nami nitakupa majibu", anaeleza.

Endelea kusoma story:

source: http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=3013 Toleo No 176 la tarehe 9Machi- 16 Machi, 2011
hs3.gif
 
Last edited by a moderator:
Maaskofu: Dawa ya Mwasapile inaponya

  • Ni maaskofu wa KKKT Laizer, Shao na Akyoo

  • Wathibitisha kuwa waliinywa na wameponywa
Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile akiongea na wageni wake waliofuata huduma yake ya tiba nyumbani kwake Loliondo.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limesema linatambua na kubariki dawa inayotolewa na Mchungaji wake mstaafu anayefanyia shughuli zake Loliondo, Ambilikile Mwasapile, huku baadhi ya maaskofu wa kanisa hilo wakithibitisha kwamba wamekunywa dawa hiyo na kuponywa.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kwa njia ya simu, Maaskofu wa kanisa hilo Thomas Laizer wa Dayosisi ya Mkoani Arusha, Dk. Martin Shao wa Dayosisi ya Kaskazini, walisema huduma inayotolewa na Mchungaji Mwasapile ni sahihi na imeanza siku nyingi na kwamba wao ni miongoni mwa watu wa mwanzoni waliowahi kunywa dawa hiyo na kupona.
Askafu Laizer alisema kwa mujibu wa imani na taratibu za KKKT, mchungaji huyo yupo sahihi na Kanisa halina mgogoro naye.

"Ifahamike kwamba kazi ya utoaji dawa haikuanza jana, ilianza siku nyingi na mimi kama Askofu niliyembariki Mchungaji Mwasapile, nililetewa taarifa na wachungaji wengine pamoja na wakuu wangu wa majimbo juu ya mafunuo ya Mchungaji na ndipo tulipoanza kufuatilia na kufanya mahojiano naye na Kanisa likagundua kwamba tiba yake ipo sahihi," alisema Askofu Laizer.

Askofu Laizer alisema binafsi alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na shinikizo la damu kwa muda mrefu, lakini baada ya kupewa dawa ya mchungaji huyo amepona na hajapata kunywa dawa nyingine.

"Unajua kuna watu wanashangaa kinachofanyika pale, ni kwamba dawa ile inaambatana na sala pamoja na imani," alisema.

Alisema akiwa kiongozi wa kanisa alipopata habari hizo aliunda jopo la wachungaji kufuatilia kwa kina ufunuo na uwezo wa kuponya wa mchungaji huyo na ikagundulika kwamba hajaenda kinyume cha imani ya KKKT.

Alisema hata mti ambao mchungaji huyo anautumia kuchemsha na kuwapa watu, unajulikana na kila mtu, hivyo hakuna kukengeuka kunakofanywa naye.

"Zaidi sana kinachofanyika pale ni sala na imani, hakuna kitu kibaya tulichokiona sisi kama viongozi wa Kanisa," alisema.

Pamoja naye aliwataka maaskofu wenzake, ambao walikwenda kumtembelea mchungaji huyo mstaafu kwamba ni Paul Akyoo wa Dayosisi ya Meru aliyefuatana na mkewe, pamoja na Dk. Martin Shao wa Dayosisi ya Kaskazini.

"Mke wa Askofu mwenzangu Akyoo alikuwa hawezi kutoka alikuwa akisumbuliwa na kisukari, lakini baada ya kupewa dawa hiyo juzi nilipompigia simu, akasema amepona na yupo kwenye harusi," alisema.

Askofu Laizer alisema pamoja na jambo jema linalofanywa na mchungaji huyo, kuna watu wameshaanza kutia fitina kutokana na wivu tu.

Akizungumzia historia ya mchungaji huyo, alisema tangu aanze kazi ya kuchunga kondoo alikuwa mtiifu na mnyenyekevu.

Alisema alimbariki Mwasapile kuwa Mchungaji mwaka 1980 mjini Babati na alikaa eneo hilo kwa miaka saba.
Alisema baada ya hapo alihamia eneo la Sombe ambako alikaa kwa miaka 12.

Kwa upande wake Askofu Dk. Shao alisema anamshukuru Askofu mwenzake Laizer aliyemshirikisha katika msafara huo, pamoja na Akyoo.

Alisema baada ya kufika na kuzungumza na Mchungaji huyo waligundua kwamba hakuna dalili yoyote ya ushirikina katika utoaji wa dawa hiyo wala hakuna udanganyifu wa aina yoyote.

Alisema baada ya kufika huko na kukuta umati wa watu, waliwatoa hufu wagonjwa wote kwamba mtu aliyekuwa akiwapa tiba wanamfahamu na ni mtumishi mwenzao wa muda mrefu.

Alipoulizwa kama na yeye alikunywa dawa hiyo, Askofu Shao alisema: "Nilikunywa, ukishasema kwamba kitu fulani ni halali, basi unatakiwa ushiriki, mimi nilikunywa dawa hiyo, hasa ikizingatiwa kwamba inatibu magonjwa mengi."

Alisema watu wanaopuuza dawa ya Mchungaji huyo ni wale ambao hawajui njia anazotumia Mwenyezi Mungu kuwaponya watu wake.

Alisema walijadiliana na wagonjwa wote, na kumuuliza maswali kadhaa mchungaji huyo na kubaini kwamba maono aliyopewa na Mungu ni sahihi.

"Mungu ana njia nyingi sana za kugawa vipaji kwa watu wake,"alisema Askofu Shao.
Aliwataka wananchi wote kumuomba Mchungji huyo ili aendelee kuwa na afya, hasa ikizingatiwa kwamba ana majukumu makubwa ya kuhudumia watu kuanzia alfajiri hadi usiku.

"Kwa hiyo sasa tunachojadili ni kumsaidia ili aendelee vema na pia kuhakikisha utaratibu mzuri unakuwepo katika kutoa huduma zake, pia tunaangalia suala zima la mazingira ili mti unaotumika kutibu usitoweke,"alisema.

Source: IPP MEDIA

Hapo pekundu aliposema Askofu Shao ni busara.
 
Kwanza jina lako linadhihilisha wewe uko hoi, pili nina hakika wewe huna imani na ulimwengu unao ishi. Ukiambiwa hiki ni kivuli chako pia utakataa!!!!!! Sasa waulize watu lukuki waliokwenda Loliondo na mpaka sasa wanakwenda je wanapona????????? Ndg yangu watu wamejaa huko si Waarabu, Wahindi, Wazungu, matajiri ndo usiseme, PM ALIKUWA HUKO, Mkuu wa Boma kaisharudi toka huko. Sijui nikwambie vipi???????? Hayo ni maajabu ya Mungu, ni imani yako tuu. Mwamini Mungu yote yawezekana !!!!!!!!

Mkuu swala ni kuwa sio kutokuwa na Imani, la hasha ,bali kama wanadamu ambae Muweza wa yote ametuumba lazima tutafakari kabla ya kuamini au kupuuza juu yan jambo hili, kwani tumeelezwa na Falsafa za utambuzi kuwa UKIWA KWENYE SHIDA AU FURAHA basi unapofanya uamuzi ni lazima uwe makini na ikibidi ufikiri mara kadhaa uamuzi unaokusudia kuutenda.......... wengi walijuta na kujilaumu....Wanadamu tubadilike kwa kutumia % japo nusu za uwezo wetu wa kufikiri.....Tusifuate tu Mass ya watu bila ya kutafakari..... Dunia inaelekea kulala sasa....
 
Back
Top Bottom