Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

asna hassan(60) --- hawa ndugu zetu si wamekatazwa kwenda huko?
 
Mashahidi wa maradhi ya ukimwi, kisukari wasimulia

na Betty Kangonga na David Frank , Mbeya

amka2.gif
USHUHUDA zaidi umezidi kueleza kwamba tiba inayotolewa Loliondo na Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile (78), inaponya magonjwa mbalimbali sugu yakiwamo magonjwa ya ukimwi na kisukari.
Taarifa za kiushuhuda zilizolifikia Tanzania Daima Jumapili kwa zaidi ya wiki moja sasa kutoka kwa maofisa wa serikali wilayani Ngorongoro na baadhi ya wagonjwa walioeleza kuinywa dawa ya mchungaji huyo maarufu kwa jina la Babu, zimesema tiba hiyo inatibu kwa imani na kwamba tayari wapo wagonjwa kadhaa wa ukimwi waliopimwa hospitalini baada ya kuitumia dawa hiyo na kuonekana hawana virusi vya ugonjwa huo tena.
Mmoja wa mashuhuda wa uponyaji wa tiba hiyo inayotolewa katika Kijiji cha Semunge wilayani humo, ni Mollel Lucas, ambaye amejitambulisha kuwa ni ofisa wa serikali katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro anayeshughulikia masuala ya maendeleo ya jamii.
Kwa mujibu wa Mollel, yeye na baadhi ya watendaji wenzake ndio waliokuwa wa kwanza kushuhudia uponyaji wa dawa hiyo baada ya mwanakikundi mmoja kilicho chini ya kamati ya halmashauri kuinywa dawa ya babu huyo na baadaye kupimwa hospitalini na kuonekana hana tena virusi vya ukimwi alivyokutwa navyo awali.
Akifafanua zaidi ushuhuda wake huo, alisema katika halmashauri yao kuna kamati inayoitwa SIMAC inayofanya kazi za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na kamati hiyo pia ina kikundi cha kuwasaidia watu wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo kwa kuwapa misaada mbalimbali.
Alisema taarifa juu ya tiba hiyo iliwafikia kupitia mwanachama mmoja wa kikundi hicho aliyekuwa amefiwa na mumewe na ambaye baada ya kupima katika hospitali za wilaya na mkoa aligundulika kuwa ameambukizwa virusi hivyo.
Alisema dada huyo alikuwa pia akitumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo (ARVs) lakini hali yake haikuwa nzuri, lakini baada ya kupewa dawa ya mchungaji huyo hatimaye alianza kujisikia vizuri na hatimaye kubaini kuwa amepona.
“Bahati nzuri huyo dada anakaa karibu kabisa na mchungaji huyo kwa hiyo aliweza kupata tiba ya Mwasapile …ni mmoja wa watu wa mwanzo kabisa kutibiwa, tunamjua vizuri.
Baada ya kutumia tiba hiyo hali yake ilibadilika na kurudi kama zamani ndipo aliporudi kwa mchungaji Mwasapile na kumuelezea kuhusu afya yake …na Mwasapile alimtaka akapime kwa mara nyingine ili kuona kama ugonjwa huo umekwisha,” alieleza.
Alisema aliporudi katika hospitali aliyofanyia kipimo mara ya kwanza madaktari walistaajabu kukuta hana virusi vya ukimwi lakini waliamini kuwa walikosea vipimo vyao na kumtaka akapime hospitali za juu zaidi.
“Alipopima katika zahanati ya Digodigo ambapo kuna huduma hiyo aligundulika hana virusi hivyo, wakaamua kumwandikia ili kupata uhakika katika hospitali teule ya Waso, ambayo ilikuwa imemuanzishia dozi ya ARVs lakini nako walipompima hawakukuta virusi hivyo,” alisema na kuongeza:
“Taarifa za dada huyo ambaye ni mwanachama wa kikundi cha halmashauri zilizagaa kila kona hata baadhi ya wanachama wengine wakalazimika kwenda kunywa dawa hiyo.”
Kwamba, hali hiyo ilisababisha wagonjwa waliokuwa wakitumia dawa za kupunguza makali ya ukimwi kupungua idadi yao, na halmashauri ikalazimika kutuma Mratibu wa Ukimwi wa wilaya upande wa afya kwenda kuonana na babu Mwasapile kumshauri asitishe dawa yake.
“Hiyo ilikuwa Juni 2010 lakini hata baada ya kurejea watu ndiyo walizidi kumiminika kwa mchungaji huyo, hivyo halmashauri ilibidi ikae na mkuu wa wilaya ili kuona namna ya kumzuia babu huyo, maana wengi walikuwa wakikatiza dozi,” alieleza.
Alisema hata hivyo hawakuweza kwani ilibidi kurudi tena kwa Mchungaji Mwasapile Juni 26, 2010 na kumuomba awasaidie kuwaambia wagonjwa hao wasiache kutumia ARV’s pindi wanapokunywa tiba hiyo ambayo mti wake kwa Kimasai unajulikana kama Lawa.
“Kama SIMAC tulikaa na mkuu wa wilaya na kumuelezea hofu yetu ya watu kukatiza tiba za ARVs tukimwomba hasimamishe huduma za mchungaji huyo lakini ilishindikana, kwani usafiri ukawa shida baada ya watu kugundua kuwa halmashauri ina mpango wa kuzuia,” alisema.
Alisema wakati huo kutoka makao makuu ya Wilaya ya Ngorongoro mpaka kufika kwa Mchungaji Mwasapile nauli ilikuwa sh elfu tano, lakini ilianza kuongezeka kadiri watu walivyokuwa wakitoa taarifa za sifa ya tiba hiyo.
Molleli alisema katika kipindi hicho tiba hiyo ilikuwa ikidaiwa kutibu kwa siku 21 lakini hadi kufikia Desemba mwaka 2010 ilidaiwa kuwa inaponya ndani ya kipindi cha siku saba pekee.
Mwingine aliyeelezwa kuwahi kuitumia tiba hiyo ambaye alikuwa alidhaniwa angefariki dunia muda wowote kutokana na maradhi ya ukimwi ni mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Babati aliyekuwa mahututi lakini baada ya kunywa dawa hiyo alipona na kuendelea na kazi.
“Ni wengi sana waliokunywa dawa hiyo na kupona… hasa wanachama wa kikundi chetu, lakini ilipofika Desemba dawa hiyo ilijulikana zaidi kwa kuponya magonjwa mengi, ikiwamo kisukari na presha (shinikizo la damu),” alisema.
Aidha, kuna taarifa pia zinazomhusu mtaalamu mmoja wa masuala ya maji katika wilaya hiyo, kwamba aliponywa ugonjwa wa kisukari na hivi sasa afya yake imeimarika huku akiwa na uwezo wa kutumia vyakula mbalimbali ambavyo mwanzoni alikatazwa kabisa kuvitumia.
Ushuhuda mwingine ulioelezwa ni wa kijana mmoja ambaye alikuwa akipewa dawa za ARVs kwa takriban miaka 18 lakini mara baada ya kutumia tiba hiyo sasa anaonekana amepona kabisa magonjwa nyemelezi yaliyokuwa yakimsumbua. (majina ya wote waliotajwa kupona kwa sasa yanahifadhiwa).
Hata hivyo, wapo mashahidi wengine waliojitokeza na kuwa tayari kuripotiwa kwa majina yao kuhusu uponyaji uliofanywa na tiba hiyo na miongoni mwao wamo maaskofu wa KKKT.
Kanisa hilo la Kilutheri limesharipotiwa likitoa msimamo wake kwamba: “Linaitambua na kubariki dawa inayotolewa na Mchungaji wake mstaafu anayefanyia shughuli zake Loliondo, Ambilikile Mwasapile”, huku baadhi ya maaskofu wa kanisa hilo wakithibitisha kwamba wamekunywa dawa hiyo na kuponywa.
Kwa nyakati tofauti, maaskofu wa kanisa hilo, Thomas Laizer wa Dayosisi ya mkoani Arusha, Dk. Martin Shao wa Dayosisi ya Kaskazini, walisema huduma inayotolewa na Mchungaji Mwasapile ni sahihi na imeanza siku nyingi na kwamba wao ni miongoni mwa watu wa mwanzoni waliowahi kunywa dawa hiyo na kupona.
Askofu Laizer alisema kwa mujibu wa imani na taratibu za KKKT, mchungaji huyo yupo sahihi na kwamba hawana mgogoro naye.
“Ifahamike kwamba kazi ya utoaji dawa haikuanza jana, ilianza siku nyingi na mimi kama askofu niliyembariki Mchungaji Mwasapile, nililetewa taarifa na wachungaji wengine pamoja na wakuu wangu wa majimbo juu ya mafunuo ya mchungaji na ndipo tulipoanza kufuatilia na kufanya mahojiano naye na kanisa likagundua kwamba tiba yake ipo sahihi,” alisema Askofu Laizer.
Askofu Laizer alisema binafsi alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na shinikizo la damu kwa muda mrefu, lakini baada ya kupewa dawa ya mchungaji huyo amepona na hajapata kunywa dawa nyingine.
“Dawa inayofanyika pale inaambatana na sala na imani, lakini watu wanashangaa.
“Mke wa Askofu mwenzangu Akyoo alikuwa hawezi kutoka, alikuwa akisumbuliwa na kisukari, lakini baada ya kupewa dawa hiyo juzi nilipompigia simu akasema amepona na yupo kwenye harusi,” alisema.
Hata hivyo gazeti hili halikufanikiwa mara moja kupata uthibitisho wa vyeti vya baadhi ya wagonjwa hasa wa ukimwi ambao wamedaiwa kupona, kwani wengi wameamua kuwa wasiri kutokana na unyeti wa ugonjwa huo.
Wakati huo huo watu watano wamefariki dunia na wengine kumi na nne kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili yaliyogongana uso kwa uso katika eneo la Kijiji cha Esilalei, Mto wa Mbu wilayani Monduli, yaliyodaiwa kuwa yalikuwa yakielekea Loliondo kwa babu huyo.
Magari hayo yalikuwa katika mwendo wa kasi kwa sababu ya kile kilichoelezwa kuwa dereva alikuwa akijaribu kuwawahisha abiria wake kwenye tiba ya babu huyo.
Katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 11:30 alfajiri ya jana katika eneo hilo madereva wa magari yote mawili yenye nambari za usajili T.606 ABU na T. 681 ABX na mtu na mkewe walifariki papo hapo.
Habari za ajali hiyo zilizothibitishwa na Ofisa Mnadhimu wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, zilieleza kuwa ajali hiyo kwa mujibu wa taarifa za awali ilisababishwa na vumbi lililotanda eneo hilo hivyo kufanya madereva wote wawili kukosa mwelekeo na kugongana.
“Ni kweli ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo na watu watano wamefariki dunia na wengine kumi na watatu wamejeruhiwa nadhani kwa taarifa za awali tunaweza kueleza kuwa zimesababishwa na mwendo wa kasi, kwani magari hayo mawili moja lilikuwa linatoka Loliondo na jingine linakwenda Loliondo kwa ‘Babu’ si unajua shauku ya kupata tiba’, alisema kamanda huyo.
Kamanda Mpwapwa aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Zakayo Laizer (36) ambaye alikuwa dereva katika gari namba T. 606 ABU na dereva mwingine ni Beatus Morris Kiboa (39), ambaye alikuwa dereva katika gari nambari T. 681 ABX. Wengine ni Raphael Kiboa (65) na mkewe aliyetajwa kwa jina la mama Kiboa (62) na Ismail Ngozi Mohamed (38).
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo na hali zao kuelezwa kuwa haziridhishi ni pamoja na Kordin Silangei (55), Elibariki Raphael (58), Asna Hassan (60), Namayani Legeri (40), Kirita Mediliyeki (65), Ngaisi Francis (38) na Sangau Magalla (90).
Majeruhi wengine ni Estomih Ole Muunyo (54), Erick Lukas aliyetajwa kuwa ni mwanafunzi, Evalyne Lukas (40), Mama Tivae (28), Anord Michael (11) na Elibariki Kiboa (49), ambao kwa mujibu wa Kamanda Mpwapwa majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Serikali wilayani Monduli.
Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi zaidi kujua chanzo cha ajali hiyo na kuwaonya madereva kuacha kuendesha gari katika mwendo wa kasi.
Tangu kuibuka kwa mchungaji huyo makundi kwa makundi ya watu wakiwamo vigogo wa serikali, viongozi wa dini na vyama vya siasa, wamekuwa wakimiminika kijijini Samunge usiku na mchana kwa ajili ya kwenda kuwahi tiba hiyo.

Source Tanzania Daima.

Mtazamo: Ushuhuda unafanyika bila ya vithibitisho??? Nawaachia wapenzi wa dawa ya babu mutupatie majibu.
 
najua wana jf wengi mnachukulia kwa mzaha tiba ya loliondo. kuna ndugu yangu alikuwa na ngoma siku nyingi alitumia tiba amepima tena ameambiwa amepona. nilikuwa siamini ila ni maajabu. soma pia gazeti la citizen leo kwa ushuhuda zaidi!
 
Hadi JF tumetekwa kirahisi, mafisadi wanatumia kila mbinu kufanya hii tiba ya babu ndiyo iwe mjadala kwa sasa ili watu wasau mjadala uliokuwa ukiendelea wa Dowans. Sasa hivi vichwa vya habari katika vyombo vyote vya habari ni kuhusu tiba ya babu. Ushindi dhahiri kwa mafisadi!
 
Usishangae ya Loliondo kwani ni Ya Musa! bali utashangaa ya Farao! ambapo iko siku atajitokeza mwingine na kudai kaoteshwa na Mungu ili awape maji Binaadamu ili uwe Tajiri!!! na amini usiamini watamiminika mamia ya watu watakaoamini dawa hiyo huku Wahariri wa Magazeti yetu ya Bongo wakishabikia hayo kwa kudai wamesikia baadhi ya hao watu waliokunywa hiyo dawa tayari wameshakuwa matajiri!!!

Hapa ndipo tulipofika Watz! sasa tunaishi kwa maono na ndoto za usiku!!!!

Watu wanakula vyakula ovyo bila mpangilio na kunywa pombe kila saa huku wakikamilisha kwa ngono hatari wataacha kuuguwa? halafu wanataka kunywa kikombe kimoja cha dawa ili wapone!! hakuna njia ya mkato, watu waache kubugia ovyo na mazoezi sana ili kuhifadhi afya zetu!

Yaani Watz tunavyopenda vya mteremko!!
 
Hadi JF tumetekwa kirahisi, mafisadi wanatumia kila mbinu kufanya hii tiba ya babu ndiyo iwe mjadala kwa sasa ili watu wasau mjadala uliokuwa ukiendelea wa Dowans. Sasa hivi vichwa vya habari katika vyombo vyote vya habari ni kuhusu tiba ya babu. Ushindi dhahiri kwa mafisadi!

Inaonyesha CCM iko katika maji marefu sana -- inatumia kila mbinu kuwatetea mafisadi.
 
najua wana jf wengi mnachukulia kwa mzaha tiba ya loliondo. kuna ndugu yangu alikuwa na ngoma siku nyingi alitumia tiba amepima tena ameambiwa amepona. nilikuwa siamini ila ni maajabu. soma pia gazeti la citizen leo kwa ushuhuda zaidi!

hii dawa siipingi lakini napinga huu ushuhuda wa kuwa kuna ndugu yangu aka jirani au rafiki.. Mimi nataka mtu aje hapa kama yeye mtibiwa/mtibwaji/aliyetibiwa aja aliyepona na wala sio kuna (.........) yangu, ushuhuda kama huu hauna mashiko hata kidogo.
 
Hii inahsusiana vipi na ufisadi na ccm? mara nyingine tusiwaonee! tuzungumzie tiba na tuzungumzie ufisadi wa ccm tofauti.
 
Mdondoaji na watu wengine mnaodadisi hii 'tiba' ya babu!
Hii sio mara ya kwanza na wala haitakuwa mara ya mwisho kwa watu wa aina hii ya babu wa Loliondo kujitokeza. Mnamo miaka ya 2003 (sina uhakika na kumbukumbu zangu) sehemu za Moshi vijijini alijitokeza mtoto aliyekuwa anatibu kama huyu babu.... kwa kutumia imani na unapewa maji aliyokuwa anayaita ya 'baraka' unakunywa. Alifanikiwa kuvuta umati mkubwa wa watu (japo si kwa kiwango cha babu) lakini japo mwanzoni kulikuwepo na shuhuda za kupona lakini kwa sasa sijui alikoishia. Mambo nililoligundua kuhusu 'watabibu' wa aina hii:
1. Hudai wametokewa na Mungu
2. Huanza kuvuta watu polepole, baada ya muda watu huongezeka sana na mwisho huanza kupungua na 'wanapoishia' hakuna anayekumbuka kuwafuatilia wao wala wagonjwa wao, jambo linatoa mwanya kwa 'waganga' wapya wanapoibuka watu wasifanye rejea ya nyuma.
3. Mara nyingi hutaka kutoa dawa wenyewe kwa mikono yao na wanywaji hunywea papo hapo.
4. Gharama zao zinakuwa ndogo sana au bure.
Mwisho nataka kusema tu hizi ni dalili za watu tuliokata tamaa na tunajaribu kutumia upenyo wowote kutatua matatizo yetu.
 
Woman who set off the rush for the ‘drink'

Sunday, 13 March 2011 09:55

By Tom Mosoba

Loliondo. Amid the ongoing stampede in Samunge village, one quiet woman goes about her daily chores, largely unnoticed.The attention is after all on the old man with a plastic cup, dishing out doses of what he has described as "God's miracle cure for the ailing nation."

But today's riveting story in Ngorongoro district about a herb that Mr Ambukile Mwasapile says cures major chronic diseases that account for a huge percentage of deaths in the country like cancer, Aids and diabetes among others, could not have happened were it not for the woman, Wilia John,30.

A mother of three surviving children, Wilia may not be known to the thousands of patients who have thronged Samunge village in recent months in search of a cure, but her story in the village is told even by small children.
The unemployed and peasant widow is after all the one whose experience would later spark off the exodus into the area.

The Citizen on Sunday caught up with her at her small grass thatched hut for a chat over her almost unbelievable tale about recovering from HIV/Aids.

Giggling about the real intention of our visit, she soon relaxes and agrees to explain how she met Pastor Mwasapile who gave her a glass of a herbal medicine that she later confessed cured her of the deadly disease.

"I have a second chance to live and God has shown mercy on his people through Pastor Mwasapile," she said, cuddling her beautiful nine months old daughter, Evelyn. Mother and child, she offered, are all free of any infection. She however, spared the details of her little girl's father hopefully for another day.

Ms Wilia's husband died over four years ago from what medical personnel at Waso health centre said was Aids.

She said the husband who worked as a watchman at a local school may have contracted the disease after briefly being transferred to another place called Malambo, where he lived alone for some time.

Life soon turned upside down for the young widow after she, and another of her young children (now deceased) would also be diagonised with the same disease. "The child died not long after the father had been buried."

Through assistance of a local campaign group, she was put on Anti retroviral drugs (ARVs) that were being delivered through the nearby Digo-Digo dispensary. "Then one day I was summoned to the pastor's house by one of my children. The pastor said he wanted to see me over my condition which he had not known from the outset," she narrated.

According to her, Mr Mwasapile said God had spoken to him in a vision that said that he uses a local shrub called ‘mugariga' to cure her of the ailment. "I drank a glass of the concoction and took off.

However I continued using the ARVs and often went for the scheduled check-ups at the Digo-Digo dispensary.
"Then came the astonishing discovery in October.

In two or three of the check-ups, the nurses detected something unusual about my blood. The viruses were diminishing!"

"The medical personnel got curious and wanted to know what I had been taking lately. However I did not remember and told them as much. They said my blood cells were coming back to normal.

Wilia said she became confused and went for further tests in Waso health centre that returned negative results."When a second test after sometime proved the same, I was incensed and thought the nurses who had taken samples soon after my husband died lied about my status."

But the woman said one Sunday during prayers, Mr Mwasapile gave testimony about the vision he had been receiving to use the shrub to treat people. "I recalled the one glass of medicine he had given me and immediately stood up to tell my story. It was the first time I was going public in church to announce my new status," said the woman.

Wilia's case, though appear plausible to many villagers and those who have thronged the old man's home for a similar treat, The Sunday Citizen could not independently verify her medical records.

She would soon after stop using the ARVs completely and subsequent tests, she claims have been negative. "It is for that reason that health personnel said I could give birth again to a healthy baby."

She said her clinic cards were taken away by the medical personnel during the time which she was accusing them of malice. But efforts to reach either spokesperson for the Digo-digo or Waso health centres were unsuccessful by the time of living Loliondo.

Disclaimer: While playing its role of informing and educating the public, The Citizen on Sunday would like to caution the public that there is no scientific evidence – according to medical authorities, including the Health and Social Welfare ministry – that supports her claim

source: the citizen on sunday:

http://www.thecitizen.co.tz/sunday-...woman-who-set-off-the-rush-for-the-drink.html

MY TAKE

1. Its high time now Goverment should make sure, a complete obejective investigation is carried out

2. A well know sample of patients with HIV/AIDS from a well known source , a governemt hospital etc, should be brought to Babu and he prescribe whatever he got and a difined management be conducted by a medical Dr ...
3. Then we want the results after some period of time..
 
mdondoaji na watu wengine mnaodadisi hii 'tiba' ya babu!
Hii sio mara ya kwanza na wala haitakuwa mara ya mwisho kwa watu wa aina hii ya babu wa loliondo kujitokeza. Mnamo miaka ya 2003 (sina uhakika na kumbukumbu zangu) sehemu za moshi vijijini alijitokeza mtoto aliyekuwa anatibu kama huyu babu.... Kwa kutumia imani na unapewa maji aliyokuwa anayaita ya 'baraka' unakunywa. Alifanikiwa kuvuta umati mkubwa wa watu (japo si kwa kiwango cha babu) lakini japo mwanzoni kulikuwepo na shuhuda za kupona lakini kwa sasa sijui alikoishia. Mambo nililoligundua kuhusu 'watabibu' wa aina hii:
1. Hudai wametokewa na mungu
2. Huanza kuvuta watu polepole, baada ya muda watu huongezeka sana na mwisho huanza kupungua na 'wanapoishia' hakuna anayekumbuka kuwafuatilia wao wala wagonjwa wao, jambo linatoa mwanya kwa 'waganga' wapya wanapoibuka watu wasifanye rejea ya nyuma.
3. Mara nyingi hutaka kutoa dawa wenyewe kwa mikono yao na wanywaji hunywea papo hapo.
4. Gharama zao zinakuwa ndogo sana au bure.
Mwisho nataka kusema tu hizi ni dalili za watu tuliokata tamaa na tunajaribu kutumia upenyo wowote kutatua matatizo yetu.

mfano mmoja(mtoto) hauwezi kujenga hoja yenye nguvu jaribu kuongeza mifano
 
Isome vizuri hii habari hasa hapo chini chini.
Jaribu kuwa great thinker hakuna jipya hapa ni porojo zile zile zisizothibitishwa.
 
Mdondoaji na watu wengine mnaodadisi hii 'tiba' ya babu!
Hii sio mara ya kwanza na wala haitakuwa mara ya mwisho kwa watu wa aina hii ya babu wa Loliondo kujitokeza. Mnamo miaka ya 2003 (sina uhakika na kumbukumbu zangu) sehemu za Moshi vijijini alijitokeza mtoto aliyekuwa anatibu kama huyu babu.... kwa kutumia imani na unapewa maji aliyokuwa anayaita ya 'baraka' unakunywa. Alifanikiwa kuvuta umati mkubwa wa watu (japo si kwa kiwango cha babu) lakini japo mwanzoni kulikuwepo na shuhuda za kupona lakini kwa sasa sijui alikoishia. Mambo nililoligundua kuhusu 'watabibu' wa aina hii:
1. Hudai wametokewa na Mungu
2. Huanza kuvuta watu polepole, baada ya muda watu huongezeka sana na mwisho huanza kupungua na 'wanapoishia' hakuna anayekumbuka kuwafuatilia wao wala wagonjwa wao, jambo linatoa mwanya kwa 'waganga' wapya wanapoibuka watu wasifanye rejea ya nyuma.
3. Mara nyingi hutaka kutoa dawa wenyewe kwa mikono yao na wanywaji hunywea papo hapo.
4. Gharama zao zinakuwa ndogo sana au bure.
Mwisho nataka kusema tu hizi ni dalili za watu tuliokata tamaa na tunajaribu kutumia upenyo wowote kutatua matatizo yetu.

Mkuu,

Asante sana na moshi vile vile kuna jamaa aliwahi kutokea miaka ya 1990s akisema anatibu dawa ya kifua kikuu hivi hivi akasema anayekunywa dawa yake aliyeoteshwa na mungu hupona. Kuna mzee mmoja amefariki mwaka jana alikunywa hiyo dawa akadai amepona akakaa muda mrefu hali ikaja kuwa mbaya zaidi miaka ya 2004 kwani inasemekana aliacha kabisa tiba alizokuwa amepewa kwa madai amepona TB. Kuja kufanyiwa X-Ray hali ilikuwa ni mbovu vibaya sana na hali yake haiwezi tena kuwa nzuri. Nakubaliana na wewe kuwa watu wakiwa desperate na matatizo hata uwezo wao wa kufikiri huwa finyu. Hilo jambo nimelisema na nitaendelea kusema kuwa jamani biashara hizi maono sijui ufunuo zilikuwapo tangu mwanzo ila kwakuwa watu hawahoji zinabakia kuwa watu wanaaminishwa pasina kuwa na tafakari yakini ya kitu gani kinaendelea.

Ndio naendelea kuuliza je huyo sijui rafiki yako, jirani yako, shoga yako au ndugu yako aliyekunywa dawa hiyo ulipitia ngazi hizi hapa kushahidia amepona?:-
a. Kwanza uliona cheti chake cha hospitali, zahanati, taasisi husika kuwa anasumbuliwa na maradhi hayo.
b. Alipotoka huko ulienda nae kupima, alienda kupima au kuna mtu alimpeleka kupima?
c. Matokeo aliyopima je uliyaona.

Mwenye shida hula hadi uchafu for the sake of kupona. Wazungu wanasema desperate times comes with desperate measures.
 
Woman who set off the rush for the ‘drink'

Sunday, 13 March 2011 09:55

By Tom Mosoba

Loliondo. Amid the ongoing stampede in Samunge village, one quiet woman goes about her daily chores, largely unnoticed.The attention is after all on the old man with a plastic cup, dishing out doses of what he has described as "God's miracle cure for the ailing nation."

But today's riveting story in Ngorongoro district about a herb that Mr Ambukile Mwasapile says cures major chronic diseases that account for a huge percentage of deaths in the country like cancer, Aids and diabetes among others, could not have happened were it not for the woman, Wilia John,30.

A mother of three surviving children, Wilia may not be known to the thousands of patients who have thronged Samunge village in recent months in search of a cure, but her story in the village is told even by small children.
The unemployed and peasant widow is after all the one whose experience would later spark off the exodus into the area.

The Citizen on Sunday caught up with her at her small grass thatched hut for a chat over her almost unbelievable tale about recovering from HIV/Aids.

Giggling about the real intention of our visit, she soon relaxes and agrees to explain how she met Pastor Mwasapile who gave her a glass of a herbal medicine that she later confessed cured her of the deadly disease.

"I have a second chance to live and God has shown mercy on his people through Pastor Mwasapile," she said, cuddling her beautiful nine months old daughter, Evelyn. Mother and child, she offered, are all free of any infection. She however, spared the details of her little girl's father hopefully for another day.

Ms Wilia's husband died over four years ago from what medical personnel at Waso health centre said was Aids.

She said the husband who worked as a watchman at a local school may have contracted the disease after briefly being transferred to another place called Malambo, where he lived alone for some time.

Life soon turned upside down for the young widow after she, and another of her young children (now deceased) would also be diagonised with the same disease. "The child died not long after the father had been buried."

Through assistance of a local campaign group, she was put on Anti retroviral drugs (ARVs) that were being delivered through the nearby Digo-Digo dispensary. "Then one day I was summoned to the pastor's house by one of my children. The pastor said he wanted to see me over my condition which he had not known from the outset," she narrated.

According to her, Mr Mwasapile said God had spoken to him in a vision that said that he uses a local shrub called ‘mugariga' to cure her of the ailment. "I drank a glass of the concoction and took off.

However I continued using the ARVs and often went for the scheduled check-ups at the Digo-Digo dispensary.
"Then came the astonishing discovery in October.

In two or three of the check-ups, the nurses detected something unusual about my blood. The viruses were diminishing!"

"The medical personnel got curious and wanted to know what I had been taking lately. However I did not remember and told them as much. They said my blood cells were coming back to normal.

Wilia said she became confused and went for further tests in Waso health centre that returned negative results."When a second test after sometime proved the same, I was incensed and thought the nurses who had taken samples soon after my husband died lied about my status."

But the woman said one Sunday during prayers, Mr Mwasapile gave testimony about the vision he had been receiving to use the shrub to treat people. "I recalled the one glass of medicine he had given me and immediately stood up to tell my story. It was the first time I was going public in church to announce my new status," said the woman.

Wilia's case, though appear plausible to many villagers and those who have thronged the old man's home for a similar treat, The Sunday Citizen could not independently verify her medical records.

She would soon after stop using the ARVs completely and subsequent tests, she claims have been negative. "It is for that reason that health personnel said I could give birth again to a healthy baby."

She said her clinic cards were taken away by the medical personnel during the time which she was accusing them of malice. But efforts to reach either spokesperson for the Digo-digo or Waso health centres were unsuccessful by the time of living Loliondo.

Disclaimer: While playing its role of informing and educating the public, The Citizen on Sunday would like to caution the public that there is no scientific evidence – according to medical authorities, including the Health and Social Welfare ministry – that supports her claim

source: the citizen on sunday:

Woman who set off the rush for the

MY TAKE

1. Its high time now Goverment should make sure, a complete obejective investigation is carried out

2. A well know sample of patients with HIV/AIDS from a well known source , a governemt hospital etc, should be brought to Babu and he prescribe whatever he got and a difined management be conducted by a medical Dr ...

3. Then we want the results after some period of time..

Mkuu this is a good advice BUT there is a catch somewhere!!!, according to Mr Mwakipelise by his words once you have no faith you wont be cured, that means by bringing the benefits of the doubts and applying investigation to few victims of HIVs after meeting Babu won't work and the results will remain positive to those affected ones, simply because they need faith to get cured. You can not just send victims there with no faith but with full of doubts to go and test Babu! it wont work!
 
[/COLOR]

Mkuu ,

You made a very sensible comments...

and I can see a real a trick there ...

Ok may be we take all the conditions requred by REV ..and then we find a couple of victims with all the conditions...That can be arranged!!

you see what we are interested ...is to have something well planed.... and objective...

and we do THE OBJECTIVE TEST ....

if he combine HERBS + GOD BLESSING WE WILL ARRANGE ALL THAT TO OUR VICTIMS ...and even control experimets..

Then we will take samples to the well known laboratory for routine check up!

What we want is to test "IT" negative or positive!!
 
Kuna kazi kubwa kuweza kuhudumia watu wote hao. Ukweli mwingine ni kuwa kuna wagonjwa wengi sana nchini mwetu na huduma zetu za afya si nzuri hata kidogo. Loliondo kumegeuka kuwa eneo la kuramaga (hija) hapa nchini na kadiri siku zinavyokwenda na ukweli wa tiba kudhihirika ni wazi kuwa sehemu hiyo iliyokuwa haifahamiki nchini mwetu itafahamika duniani. Nimezungumza na rafiki yangu ambaye alikuwa anaumwa kisukari sugu ameniambia kuwa yeye na wenzake kumi walikwenda kwa Babu Januari 12, 2011 wakati huo hapakuwepo na foleni. Hivi sasa ni mzima kama chuma cha pua. Vilevile wenzake nao wamepona. Ni vema basi wale wote waliotibiwa na Babu na kupona wakajitokeza ili wapimwe na kuthibitishwa kupona kwao ili kuondoa kiwingu cha mashaka juu ya tiba hii ya miujiza. Ni kweli Mungu huchagua viumbe dhaifu kufanya mambo yake. Mungu wetu aabudiwe na kutukuzwa. Amina
 
Ndugu Zangu,

ABRAKADABRA ni neno lisilo na maana yoyote yenye kueleweka na kuleta mantiki. Mwenye kuongea na kujifanya anafanya vitu vya miujiza na vya kimazingaombwe kimsingi anachofanya ni abrakadabra, hata kama halitamki neno hilo. Ni mambo yasiyo na uthibitisho wa kisayansi na mara nyingi wenye kutenda hudai kuwa ’ wameoteshwa’ na kumhusisha Mungu, hivyo basi, huwezi kuthibitisha kisayansi.

Na Watanzania tunaumwa kweli. Tumekuwa wagonjwa wenye kutafuta chochote kile ili tupate nafuu ya maradhi yetu. Na ’ watalaamu’ wa tiba ya maradhi yetu wanatugombania. Ndio, ni wagonjwa tunaogombaniwa. Si tumemsikia Askofu fulani wa Kanisa la kule Mwenge, tayari amemshambulia ’ Babu’ hadharani. Anatishia kumchukulia ’ wagonjwa’ wake! Askofu nae ni ’ mgonjwa’- maradhi yake ni pesa, hatosheki.

Na si tumemsikia ’ Babu’ wa Loliondo anavyojisifu na kujitangazia unabii? Anasema; “Na kama nilivyokueleza, mimi ni Mchungaji mstaafu lakini pia ni “Nabii” ambaye naweza kuona maono au ndoto na kuzungumza na Mungu mara kwa mara . Na yote ninayoyatekeleza kama unavyoona ni maagizo ya Mwenyezi Mungu.”
“Nimefanya kazi za uchungaji tangu mwaka 1967 katika sehemu kadhaa nchini hadi mwaka 1989 nilipohamishiwa katika eneo hilo. Na nimefanya kazi za uchungaji hapa hadi nilipostaafu mwaka 2002”

‘Nilianza kuota maono na kusikia sauti ya Mungu tangu mwaka 1991 ikinieleza kuwa nibaki kuishi eneo hili; kwani Mungu alikuwa anataka kunipa kazi maalumu ambayo kwa wakati huo sikuifahamu” ( RAIA MWEMA NA: 176)

Sitatafuna maneno bali kuweka bayana, kuwa hayo ya ’ Babu’ wa Loliondo ni abrakadabra. Kwa wajanja neno hili Abrakadabra ni neno la ajabu, neno la miujiza. Kwa kawaida neno hulala, lakini abrakadabra laweza kusimama katika pembe tatu.

Zama hizi, ambapo watu wengi wamekumbwa na hali ya umasikini mkubwa, ujinga na maradhi, kumeibuka manabii wa siku za mwisho. Wenye kunufaika na hofu za wajinga, masikini na wenye maradhi kwa kutumia abrakadabra. Lakini abrakadabra inatumika pia kututoa kwenye kujadili mambo yetu ya msingi.

Manabii hawa wa kujitangaza hufika mahala wakawa na nguvu kiasi cha kuwa na ushawishi mkubwa. Mwandishi Danny Sofe katika kitabu chake; "His Exellency Head Of State" (Mheshimiwa Mkuu wa Nchi) anabainisha hili kwa kumchambua mmoja wa wahusika wakuu katika kitabu hicho. Moses Akaba,

Bwana huyu, Moses Akaba alikuwa Mwalimu na msomi wa uchumi na maarifa ya Biblia. Mwanafunzi mmoja wa shule yake alianguka ghafla na kuzimia. Alipelekwa hospitalini na kudhaniwa kuwa amekufa, mara alizinduka ghafla. Akaelezea kisa chake, kwamba alijikuta akiwa kwenye handaki jembamba na lenye giza. Mwisho wa handaki hilo kulikuwa na mwanga.

Alipoukaribia mwanga alimwona mtu aliyevalia joho jeupe. Mtu huyu alimwambia kuwa Mungu alimtaka arudi tena duniani kwa vile kazi aliyotakiwa kuifanya duniani alikuwa hajaimaliza. Kwamba wazazi wake masikini walimwihitaji.

Kijana huyu aliamini kuwa mtu yule mtakatifu aliyekutana naye kwenye mpaka wa mauti na uhai alikuwa Moses Akaba, mchumi na msomi wa maarifa ya Biblia na ambaye alikuwa mwalimu katika shule ya kijana yule. Baada ya kusikia kauli ya kijana yule, Moses Akaba akajitangaza kuwa nabii, akaanzisha kanisa la Life-After -Life (Maisha Baada ya Maisha.)

Nabii Akaba alikuwa hodari sana wa kulitawala jukwaa na kuzungumza katika hadhara. Akaba alikuwa na mbinu na uwezo mkubwa wa kushawishi. Watu wengi na hasa masikini walijiunga na kanisa lake. Walichanga pesa na vito vyao vya thamani.

Na Watanzania tunazidiwa na WaNigeria tu katika dunia hii katika mambo ya abrakadabra. Na foleni za kwa ' Babu' Loliondo zitapungua mara ile Watanzania watakapoamka kuwa abrakadabra ya ' Babu' ni miyeyusho. Lakini kwa vile bado tunaumwa, basi, tunabadilisha ' hospitali'.

Naam. Hakuna lililo bora kwa mwanadamu kama kuwa na hekima. Kwa mwanadamu, kuelewa jambo hutanguliwa na kutanabahi. Ina maana ya kufikiri kwa umakini na kugundua undani wa mambo. Ni bahati mbaya, kuwa wengi wetu tu wavivu sana wa kutanabahi.

Ndio, tumekuwa ni watu wa kufuata mkumbo wa fikra, hatujipi tabu ya kutanabahi. Jambo hili laweza kuwa na madhara makubwa. Zamani sana alipata kutokea mtabiri wa nyota katika mji mmoja mdogo kule Ulaya.

Huyu alitawatabiria watu wa mji huo , kuwa katika tarehe fulani kungetokea kimbunga kikubwa. Kimbunga hicho kingeangamiza majengo na kuna watu wangepoteza uhai. Salama yao? Ndio, pindi dalili za kuanza kwa kimbunga hicho zingeonekana, basi, wakazi wa mji huo waharakishe kuelekea Kaskazini ya mji huo kuliko na milima.

Jioni moja giza lilianza kuingia katika siku iliyotabiriwa. Ikafika saa tatu za usiku bila kuonekana kwa dalili za kimbunga. Ghafla, bwana mmoja kupitia dirisha lake aliona gari likitoka kwa kasi ya kutimua vumbi kutoka nyumba ya jirani. Bwana yule aliamini kuwa kimbunga hicho sasa kimeingia kwenye mji wao na kwamba jirani yake alikuwa akikimbia na familia yake kuokoa maisha yao.

Bwana yule naye akaamrisha familia yake kuingia ndani ya gari. Naye akaondosha gari lake kwa kasi ya kutimua vumbi kuelekea Kaskazini ya mji. Mwenye nyumba nyingine baada ya kuona gari mbili zikipita kwa kasi nje ya nyumba yake, naye akaamini kimbunga kilichotabiriwa kimewadia. Akabeba familia yake na kutimua vumbi na gari lake. Kuona hivyo, wakazi wa mji huo, mmoja baada ya mwingine, wakaanza kukimbia mji wao kuelekea Kaskazini wakihofia kimbunga. Kijiji kizima kikahama!

Huko walikokimbilia wakaanza kuulizana; Ilikuwaje? Ikabainika, kuwa yule bwana wa kwanza aliyevurumisha gari lake alikuwa amegombana na mkewe, na aliamua kuondoka nyumbani kwake akiendesha gari kwa kasi akiwa na hasira, basi. Na hasira zilipomwisha akajirudia nyumbani kwa mkewe!

Tuna cha kujifunza katika kisa hicho. Si tunaona, kuwa sasa kila mmoja anamzungumzia ’ Babu’ wa Loliondo. Wengi wanafunga safari kwenda Loliondo. Hatutumii muda mwingi kujiuliza; Ya kwa ’ Babu’ Loliondo yalianzaje? Na je, kama ’ Babu’ wa Loliondo ana dawa ya kutibu kansa, kisukari na hata UKIMWI kuna uthibitisho wa Kisayansi?

Na mengine ni rahisi kuyapima hata kwa masikio kujua kama kuna ukweli. Fikiria, maelfu haya ya watu waliopata ’ Kikombe Cha Babu’, kama kungekuwa na watu mia tano tu waliopona, basi, tunashindwaje kuwapata watu ishirini miongoni mwao wa kututhibitishia kisayansi, kuwa walikuwa na maradhi hayo sugu kabla na sasa wamepimwa na hawana tena.

Ni mtazamo wangu, kuwa hii ya kwa ’ Babu’ Loliondo ni Abrakadabra nyingine. Serikali ilikuwa haina sababu ya kubabaika katika kulitolea msimamo hili la Loliondo. Msimamo wa awali ulikuwa sahihi kabisa; kusimamisha zoezi la utoaji wa tiba hiyo mpaka Serikali itakapojiridhisha juu ya dawa hiyo kupitia uchunguzi wa kisayansi.

Ndio, Serikali ilipaswa kuueleza umma, kuwa kwa sasa dawa hiyo haitambuliki kisayansi, haijafanyiwa uchunguzi, inahitaji kufanyiwa uchunguzi ili kuhakikisha, sio tu kama inatibu, bali kama ina madhara kwa mwanadamu. Hilo ni jukumu la Serikali katika kulinda usalama wa watu wake. Na huko hakutakuwa kuingilia masuala ya imani za watu.
Maggid
Dar es Salaam.
Jumatatu, Machi 14, 2011
http://mjengwa.blogspot.com
 
asante mkuu nimekupata,hanipati ng'o nitaendelea kusema na ngoma yangu
 
Back
Top Bottom