Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

oooh mara hii wameshawasili, walinitumia email juzi, ila itabidi wakae kwenye foleni kwani huduma natoa kwa kufuata utaratibu si watokako
 
tumechoka na hiz habari za babu,kwanza hii thread sio mahali pake huku,pse mod deal na hizi tread za babu

sema nimechoka... usijumuishe mioyo ya watu kwenye fikira zako unazozijua wewe ..... aliyetoa mada ana haki kuliko upupu unaoeneza
 
sema nimechoka... usijumuishe mioyo ya watu kwenye fikira zako unazozijua wewe ..... aliyetoa mada ana haki kuliko upupu unaoeneza

Kweli, mie nina hamu sana ya kuendelea kuzisikia habari za babu so usijumishe wote. Tunataka kujua ukweli wa habari hizi, watu wanaokwenda, matokeo yake n.k. Wadau endeleeni kutuletea.
 
.
Hivi yule wa Yerusalemu sii ndie huyu wa Africa eeeh?
Ukitaka kuwasiliana na huyu wa Yerusalemu inakulazimu kwenda hija huko huko au;
.

Nadhani mambo haya mkuu tuwaachie waumini wenyewe. No comment
 
mimi kwa babu hunipeleki hata kwa winchi.

manabii walikuwa wanatoka na kuwatangazia watu kila 'walipooteshwa na Mungu'. Rejea Yona 3:1---

huyu babu anasema kaoteshwa, lakini mbona hatukumsikia akitangaza?

kwa mtizamo huo, mimi namchukulia babu kama 'a new sangoma in Tanzania'.

Hivi wewe unajua maandiko au unachomekea tu chochote kinachokuja kichwani? Hii ndiyo Yona 3:1 (Jonah 3:1-2) Then the word of the Lord came to Jonah a second time: 2 "Go to the great city of Nineveh and proclaim to it the message I give you."
Ulitaka babu ahubiri habari ya hukumu au nini? Kina Musa, Elia, Elisha na wengine walioponya hawakuwa manabii? Musa aliponya kwa watu wote kuangalia nyoka wa dhahabu aliyetundikwa juu ya mti. Au hili unalionaje? Kama huna cha kusema nyamaza na mwache babu aendelee na kazi aliyotumwa.
 
Waliokunywa dawa ya babu kufariki baada ya miezi sita tu ?Eti ni kweli jamani kwamba wale wote waliokunywa dawa ya babu kama ni mafisadi watakufa ndani ya miezi sita hadi mwaka mmoja tu ?Ninauliza maana na mimi ni fisadi pia. Ili nifanye uamuzi wa kuidharau kama kipindi chake cha uhai ni kifupi hivyo !mbunge,ccm
 
Ndio hivyo hivyo Nuhu aliambiwa ajenge safina,akawambia watu kuwa kutakuwa na gharika wakabisha..matokeo yake walipoona mvua imeshika kasi ndo wakaanza ooh! Nuhu tufungulie mlango,bahati mbaya kwao ikawa too late!
Ila kama hutaki kwenda kwa babu si unyamaze uwaache wanaotaka kwenda? shida iko wapi? umelazimishwa?
 
Waliokunywa dawa ya babu kufariki baada ya miezi sita tu ?Eti ni kweli jamani kwamba wale wote waliokunywa dawa ya babu kama ni mafisadi watakufa ndani ya miezi sita hadi mwaka mmoja tu ?Ninauliza maana na mimi ni fisadi pia. Ili nifanye uamuzi wa kuidharau kama kipindi chake cha uhai ni kifupi hivyo !mbunge,ccm

Nenda kamwuulize babu
 
ataponeshwa na she*****ji yake J, asituzingue,

AKATUBU KWANZA NA ARUDISHE HELA ZETU.
 
Hakika huyu Babu siyo wa kawaida kabisa kwa sababu kuna jamaa yangu wa karibu kabisa alikwenda huko Loliondo kukomunika mrigariga yeye na mwanaye aliyekuwa akisummbuliwa na kifafa. Jamani yule mtoto amepona kabuisa kifafa. Hakika ni muujiza wa karne.
 
I have read the General's Story from the beggining to the end. What i have discovered is that most Tanzanians write things by assumptions. THE WORD RESEARCH to us Tanzanians is quite ambiguous word. This is what is also facing mr Ulimwengu. ''What testimony is he looking for if thousands and thousands of people are scrambleling for KIKOMBE every day!!! I guese he need to conduct research in order to satisfy himselves. I believe in one way or another Mr Ulimwengu has a relative or neighbour saffering from one of the deseases mentioned by people and MEDIAs that they can be cured at BABUs place. I advice him there fore to take somebody to BABus home to get the MEDICs and there after wait to see the results.
NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK OUT???

I agree with you and remind him to do his HOME WORK asitafute shortcut, Jenerali fanya uchunguzi kujidhihirisha.
 
Hivi wewe unajua maandiko au unachomekea tu chochote kinachokuja kichwani? Hii ndiyo Yona 3:1 (Jonah 3:1-2) Then the word of the Lord came to Jonah a second time: 2 "Go to the great city of Nineveh and proclaim to it the message I give you."
Ulitaka babu ahubiri habari ya hukumu au nini? Kina Musa, Elia, Elisha na wengine walioponya hawakuwa manabii? Musa aliponya kwa watu wote kuangalia nyoka wa dhahabu aliyetundikwa juu ya mti. Au hili unalionaje? Kama huna cha kusema nyamaza na mwache babu aendelee na kazi aliyotumwa.

karopoka
 
Kazi kweeeli! Mi naona hivi, ni watu wengi sana wameshaenda kwa babu na kupata kikombe. Wengi pia wamepata nafuu au kupona kabisa. Hata ktk hali ya kawaida hosp. zipo na tiba zinaendelea kutolewa, pamoja na kutumia tabibu wabobevu na dawa zilizopita katka maabara, wagonjwa wamekua wakipoteza maisha kwa kiwano kikubwa sana. Kwa hiyo kufa watu hata mia baada ya watu laki moja kupona isiwe ajabu!
Nawasilisha
 
Tafadhali tunaomba maoni na uzoefu wako kwa wagonjwa ambao tayari wamepata tiba ya Mchungaji na wamerejea mayumbani na kuendelea na maisha baada ya tiba.

Mchungaji ANAHUBIRI kufuata aina fulani ya mtindo wa maisha ili kupata na kudumisha afya baada ya kunywa dawa yake.

1. Je mafanikio ya matibabu hadi sasa yamewapa wagojwa msukumo mpya wa mabadiliko kwenye nyanja hizi hizi :

(a) ULAJI
(b) UNYWAJI
(c)MAHUSIANO

Waliokwisha pata matibabu kwa namna yeyote wamebadili mitazamo yao kuhusu namna ya ulaji ili kudumisha afya waliyokwisha ipata(diabets/HBP? etc), wamebadilisha namna na mtizamo wa uywaji wao kwani makosa kwenye ulaji na unjwaji yanaweza kuwa chimbuko la magonjwa mbalimbali. Na Je Wanamtizamo na maisha mapya kimahusino kwani hapo napo ni muhimu kuboresha afya iliyopatikana?

2. Je kwa kuwa sasa watu wamepona baada ya kutoka Loliondo ... wamejenga MAHUSIANO mapya KIFAMILIA, UJIRANI, KIIMANI, na jinsi wanavyohusiana maKAZINI?

Mchangonwako utakuwa na umuhimu mkubwa.

Kama utakuwa na mifano hai toka kwa wagonjwa ambatanisha hapa ili kutia uzito hoja yako!
 
Back
Top Bottom