Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Haya mambo ya imani ni magumu sana kwa sababu kila mtu ana tafsiri yake juu ya maandiko ndo maana kuna wengine wanapinga kwa nguvu hiyo tiba ya babu, Wengine wanadiriki hata kusema ni nabii wa uongo. Kwa hiyo inategemea inaweza kuwa kweli au si kweli nani ajuaye?

Ni kweli mkuu!! Mambo ya imani ni magumu sana, maana ni personal and intenal feelings!!! "Aaminiye na atapona" ndo ujumbe wa Bwana yesu!! Sasa hapa haiendani na scientifi proof!! Kwa hiyo tunayaacha kwa kila aaminiye maana walioamini wameponywa, na wasio amini bado wamebakia na mashaka!! Yote tunamuachia MUNGU, maana anakusudi lake.
 
Ufunuo wa Yohana sura 22:1-2 umenena hivi 'Kisha yule malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima ung'aao kama kioo na kutiririka kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo, 2kupitia katikati ya barabara kuu ya mji huo. Katika pande zote za mto huo kulikuwa na mti wa uzima utoao matunda ya aina kumi na mbili, na kuzaa matunda yake kila mwezi. Majani yake ni ya kuwaponya watu wa mataifa.

My take:
kwa imani yangu ya Kikristu nashawishika kusema kuwa huo mti ulioongelewa hapa ndiyo mchungaji Ambilikile Mwasapile anautumia katika hiyo tiba. Je wadau mwasemaje?
Mkuu! Bila shaka ndiyo yenyewe.
m
 
Nimekomaaa kabisaaaaaaa
 
Mungu alipounda dunia alikaa kutumia sayansi?

Alibadili maji kuwa wine

Watu vijijini kutwa wanakunywa miti shamba leo ndo wanataka wa babu

Muendao kwa babu nendeni na IMANI na msisahau kusali etc
 
Mungu alipounda dunia alikaa kutumia sayansi?

Alibadili maji kuwa wine

Watu vijijini kutwa wanakunywa miti shamba leo ndo wanataka wa babu

Muendao kwa babu nendeni na IMANI na msisahau kusali etc

ikifikia hapo kwenye red ndipo mjadala unaishiaga hapo.
 
Isije ikawa kwa kutumia pesa yake walihonga wakavuka foleni halafu ndio ikawa hivyo..

Na kama kwa habari zisizothibitishwa alikwenda kuhonga hadi kanisani ili wachague askofu mwingine, huenda hata huko walitafuta short cut!
 
WApendwa wana JF, Naomba kama kuna mtu aliyekuwa anasumbuliwa na saratani na akabahatika kupata tiba kwa babu Loliondo, atuthibishie kuwa kwa sasa hajambo saana. Anaweza kutupatia pia ushahidi wa kisayansi kuunga mkono ushuhuda wake. Ushahidi huo unaweza kuwa ni picha za X-rayau report ya Daktari ya kuthibitisha kuwa kweli amepona au kuna unafuu mkubwa wa ama kulimit kusambaa kwa saratani au kuimaliza kabisa. Jamani naomba hili nikijua kuwa tiba hii inafanya kazi kiimani zaidi. Hivyo tunaomba ushahidi na sisi wengine tuweze kuamini. So far sijasikia au kuona ushahidi wa kisayansi kuthibitisha uhakika wa tiba ya babu zaidi ya shuhuda za maneno tu bila evidence.
 
Kaka sijui kama utaupata huo ushahidi. hata mimi nina hamu nao. Tumeambiwa tumuangalie Mrema, Lyatonga akipona tutajua kuwa inatibu kisukari. Lkn mtu mmoja tu kati ya mamilioni yanayoenda huko Loliondo, sijui!! Tunaambiwa dawa inatibu kwa siku saba lakini babu ameanza karibia mwezi sasa na kila siku wanakunywa watu zaidi ya 3000!! Hata watu kumi wenye kansa au ngoma hawajatokea hadharani na tumepona na vyeti vyetu vya mwanzo hivi hapa na vya sasa hivi hapa na madaktari wajitokeze kusema kweli hao wamepona. Bongoland bwana kwa usanii haiwezekani!!
 
Nenda wewe na maradhi yako halafu uje utueleze umepona nini na dr wako athibitishe!
 
Nenda wewe na maradhi yako halafu uje utueleze umepona nini na dr wako athibitishe!

Hee jamani jamaa si ameomba ushahidi kabla hajaenda!! Sasa kama wewe NATA umeenda na kupona si uweke mambo hadharani ili iwe fundisho kwa watu wasio amini na wenye nia ya kuto amini!!
 
.....Lakini pia hakuna mtu aliekufa kutokana na dawa hio, hivyo kama haiponyeshi kama mnavyotaka ushahidi tukubaliena pia kuwa hio sawa sio sumu kama wizara ilivyowahi kuripoti!!!!
 
Hee jamani jamaa si ameomba ushahidi kabla hajaenda!! Sasa kama wewe NATA umeenda na kupona si uweke mambo hadharani ili iwe fundisho kwa watu wasio amini na wenye nia ya kuto amini!!

Mie bado cjaenda, wasiwsi wangu watu wengi wasingependa kutangaza aina za magonjwa yao waliyopona. Wengi nackia kisukali kisukali.
Na hao wansema wanapona sasa kuwasumbua kwa utomaso wetu eti wakamwite dr aje atudhihilishie
Mh naona inahitajio mtafiti.
Na kwa vile yeye analihitaji hilo afanye utafiti na rahisi zaidi itakuwa kwake .
Atake time afanye akanywe kikombe halfu aende kwa dr tutashukuru akituletea ushahidi wa kisansi pia
 
imani ndugu... Na dhambi kama uazo nyingi huponi
' but we jamaa tupe source or link
Na pengine ndio wale waliokuwa wanatumia umaarufu hawafati foleni maana nilimsikia babu akisema ukitumia umaarufu na kuwapita wengine waliokutangulia huponi inabidi kila mtu aende kwa foleni.
 
Wakati watanzania wakimiminika kwenda wilayani Loliondo,kwa Babu kupata dawa inayodaiwa kutibu magonjwa sugu, Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz ameibuka na kusema tiba hiyo haina lolote akidai kwamba ndugu zake watano wameitumia lakini hajapona hata mmoja.

... "Ndugu zangu wananchi wa Igunga, mimi mjomba wangu Hassan mnamfahamu karibu wote hapa mjini ni mgonjwa wa siku nyingi wa kisukari. Ameshakunywa dawa hiyo lakini mpaka sasa ni mgonjwa kama mnavyomuona sasa hiyo dawa inaponyesha nani?"

Mbona haongelei ya swaiba wake .... ..... .... .. Oops mwizi mwenza wa pale Magogoni siku zako zinahesabiki we ngoja tu!
 
hahaha, acheni jamani, hivi ni kweli alienda au wanamsingizia tu?|
 
Nenda wewe na maradhi yako halafu uje utueleze umepona nini na dr wako athibitishe!

Laiti ningelikuwa naumwa, ningelifanya hivyo. Wajua sijui kwanini watu hawajitokezi kutoa ushahidi kwa wale waliopona kweli. Mimi nauliza kwa sababu nina jamaa zangu wawili, mmoja anasumbuliwa na Kansa ya ziwa na mwingine anasumbuliwa na Kisukari. Wote wawili wameshatumia dawa ya babu na leo ni wiki ya pili toka warejee. Kusema ukweli toka wamerejea sijaona unafuu wowote na leo ni siku ya 14. Kama huyu wa kansa hata kupata usingizi kwake ni taabu. Ndio maana nauliza kama kweli kuna watu waliopona, ili nami na wagonjwa wangu tuishi kwa matumaini kuwa huenda iko siku nasi watapona.
 
Back
Top Bottom