StaffordKibona
JF-Expert Member
- Apr 21, 2008
- 669
- 60
asante kwa ushuhuda pole sana mkuu, mimi nitakuwa wa mkristu wa mwisho tz kumwamini huyu babu.
so do i
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
asante kwa ushuhuda pole sana mkuu, mimi nitakuwa wa mkristu wa mwisho tz kumwamini huyu babu.
Kwa wanajamii wote, naomba kutoa ushuhuda kuwa nilimpeleka mgonjwa wangu mke wa rafiki yangu mpenzi kwa Babu wiki mbili zilizopita ili kupata dawa kutokana na maradhi ya Breast cancer ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Kama sote tunavyojua hakuna dawa ya kutibu kansa, lakini baada ya kusikia habari za Babu tulijenga imani kuwa huenda akapona. Tulimpeleka huko, na baada ya kukaa siku mbili kwenye foleni alibahatika kupata dawa na kuinywa. Lakini toka anywe hiyo dawa hali yake imekuwa sio nzuri na kudhoofu siku hadi siku hadi hii leo saa nne asubuhi amefariki dunia. Ninatoa ushuhuda huu si kwa kuwakatisha tamaa watu la hasha bali ni kutaka kuweka vitu hadharani ili watu wajue kuwa pamoja na kuwa huenda dawa hiyo ikawatibu baadhi ya watu lakini watu tujue pia hakuna dawa ya kuponya kifo. Huenda kweli babu anatibu kwa imani, lakini sidhani kama wale wote wanaoenda huko hawana imani. Namalizia kwa kuzidi kuwaomba waliotibiwa na kupona kweli wajitokeze watuthibitishie kwa ushahidi wa kitabibu.
Hakuna mfuasi wa babu kwani babu si imani wala itikadi. Yeye anakupa kikombe unakunywa na kuondoka; hakuna anapokuhubiri eti uingie kweye imani yake ya lilutheri.
Babu anasema yeye si mganga, bali kinachotibu ni neno la Mungu ambalo Mungu mwenyewe ameliweka kwenye huo mti; yeye ni wakala tu wa kukunganisha na hilo neno. Na ameelekezwa kuwa dawa ataitolea hapo na itanywewa hapo. (hii inaondoa uchaachuaji pia)
Kuhusu masharti, naona hiyo imeshaelezwa vizuri zaidi - hata Yesu aliponya kwa masharti.
Wakatoliki wanaukiritimba wa kutambua matukio kama haya na mwisho wake ni kushindwa kutumia kwa manufaa matukio ya namna hii. Kama mtakumbuka kabla ya mauaji ya Rwanda, kuna mtu alitokewana Bikira Maria na akaelezwa kuwa naona damu nyingi inamwagika hapa, Bikira Maria akamweleza kuwa watu wamrudie Mungu nk. Lakini kanisa katoliki lilichelewa sana kuutambua muujiza huo na kuufanyia kazi hadi mauaji ya kimbari ya Rwanda yalipotokea na watu wengi kuuawa ndani ya kanisa alimotokea Bikira Maria; ndipo kanisa liliposhtuka - oo kumbe huo ndio ujumbe aliokuwa ameuleta Bukira Maria! Ujumbe ulisema watu wamrudie Mungu, kama kanisa lingetambua mapema na kuwahubiri sana watu kuwa Bikira Maria ametokea mahali hapa na kuleta ujumbe kuwa tumrudie Mungu; watu wasingeuana kwa kiasi hicho!
Nashauri watu wenye magonjwa sugu wakanywe kikombe kwa babu maana hatujui kikombe kitakuwepo hadi lini.
Suala la tiba kuwa ya muda mfupi - hata Yesu alihubiri kwa miaka 3 tu!
anachosema ni kuwa dawa ya babu ime speed up kifo cha shemejie. Kufa kila mtu atakufa hakuna mjadala hapo. si vibaya tukahabarishana na yatokanayo na dawa ya loliondo. kuna mazuri na machungu. Kwa hiyo wale ambao hawajaenda waweza kutafakari zaidi.
Pole sana siku yake ilifika tu, mimi bosi wangu ameenda na sasa yuko fiti sana ameanza hadi kula vyakula alivyokataliwa na doc
Kwa wanajamii wote, naomba kutoa ushuhuda kuwa nilimpeleka mgonjwa wangu mke wa rafiki yangu mpenzi kwa Babu wiki mbili zilizopita ili kupata dawa kutokana na maradhi ya Breast cancer ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Kama sote tunavyojua hakuna dawa ya kutibu kansa, lakini baada ya kusikia habari za Babu tulijenga imani kuwa huenda akapona. Tulimpeleka huko, na baada ya kukaa siku mbili kwenye foleni alibahatika kupata dawa na kuinywa. Lakini toka anywe hiyo dawa hali yake imekuwa sio nzuri na kudhoofu siku hadi siku hadi hii leo saa nne asubuhi amefariki dunia. Ninatoa ushuhuda huu si kwa kuwakatisha tamaa watu la hasha bali ni kutaka kuweka vitu hadharani ili watu wajue kuwa pamoja na kuwa huenda dawa hiyo ikawatibu baadhi ya watu lakini watu tujue pia hakuna dawa ya kuponya kifo. Huenda kweli babu anatibu kwa imani, lakini sidhani kama wale wote wanaoenda huko hawana imani. Namalizia kwa kuzidi kuwaomba waliotibiwa na kupona kweli wajitokeze watuthibitishie kwa ushahidi wa kitabibu.
POLE KWA KUMPOTEZA MPENDWA WAKO! LAKINI PIA WANGAPI WANAFIA MAHOSPITALINI? BABU ANATIBU "MAGONJWA" SIYO "KIFO" LAZIMA TUJIFUNZE KUTOFAUTISHA HIVO VITU VIWILI MAAKE IMEANDIKWA"BINADAMU LAZIMA ATARUDI MAVUMBINI ALIKOTOKA" SO MUDA WA KUFA UKIFIKA UTAKUFA TU HATA KAMA UMEWEKEWA MASHINE ZA OKSIJENI, KUBADILISHIWA FIGO etc! ENYI WATANZANIA NENDENI MKANYWE DAWA!:hatari:
Bikira Maria? Who is she? Au ndo yule tunaambiwagwa malkia wa mbingu? Yeremia 7:18.
Sorry, just being curious!
:lol::lol::lol: