Nundu_Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 811
- 349
Ye yote anayetafakari kwa kina, aliye na elimu ya vitu na uelewa wa mambo hawezi kuzingatia akilini mwake kwamba mtu wa kwanza alikuwa na rangi gani; au alianza kuishi eneo au bara gani.
Rangi ya mtu; vyovyote inavyoitwa: mweusi au mweupe, si kitu chenye nafasi katika maana yenyewe ya mtu. Vivyo hivyo eneo aliloanza kuishi. Kwasababu rangi sio mtu wala mtu sio rangi; na wala eneo sio utambulisho wa mtu.
Sayansi imejaribu kueleza mambo hayo mawili: tofauti za kirangi katika watu na katika jambo la eneo, alipoanza kuishi mtu wa kwanza, sayansi haijafanikiwa kufahamu hilo, lakini imefanikiwa kuonyesha kuwa mtu amekuwepo dunia kwa muda mrefu.
Kitu muhimu hapa duniani ni mwili na sio rangi wala eneo la kuishi. Mwili ndio muhimu kwa maisha ya hapa duniani. Umuhimu wa mwili sio kwa jinsi unavyoonekana, hilo sio muhimu hata kidogo. Umuhimu wa mwili ni jinsi unavyotunzwa na kulindwa. Umuhimu huu unatokana na sababu kwamba kwenye mwili kuna Ubongo na katika ubongo ndipo zinapofanyika kazi za kiakili.
Mwili ni muhimu kwasababu akili peke yake bila mwili inapungukiwa. Yaani kwamba, ili mtu ufanye kazi za kiakili na kimaendeleo anahitaji mwili wala sio rangi ya mwili.
Rangi ya mwili kwa yenyewe haimfanyi mtu awe bora. Kinachomfanya mtu awe bora ni jinsi alivyoutunza na kuulinda mwili wake hata ukaunganika na roho yake.
Eneo kwa lenyewe halikufanyi au halimfanyi mtu uwe bora ila matumizi mazuri ya mwili ambayo humfanya mtu uungane na Mungu wako na hivyo kufanyika kwa kazi za kiakili.
Hakuna mtu anayejua kwa hakika dunia ilianza lini na mtu wa kwanza aliishi wapi au aliitwa nani. Nadharia ya Mageuzo Yenye Maendeleo (Evolution theory) inaweza kutusaidia kujifunza katika kuelewa mambo haya.
Tunakuwa watu wajinga na wapumbavu kwa sababu tunaacha watu wengine wafikiri kwa ajili yetu. Ina maana gani mtu wa kwanza kuwa mweusi lakini si bora?
Watu makini hawajadili au hawajivunii rangi au eneo la mtu, bali mtu alifanya nini alipokuwa duniani.
Wayahudi wanakuwa mfano bora kwenye Maandiko Matakatifu sio kwa sababu ya rangi na eneo lao, lakini kwa sababu ndiyo jamii pekee iliyokuwa na Ufahamu wa Kina wa Mambo na Elimu ya Vitu, Imani Kwa Mungu Mmoja.
Sio kweli kwamba wakati wa Wayahudi hakukuwa na jamii nyingine, zilikiwepo lakini zilikiwa jamii za miungu- hazikuwa na ufahamu wa kina wa mambo na elimu ya vitu.
Tusiache watu wengine wafikiri na kuamua kwa ajili yetu, tutumie ubongo wetu. Mambo yote yako wazi ukitumia vizuri ubongo wako.