Habarini wana Jf, kiuhalisia mimi ni miongoni mwa watu wanaokataa Ndoa kwa sababu maalum kabisa na wala sifati mkumbo na nimeanza kuchukia maisha ya ndoa tangu nilivyojitambua tu na kuanza kujua huyu ni Mama na huyu ni Baba basi ndo hapo hapo nilipoanza kuichukia Ndoa, Leo nitaleta kisa changu kifupi,
Baba yangu alikuwa mwanajeshi lakini tangu mimi nilivyojitambua katika umri mdogo nilikuwa nikishuhudia Mama yangu akipigwa vipigo kila siku tena kwa sababu zisizo na maana kabisa na uzuri ni kwamba mara nyingi Baba alipoanza kumpiga mama alianza kumpiga huku mimi nikiwa najua kabsa sababu ya ugomvi huo na hizi ni baadhi tu ya sababu,
Kuna siku mama alimuuliza Baba una siku mbili hujalala nyumbani na hukuniambia upo wapi kwanini ulifanya hivyo ? Baba alikuja juu na kusema asipangiwe maisha....Mama akaendelea kusema sio sawa anachofanya hapo sasa ghafla tu nkaona kwa macho yangu Baba amemrukia mama na akaanza kumpiga vichwa na ngumi za kutosha nilikuwa mdogo sana kiumri na hata umbo niliishia kulia tu nisijue cha kufanya,
Huku nikilia na kujutahidi kumtoa Baba asimpige Mama basi Baba alichofanya ni alinitoa nje kwa nguvu na akafunga mlango huku akimpiga mama na mikanda ya jeshi ile yenye chuma mbele, alimpiga sana mpaka kesho yake mama anaamka alikuwa amevimba na amevuja damu, kiukweli kile kitendo cha kushuhudia mama akipigwa huku mimi nikishindwa kumsaidia kiliniathiri kisaikolojia mpaka leo hii nitatolea mfano huko mbele,
Kisa kingne ni siku moja mdada fulani wa pale mtaani alikuja kwetu na kuanza kulalamika kwamba Baba anamtongoza na wakati yeye ni mke wa mtu na ameshamwambia mara kadhaa, mdada huyo wakati analalamika kwa nguvu pale sebuleni kwetu mimi nilikuwa nasikia kabisa na mama akamuahidi ataongea na Baba na kuyamaliza,
Jioni ikafika Baba akaludi na ikafika usiku nikiwa nimelala niliamshwa na kelele za vilio kutoka kwa mama kwenda nilimkuta Baba amempiga vibaya sana Mama mpaka hata kunyanyuka hawezi, asubuhi nikamuuliza mama shida nini mpaka Baba amekupiga hivyo lakini alisema hakuna kitu ila kiufupi nilijua vizuri tu kuhusu sababu ya kupigwa kwake kwamba ilikuwa ni kumuuliza kuhusu huyo mwanamke aliyekuja kulalamika,
Kuna visa vingi sana vya kupigwa nitawachosha ila kisa cha mwisho kilichofanya hadi Mama na Baba wakaachana ni hiki,....
Siku moja kipindi tumetoka mjini na Mama wakati huo nipo darasa la nne nakumbuka mimi ndo nikawa wa kwanza kufungua mlango kuingia ndani, lakini ghafla niliona barua ipo chini na nikaiokota na kuifungua ila cha ajabu ???!!
ITAENDELEA