Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Ni UKWELI MTUPU! Juzi mwanamke wangu amenikimbia. NDOA NI UTAPELI! UTAPELI! SITAKI KUSIKIA TENA MAMBO YA NDOA. IT IS VERY VERY DANGEROUS. MARRIAGE IS EVIL! NI UPUUZI MTUPU. Ndoa za kweli zilikuwa zamani. Siku hizi ni utapeli tu!
Bora umeamua kuwa mkweli mwanetu. Najua wengi watashupaza mafuvu na kubisha lakini wanaelewa ukweli. Pole sana mkuu
 
Mwanamke anaweza kumpenda sana mwanaume fulani, lakini kama mwanaume huyo hayupo tayari au anasuasua kumuoa ataolewa na mwanaume aliye tayari kumuoa.

Wazungu wanasema women marry the available men. When it comes to women, they settle for who's ready not who they love.

Huyo mwanamke uliyemuoa sio kwamba anakupenda ni wewe tu ulikuwa na kimbelembele cha kumuoa ulikuwa available man.

Love and marriage is two big gap when it comes to women

Mwanamke kuwa tayari kuolewa nawe sio kwamba anakupenda ni utapeli tu.

Yule mwanaume aliyempenda lakini hakuolewa naye atakuchapia sana mkeo.
Imeandikwa, mwanamke huwa hapendi anapendwa. Upendo wa kweli wa mwanamke hujengwa taratibu. Cc Leejay49
 
Habarini wana Jf, kiuhalisia mimi ni miongoni mwa watu wanaokataa Ndoa kwa sababu maalum kabisa na wala sifati mkumbo na nimeanza kuchukia maisha ya ndoa tangu nilivyojitambua tu na kuanza kujua huyu ni Mama na huyu ni Baba basi ndo hapo hapo nilipoanza kuichukia Ndoa, Leo nitaleta kisa changu kifupi,

Baba yangu alikuwa mwanajeshi lakini tangu mimi nilivyojitambua katika umri mdogo nilikuwa nikishuhudia Mama yangu akipigwa vipigo kila siku tena kwa sababu zisizo na maana kabisa na uzuri ni kwamba mara nyingi Baba alipoanza kumpiga mama alianza kumpiga huku mimi nikiwa najua kabsa sababu ya ugomvi huo na hizi ni baadhi tu ya sababu,

Kuna siku mama alimuuliza Baba una siku mbili hujalala nyumbani na hukuniambia upo wapi kwanini ulifanya hivyo ? Baba alikuja juu na kusema asipangiwe maisha....Mama akaendelea kusema sio sawa anachofanya hapo sasa ghafla tu nkaona kwa macho yangu Baba amemrukia mama na akaanza kumpiga vichwa na ngumi za kutosha nilikuwa mdogo sana kiumri na hata umbo niliishia kulia tu nisijue cha kufanya,

Huku nikilia na kujutahidi kumtoa Baba asimpige Mama basi Baba alichofanya ni alinitoa nje kwa nguvu na akafunga mlango huku akimpiga mama na mikanda ya jeshi ile yenye chuma mbele, alimpiga sana mpaka kesho yake mama anaamka alikuwa amevimba na amevuja damu, kiukweli kile kitendo cha kushuhudia mama akipigwa huku mimi nikishindwa kumsaidia kiliniathiri kisaikolojia mpaka leo hii nitatolea mfano huko mbele,

Kisa kingne ni siku moja mdada fulani wa pale mtaani alikuja kwetu na kuanza kulalamika kwamba Baba anamtongoza na wakati yeye ni mke wa mtu na ameshamwambia mara kadhaa, mdada huyo wakati analalamika kwa nguvu pale sebuleni kwetu mimi nilikuwa nasikia kabisa na mama akamuahidi ataongea na Baba na kuyamaliza,

Jioni ikafika Baba akaludi na ikafika usiku nikiwa nimelala niliamshwa na kelele za vilio kutoka kwa mama kwenda nilimkuta Baba amempiga vibaya sana Mama mpaka hata kunyanyuka hawezi, asubuhi nikamuuliza mama shida nini mpaka Baba amekupiga hivyo lakini alisema hakuna kitu ila kiufupi nilijua vizuri tu kuhusu sababu ya kupigwa kwake kwamba ilikuwa ni kumuuliza kuhusu huyo mwanamke aliyekuja kulalamika,

Kuna visa vingi sana vya kupigwa nitawachosha ila kisa cha mwisho kilichofanya hadi Mama na Baba wakaachana ni hiki,....

Siku moja kipindi tumetoka mjini na Mama wakati huo nipo darasa la nne nakumbuka mimi ndo nikawa wa kwanza kufungua mlango kuingia ndani, lakini ghafla niliona barua ipo chini na nikaiokota na kuifungua ila cha ajabu ???!!

ITAENDELEA
 
Hiyo barua ilikuwa na picha ya mtoto kwa pembeni nikaanza kuisoma na kugundua kwamba yule kwenye picha ni mtoto wa Baba wa nje ya ndoa na ile barua ilijaa malalamiko kutoka kwa huyo mwanamke aliyezaa nae ya kwamba mwanzo Baba alikuwa anamjali sana huyo mtoto lakini sasaivi amekuwa hamjali na imetokana na mwanamke mwingine aliyempata,

Kiufupi ni kwamba huyo Mwanamke(mchepuko namba 1) aliyezaa na Baba alivyoona kwamba matunzo kwa mtoto wake yamepungua basi akabaini kwamba baba amepata mchepuko mwingne tena Namba 2, hivyo akaona tu amwage mboga na afumue siri kwa Mama ili aharaibu tu liwalo na liwe,

Kiufupi baada ya kusoma ile barua nikajifanya kama sijaisoma na nikampa mama basi na yeye baada ya kuisoma nikaona tu ameanza kutokwa machozi na akaenda chumbani kujifungia, muda kidogo na Baba akaludi ....

Mama siku hiyo alipanick sana na akampa ile barua na akamlalamikia kwamba yani unanifanya nadharaulika mpaka watu wanakuja hapa kunivunjia heshima, basi baba akaja juu kwamba yeye ni Mwanaume na asipangiwe Maisha,

Ukazuka ugomvi pale mara ghafla Baba akamvaa tena Mama na akaanza kumpiga na mama alikuwa ametoka kujifungua miezi 2 iliyopita na safari hii alimtengua Mkono mbele yangu... kidogo tu auvunje kama Muwa, aisee ile siku nilipatwa na hasira nikatafuta kisu nikamchome baba ila nikakosa nikiwa naendelea kukitafuta ghafla akaumachia na akaondoka zake (nafikiri Mungu tu alimuepusha ile siku nilitaka nimtoe roho maana nilichoshwa na manyanyaso anayopitia mama),

INAENDELEA
 
Basi baada ya Baba kuondoka nilimwambia mama leo ndo siku ya mwisho kukushuhudia unalia sitokubali tena, nikachukua simu nikampigia Babu yangu nikamwambia Baba kampiga sana mama naomba mje tumchukue tumpeleke hospitali, basi bibi na uncle na Babu wakafika ila walivyokuja tu na Baba akawa ameludi akaanza kuzuia mama asipelekwe popote Ukazuka ugomvi mkubwa pale ghafla tena Baba ndo akaharibu kabsa akamtukana bibi yetu (Kum*** la ma**k),

Aisee hapa ndo nikajua sasa kweli huyu mzee ni hakuna kitu kabisa kichwani yani badala ya kuketi chini aombe hata msamaha yeye anatukana wakwe tena?,... basi akataka hadi kumpiga bibi ila wakina uncle wakamzuia na wakamchukua mama tukaondoka tukapitia Polisi wakachukua PF3 (kama nimekosea mnirekebishe, nasikiaga watu wakiita hivyo),

Kuanzia hapo tukahamia nyumbani kwa Babu, na Baba akaanza kuja kuomba misamaha pale lakini safari hii walimkatalia kabisa maana sio mara ya kwanza kwenda kwa babu na bibi kuomba misamaha kwa makosa yale yale ya kumpiga mama na Kuwatukana,

INAENDELEA
 
INAENDELEA

Kuanzia hapo ndo ukawa mwanzo wa kuishi kwa Babu na bibi na mama akadai talaka yake ila baba akawa hataki kutoa talaka akidai ya kwamba atatoa talaka endapo Mama atakubali kumuachia watoto( mimi, mdogo wangu na Kaka yangu tuishi nae),

Mama akamkatalia hilo ombi lake na mama akaenda mahakamani kudai talaka na akasema kabisa mi sitaki mali zake wala gari ambalo nimemuachia nachotaka ni talaka tu na nibaki na watoto wangu, basi Baba akaridhia kutoa talaka ila mahakama ikaamuru Watoto tuendelee kuishi na Mama ila kuwaona ataruhusiwa kutuona, baada ya hiyo hukumu kutoka Baba alimpigia simu Mama na kumwambia hatotutunza tena na kweli alifanya hivyo tuliishi maisha ya tabu sana siwezi kuelezea,

Tulisoma shule za kata huku yule mtoto wa nje ya ndoa akisomeshwa Shule za kulipia, kiufupi saivi nimekuwa mkubwa ila changamoto nayopata ni kwamba kila mahusiano nayoingia najikuta nakuwa mkali sana hata kwa vitu vidogo tu kitu cha pili ni mbinafsi sana yani changu ni changu na cha mwisho na kibaya zaidi ni kwamba sijali hisia za mtu yoyote anayehitaji msaada wangu,

Yani naweza kuona kabsa mtu anauhitaji na pesa na mimi nina uwezo wa kumpatia hiyo hela basi sitompa na hata akinisihi kwa kiwango gani yani sitompa na mimi huona kawaida kabisa ila mbeleni tu ndo nikikumbuka naanza kujutia kwa kumnyima msaada,
 
MWISHO,

Kuna siku nilikaa nikafikiria hii imesababishwa na nini nikapata jibu kwamba usikute kipindi kile mama yangu alipokuwa anapigwa mbele yangu na mimi nisiweze kumsaidia basi ile kitu iliniathiri sana kiakili maana Mama yangu alikuwa akiteswa mbele yangu na cha kufanya sikuwa nacho,

Ile kitu ndo ilifanya mpaka hisia ndani mwangu zimekufa kabisa maana naona kama nilishindwa kumsaidia mama yangu kipindi anateseka wewe ni nani mpaka nikusaidie, kiukweli akili yangu imeharibika mno mambo ni mengi sana ningeandika kuhusu Maisha ya Wazazi wangu ila nitawachosha tu,

Nahitimisha kwa kusema siwezi kuingia kwenye Ndoa na mwanamke yoyote maana nahisi nitamtesa tu kwa hizi tabia zangu na pia sijawahi hata kutamani kuwa na familia kitu pekee nachopenda ni kuwa na mtoto tu na hivi karibuni natarajia kumpata.

Nisameheni kwa uandishi kama ni mbaya maana mimi sio Mtunzi wa Vitabu. Leta na wewe kisa chako cha kwanini unakataa Ndoa ?

MWISHO.
 
Marriage is the triumph of imagination over intelligence. ...kama hujafikiria ndoa, hujawahi kupenda
so usiwaze sana boss,

Mimi kabla ya kupenda nilikua kataa ndoa Promax,but kwa nilie nae Sasa,siku yeyote mtakula pilau,

and if get married,I want to be very married...
 
Back
Top Bottom