Babu yangu alioa wanawake Saba,na kila mmoja akazaa nae watoto kumi na mbili,na kila mmoja alijengewa nyumba na kupewa shsmba la ekari mbili.
Mengi uliyoyataja ni mahitaji ya kawaida ya mwanamke.
Je Kuna wanawake wabaya,gold diggers,yees wapo wengi!!!je Kuna ndoa zinazoumiza wanaume,zipo kibao,
Je Kuna ndoa na wanawake wazuri,?wapo weeengi tu.
Lakini Cha msingi tangu Dunia iumbwe,hakuna ndoa isiyo na matatizo!!!
Kuna ubaya gani binti,kutaka kuolewa na mtu mwenye uwezo au na mwelekeo wa kipato!?sasa unataka aolewe na kapuku,harafu uzao wake nao uishi kwa shida!umetoka familia maskini,umesoma kwa shida,uolewe Tena na kapuku harafu wanao Tena waishi maisha magumu!!!
Kijana Bado hujakomaaa,kama unatsfuta mwanamke wa kukupenda kwa mspenzi ya muvi za kifilipino na kihindi,usioe kabisa.
Ndoa ni maisha halisi sio maagizo,unaishi na binadamu sio maraika.