Narudia tena ndoa ni utumwa mkubwa saaana, broo tafuteni tu watoto Lakini tusioe kabisa.
Jamaa yangu mmoja kafunga ndoa mwaka Juzi tena kwa mbwembwe nyingii saaana, Lakini jana kakuta sms kutoka kwa mke wake "akichat" na Mwanaume mwingine (hawakufanya mapenzi Lakini walikua wanapangana wakadinyane), kambana mke wake kasema huyo jamaa ni classmate wake huko mikoani so wamekutana mkoa Mwingine baada ya miaka mingi ndio wakapeana namba.
Msela yupo na stress nyingii mno, kamwambia mke wake aondoke arudi kwao mwanamke amegoma hataki kuondoka jamaa anawaza afanyaje? Maana Kila akimuona mwanamke wake anawaza kufanya kitu kibaya mno, na jinsi wanawake walivyo kagoma kabisa kuondoka kamwambia "wewe kama unanipiga wewe nipige Lakini siondoki" mshikaji ananiambia anataka aondoke Kabisa apotee aende mkoa Mwingine akaanze maisha. kwa sababu sijaoa nikakosa Cha kumshauri kabisa, Lakini alichonisaidia ni Mimi kuongeza miaka mbele ya kuvuta tu mwanamke kumweka ndani (sio kuoa).....
Waliooa Wana stress nyingii mno. Just imagine unakutana na mwanamke kalelewa katika mazingira yao na wewe umelelewa katika mazingira yenu, ukitaka kumbadilisha tabia Hapo ndani lazima moto uwake.
Kijana USIOE ukioa utakutana na vingi vya ajabu, ukikutana na mwanamke anapenda kuchat USIOE, ukikuta mwanamke anao marafiki wa kiume USIOE (broo hakunaga urafiki wa Mwanaume na mwanamke ataliwa tu), ukikutana na mwanamke anaejifanya charming saana anazoeleka na wanaume kihurahisi USIOE , Ukiwa na Mwanamke anapenda kuvaa nguo za kubana saaana kwa ajili ya ku_impress mtu USIOE. SASA WEWE JIFANYE MKAIDI.
NDOA ni utapeli tu, unamleta mwanamke ndani kula Hela yako na Bado akufanyie kiburi, just imagine ujaoa na unaingiza kipato Cha 800k na kuendelea, hayo maraha yake yakoje mzee? Yaani kazi yako ni kwenda vacation, kula maisha kufanya unalolitaka bila kuulizwa na mtu Wala stress na kitu furaha iliyoje? Ukipata likizo nenda sehemu ambayo hujawahi kufika furahia maisha.
Ukioa utaweza kufanya hayo?...kwanza ndani ya miezi 6 tu ya ndoa utapigwa wimbi la stress mpaka unyonyoke kama kuku😀😀
MWISHO!
WANAWAKE WAZURI BADO WAPO NA WENYE HESHIMA RUDI KWA WAZEE WAKUTAFUTIE MKE KIJIJINI KWENU.