Maisha ya ndoa hayafanani kama ambavyo maisha ya kawaida hayafanani.
Nimeoa 2016,katika maisha yangu sijawahi kujutia kuoa,Mungu alipa zawadi siyo tu mke yaani ni zawadi kabisa.
Mke wangu hana mambo mengi,siyo kwamba ni kwa sababu ni wa kawaida hapana ni pisi kali sana tu umbo maridhawa na sauti isiyochosha.
Mke wangu hajui kusema neno hapana kwake ni ndiyo na kuomba ruhusa kwa kila anachokifanya,kwake ni kutoa ushauri na kusubiri mume nitekeleze.
Mungu alinipa zawadi,mke wangu hataki kabisa kusikia jambo lolote la kusimuliwa kuhusu mume wake,yeye msimamo wake ni mmoja tu,anaangalia vile mume wake anavyoishi naye kwa amani na upendo,namna mume anavyotimiza majukumu yake.
Nimeshamfungulia kabiashara ili na yeye awe na cha kufanya,hatumii hata mia bila kupata kibali.
Aisee hata ndoa zote ulimwenguni zivunjwe ili tuoane upya nitaenda kumchumbia upya mke wangu.
Pamoja na changamoto zote za ndoa bado ndoa zenye amani na upendo zipo kabisa.