Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Hawo wote wasiotaka ndoa Kuna walioaminishwa ni mbaya, waliotendewa na wanawake wasiotulia,wengine ni Malaya, wengine ni mashoga, wengine ni wanaona hela zikatumike ni haiwezekani
Kuna tofauti ya kuishi na mwanamke na kufunga ndoa apa tunachokataa ni ndoa ya mavyeti na kusaini kisheria.
 
Mambo yame badilika sana sasa, ukiishi kizamani lazima mambo yakushinde. Kutokana na uzamani kwa sasa umepungua kwa kiwango kikubwa sana.

Na wanaoishi kizamani kwenye Ndoa ndio wanafanikiwa,
Ila Sisi tunataka kuleta usasa kwenye Ndoa ambayo ni mfumo wa kizamani zinatushinda.

Ndoa ni nzuri ikitumia mfumo wa kizamani lakini ni jehanamu ukileta usasa
 
Mimi nadhani labda wanataka waolewe wao!!!

Eeh,maana kama mtu ulitokana na ndoa na umekulia kwenye familia ukiwaona wazazi wako pamoja mpaka wamezeeka kinachokufanya usiowe ni nini?
Bado hujaelewa mantinki ya Taikon ...usijibu kimhemko
 
Na wanaoishi kizamani kwenye Ndoa ndio wanafanikiwa,
Ila Sisi tunataka kuleta usasa kwenye Ndoa ambayo ni mfumo wa kizamani zinatushinda.

Ndoa ni nzuri ikitumia mfumo wa kizamani lakini ni jehanamu ukileta usasa
Kweli
 
Tatizo mnaopoa ma slay queens, wasomi sana, modern women n.k..[emoji1]...hamna sehemu rahisi kuoa kama bongo...Mimi nimejikita kwenye kuoa 'mama ntiliez'..raha sana, usiwe na wivu sana...unaweza ukajikuta kila mkoa una mke..hamna cha mkataba, pete za ndoa, sherehe, kwaito...

Nakuteua kwenye kinyang'anyiro cha Wenyeviti wa Vijana Kwa Mwaka 2023.
 
Africa haiwezekani na haifai kusema mtu hataki kuowa na kama hataki kuowa bora mara 1,000 asitake pia kuwa na mtoto kwa sababu hatuna mifumo stable kwa ajili ya kusaidia watoto wenye shida na wazazi.

Mfano kijana atakaposema hataki kuowa moja kwa moja ataiga uzungu wa kutaka kutafuta mwanamke amzalie watoto amlipe asiingiliane kwa namna yoyote na watoto sasa ikitokea huyu kijana hayupo hawa watoto watakaa ktk mazingira gani?ndugu wengi hatupendani sometimes unakuta ndugu wengine hata watoto wao kuwatunza hawawezi utegemee watoto wanaoranda randa mitaani hawataongezeka?

Na serikali zetu hizi za kiafrika hazina mifumo ya kutunza watoto wasiokuwa na wazazi hii si hatari sana maana wanaosema kuowa hawataki siyo matajiri useme wataacha mali za kuwasaidia watoto in case of anything ni maskini wengine watakufa hawana hata nguo ya pili si hawa watoto wataishia kwenye uchokoraa na wizi mtaani pamoja na ushoga kuongezeka!!!

Vijana acheni kuiga upumbavu wa wazungu siyo kila kitu ni cha kuiga ukitaka kuwa na kizazi bora kama ulivyo wewe ndoa huwezi kuikwepa.
Unaweza ukawa na watoto ukawatunza wao na Mama yao bila ya ndoa za makaratasi na sheria.
 
"Fikra zako zimehisi.." hizo ni hisia zako! Hatuishi kwa hisia.
Labda kama umekufa ila ukiwa bado unavuta hii pumzi ninayovuta mimi jua huwezi kuikwepa "hisia"

 Hata huyo anayesema kuowa hakufai nae amehisi kuna hali ya hatari ktk hiyo taasisi so utaona bado kila mtu anaishi ktk hisia.
 
Usigeneralize. Tuko malegend tulioolewa kimya kimya braza. Tulitoka kanisani, tukaenda restaurant opposite na mlimani. Nikiwa nimevaa gauni la 35k la kariakoo. Tukala sisi na wazazi wetu pande mbili na baadhi ya mashem, wifi na dada kwa upande wangu. No photoshoot, no mc, no champagne, no cake. Kibingwa..af fresh. Na tunadunda tu. Kiroho safi.
 
Mimi nadhani labda wanataka waolewe wao!!!

Eeh,maana kama mtu ulitokana na ndoa na umekulia kwenye familia ukiwaona wazazi wako pamoja mpaka wamezeeka kinachokufanya usiowe ni nini?

Exactly ulichokisema mkuu
 
Mkuu kwenye Pepsi baridi bill juu yangu…. Hawa wadada siku hizi wana tamaa sana na hawana shukrani….
 
Africa haiwezekani na haifai kusema mtu hataki kuowa na kama hataki kuowa bora mara 1,000 asitake pia kuwa na mtoto kwa sababu hatuna mifumo stable kwa ajili ya kusaidia watoto wenye shida na wazazi.

Mfano kijana atakaposema hataki kuowa moja kwa moja ataiga uzungu wa kutaka kutafuta mwanamke amzalie watoto amlipe asiingiliane kwa namna yoyote na watoto sasa ikitokea huyu kijana hayupo hawa watoto watakaa ktk mazingira gani?ndugu wengi hatupendani sometimes unakuta ndugu wengine hata watoto wao kuwatunza hawawezi utegemee watoto wanaoranda randa mitaani hawataongezeka?

Na serikali zetu hizi za kiafrika hazina mifumo ya kutunza watoto wasiokuwa na wazazi hii si hatari sana maana wanaosema kuowa hawataki siyo matajiri useme wataacha mali za kuwasaidia watoto in case of anything ni maskini wengine watakufa hawana hata nguo ya pili si hawa watoto wataishia kwenye uchokoraa na wizi mtaani pamoja na ushoga kuongezeka!!!

Vijana acheni kuiga upumbavu wa wazungu siyo kila kitu ni cha kuiga ukitaka kuwa na kizazi bora kama ulivyo wewe ndoa huwezi kuikwepa.
Unajifanya kuwahi kuoa mke anakuchapa stress unawahi kufa kabla hata ya 50 years
 
Ni yule niliyemshauri mda mwingi tukiwa sehemu za starehe kitambaa cheupe tukipata K vant kubwa na Windhoek za Kopo baridi, mda mwingi tuliwaza pesa na kula bata ila mwenzangu akawa busy kukusanya pesa za Mahali. Nilikwambia hiyo million mbili bora twende kidimbwi tuagize kuku wa kuchoma na jack Daniel kubwa ila akasema mimi sio mtu mzuri namfudisha upumbavu

Vijana nawasihi mjipende wenyewe kwanza, hawa wanawake siku hizi wamekuwa tooo cheap Sasa unaowa ili iweje. Unaleta stress za ajabu tu nakujaza majukumu ndani ya Familia unakosa hata pesa ya kula kitumbua barabarani mda wote unawaza bajeti ya kula na kusomesha watoto

Sasa kwakumalizia jamaa kaja kwangu Jana usiku analia anaomba msaada mke wake kamtoroka alimtumia meseji akasema hawezi ishi na JITU ambalo halina pesa. Ona Sasa haya mambo, kabla ya sasa jamaa alikuwa yupo vzr ila mke ndokamfilisi. Jamaa kawajengea wakwe zake ila wazazi wake wa kumzaa wanaishi kwenye banda la nyasi na kuta la Mavi ya punda. Mke wake waliyeachana saizi yupo Kwa wazazi wake anakaa kwenye mjengo mpyaa ambao jamaa aliwajengea

Finally, jamaa yupo hapa kwangu mda huu Hana hata pakulala mke ameuza kila kitu kodi ya nyumba anadaiwa. Linakoroma tu sijui nilipake mafuta [emoji30][emoji31]🥱
 
Back
Top Bottom