Sheria ya Ndoa na kufunga Ndoa ni mfumo wa wanadamu sio MUNGU wala SHETANI kwa hio usichanganye mada kwamba wanaopinga Ndoa basi wanapingana na MUNGU, wanadamu wameunda hio sheria ya Ndoa sio MUNGU wala SHETANI alieunda SHERIA YA NDOA amka kutoka kwenye huo usingizi wa kifo,
Sheria ya Ndoa ni mbovu kuwahi kutokea ni Ina mambo yaliyopitwa na wakati inabidi ifanyiwe maboresho (updates), hicho ndicho kitu watu wanakizungumzia haswa wakihitaji sheria ya Ndoa ifanyiwe marekebisho maana kwa jinsi ilivyo ni sawa na sheria ambayo haitendi haki ni sheria ambayo bias zaidi kwa kuegemea upande mmoja tu, jaribu kuelewa kwanza ndio utoe maelezo
Soma mdogo mdogo.. utaelewa
Mafarisayo kadhaa walimjia, wakamwuliza kwa kumtega, “Je, ni halali mume kumpa talaka mkewe kwa kisa chochote?”
Yesu akawajibu, “Je, hamkusoma katika Maandiko Matakatifu kwamba Mungu aliyemuumba mtu tangu mwanzo alimfanya mwanamume na mwanamke, na akasema: ‘Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja?’
Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asikitenganishe.”
Lakini wao wakamwuliza, “Kwa nini basi, Mose alituagiza mwanamke apewe hati ya talaka na kuachwa?”
Yesu akawajibu, “Mose aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu.
Lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo. Basi nawaambieni, yeyote atakayemwacha mke wake isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, akaoa mke mwingine, anazini.”
Wanafunzi wake wakamwambia, “Ikiwa mambo ya mume na mkewe ni hivyo, ni afadhali kutooa kabisa.”
Yesu akawaambia, “Si wote wanaoweza kulipokea fundisho hili, isipokuwa tu wale waliojaliwa na Mungu.
Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: Wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee.”
Yesu anawabariki watoto wadogo