Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Unachosema ni kweli, ndoa nyingi zinaingia zikiwa na misingi mibovu..

Ila haina maana tupinge ndoa na kuhamasisha.

Watu wazuri wapo na wabaya wapo.. nipo mkoa flani katika wilaya flani hakuna uchafu na ujaribifu kama wa huko mjini.. na aanafata kila taratibu..

Ndoa inabaki kuwa ni kusudi la Mungu na ni njema.. changamoto zake haifanyi tuanzishe kampeni ya kupinga..

Kuna mambo mengi mabaya yana athari sana kwa watu mbona hatuyapingi wazi wazi.. ila why ndoa ? Kuna ajenda mbaya hapo unakataa ndoa then ije nini ?
Hatupingi ndoa ila tunatumia haki yetu ya Kimaandiko ya kutofunga ndoa
 
Bado... Watakuja wasio na dini wala kuamini chochote kukupinga😂😂😂
Kupinga na kuto amini kwao, haifanyi neno la Mungu kuwa weak.. mwisho wa siku kila mtu atavuna alichopanda.. Tupo nyakati z mwisho hizi.. neno linasema "Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako."
 
Daah nyakati za mwsho tena
 
Maandiko yepi mnayotumia mkuu wangu ? Tuwekee na sie twaweza jifunza kitu
1. Wakoritnho 7:37–40

37 Lakini kama mwanamume ameshaamua moyoni mwake kuto kuoa bila kulazimishwa na mtu; kama anaweza kujitawala kabisa, basi anafanya vyema kutokumuoa mchumba wake.

38 Kwa hiyo mwana mume anayeamua kumuoa mchumba wake anafanya vizuri, lakini yule anayeamua kutokumuoa anafanya vizuri zaidi.

39 Mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mume wake maadamu anaishi. Kama mumewe akifa, basi mwanamke huyo yuko huru kuolewa na mume mwingine ampendaye, ila iwe katika Bwana.

40 Lakini kwa upande wangu naona kuwa angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo.
 
Mm nakataa ndoa ila nabinti zangu wawil mapacha nawapenda mno ,naomba nisihusishwe na chuki ya wanawake mkuu.
Nina wasiwasi na hilo, sababu nina uhakika hauna uhusiano mzuri na mama yako,lol...ungekua na foundation nzuri ya wazazi particularly mama usingekataa ndoa....hivyo kusema unapenda mabinti zako nina wasiwasi sana..
 
1. Wakoritnho 7:37–40

37 Lakini kama mwanamume ameshaamua moyoni mwake kuto kuoa bila kulazimishwa na mtu; kama anaweza kujitawala kabisa, basi anafanya vyema kutokumuoa mchumba wake.

38 Kwa hiyo mwana mume anayeamua kumuoa mchumba wake anafanya vizuri, lakini yule anayeamua kutokumuoa anafanya vizuri zaidi.

39 Mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mume wake maadamu anaishi. Kama mumewe akifa, basi mwanamke huyo yuko huru kuolewa na mume mwingine ampendaye, ila iwe katika Bwana.

40 Lakini kwa upande wangu naona kuwa angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo.
1 Wakorintho 7:9

Hata hivyo, kama mtu hawezi kujizuia, basi na aoe; maana ni afadhali zaidi kuoa kuliko kuwaka tamaa.

Je? Unaweza jizuia usifanye uasherati
 
Back
Top Bottom