1. Wakoritnho 7:37–40
37 Lakini kama mwanamume ameshaamua moyoni mwake kuto kuoa bila kulazimishwa na mtu; kama anaweza kujitawala kabisa, basi anafanya vyema kutokumuoa mchumba wake.
38 Kwa hiyo mwana mume anayeamua kumuoa mchumba wake anafanya vizuri, lakini yule anayeamua kutokumuoa anafanya vizuri zaidi.
39 Mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mume wake maadamu anaishi. Kama mumewe akifa, basi mwanamke huyo yuko huru kuolewa na mume mwingine ampendaye, ila iwe katika Bwana.
40 Lakini kwa upande wangu naona kuwa angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo.