Mimi nipo kwenye ndoa na ninapambana bila kuchoka nichomoke kwenye ndoa kutokana na mambo ya ndani ya ndoa yalivyo.
Nilikuwa kimya nasoma maoni ya wanaokataa ndoa na wanaoipa chapuo ndoa.
Hoja yangu imebase kwenye mantiki zolizowekwa na sheria. Sheria ya ndoa ya Tanzania inapeleka hasara kubwa kwa wanaume na kumfaidisha sana mwanamke.
- Sheria ya ndoa inamtaka mwanaume kumtunza mke wakati wote wawapo kwenye ndoa
- Sheria ya ndoa inammilikisha mwanamke mali za mwanaume za ndani ya ndoa. Hapa maana yake jasho la mwanaume linagawanywa kuwa jasho la wanandoa wote wakati wa ndoa
- Endapo wakaamua kutalikiana, mwanaume hupewa gawio lisiloakisi jasho lake na mwanamke hupata gawiwo zaidi ya jasho lake.
- Sheria ya ndoa haimpi jukumu mwanamke ndani ya ndoa bali majukumu.yote anapewa.mwanamume
KUna vitu vingi havijakaa sawa kwenye ndoa ambavyo vinawasababisha vijana kuwa bold and clear kukataa ndoa.
Tuzungumze maboresho ya sheria ya ndoa ndipo vijana waanze kurejea ndoani.
Mie.mwenyewe nataka leo kesho.kutemana na mwanandoa mwenzangu..