Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Ndoa changamoto sana, mfano mdogo tu tu kwenye ndoa kabati langu kubwa kidogo milango 3 lote limejaa nguo zake tu, zangu saivi nimeweka kwenye jaba.
😂😂😂😂 Uwii nimecheka, kwangu vice versa is true. Mimi ni minimalist, kuna muda nakusanya nguo nagawa nabaki nazo hata pea 15 nguo zangu chache japo quality, Za mwenzangu nyingi balaa japo na zenyewe ni kali sana .

Sijajua na mimi nianze kulalamika?
 
Ndoa changamoto sana, mfano mdogo tu tu kwenye ndoa kabati langu kubwa kidogo milango 3 lote limejaa nguo zake tu, zangu saivi nimeweka kwenye jaba.
🤣🤣🤣🤣🤣 nimecheka kwa nguvu
Jamani pole.. hiyo kesi ni ya wengi.. sijui ni tunanunua nguo kwa tamaa!! Sijui ni ile kanguo kakikutoa basi kanakaa karibu karibu hapo kabatini

Unakuta una nguo mpk zingine unazisahau… Kuna gauni niliinunua dec mwaka jana ktk shopping za sikukuu, nimekuja kuivaa mwaka huu unavyoelekea ukingoni.
 
Dah! mpaka kichwa kinauma, yaani yeye tena hana habari, ndo kwanza anauchapa usingiz wa pono. ndoa? ndoa? ndoa? hapana, natakiwa kufanya maamuzi magumu.
Kuna ujinga hua nauona sanaa...
Yaani mume anaamka saa 10 alfajiri kwenda kutafuta mkate wa mtu ambae akibaki nyumbani anaenda kutembeza mbumbusu kwa bodaboda wake..!!!

Ndoa kama NDOA.

#YNWA
 
Yalikuwepo, yapo ,yatakuwepo. Hakuna jipya kila mmoja ashinde mechi zake
Punguza kujipa moyo, hata Nyerere aliuchoka ukoloni ambao wengine waliishi nao miaka mingi akaamua KUPAMBANIA UHURU WAKE na wa WENGINE.

Usisahau, Nyerere alizaliwa na akaukuta ukoloni ila ALIUKATAA akachukua HATUA.

#YNWA
 
Back
Top Bottom