MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Ngoja nifuatilie kimyakimya labda nitajifunza kitu, vinginevyo kama sielewi vile!
 
kuna mambo luther hakuwa sahihi. ila mengi alikuwa sahihi. kuna vitabu alikuwa sahihi kutoa na vingine hakuwa sahihi. hatupaswi kuangalia in black and white.
Nataka uniambie mamlaka hayo yakutoa vitabu kwenye Biblia ukiyokamilika, yenye pumzi ya Mungu alipata mamlaka hayo wapi...???
 
kwanza, Yesu hakuwa binadamu
Pili, biblia inatumika kama nyenzo ya ushahidi kuwa alifufuka na sasa yupo hai.
Tatu, Nauliza ni wapi biblia imeeleza kwamba Maria alipaa na yupo hai mpaka sasa?
Nne, ni wapi biblia imetutaka tumtumie Mariam kama muombezi wetu?
 
nakuunga mkono mkuu.siku wakiufahamu ukweli watakuwa huru kama mimi ambavyo niko huru sasa.i hope waujue ukweli before its too late.
 
Umesahau na yale makabidhiano ya Yesu na Yohana pale msalabani..."Mama tazama mwanao na Yohana tazama mamaako" halafu watafakari kazi ya mama nini kama sio ku harmonize kati ya baba na Mtoto.
 
Samahani mkuu, naomba nipe andiko linalosema Mungu aliruhusu matumizi ya ubani, please
 
Unajua maana ya brethren na brother, unaweza kuzitofautisha na maneno sibling na blood brother......nway Amini unacho Amini...atlast tubaki watanzania.
 
Samahani mkuu, naomba nipe andiko linalosema Mungu aliruhusu matumizi ya ubani, please
Soma kitabu cha zaburi pale Daudi anapomtolea Mungu Sadaka kisha kusema "Sala yangu na Ipae mbele zako kama moshi wa Ubani..."

Pia ukisoma Kitabu cha Ufunuo utaona..
"Malaika Mtakatifu kasimama kando ya Altare/madhabahu akiwa ameshika mkononi chetezo cha dhahabu..."
 
Tunaziombea roho za marehemu wote zipate rehema kwa Mungu zipumzike kwa amani.....
Asee!! asa kuna maana gani ya nyie kumuita Yesu mwokozi wenu??? kama mnauwezo wa kuombea hadi marehemu akasehewa??? Huyo marehemu wakati wakiwa wazima hawakusikia injili ya wokovu na wakasadiki?? Mnapotezea muda someni biblia vzuri jaman,Mtu akishafuka ni hukumu tu,huwezi kubatilisha shauri la Mungu juu ya mwanadamu aliekufa eti asamehewe?? Wokovu ni njia pekee ya sisi kuungana na Yesu kristo na kutengeneza njia zetu na kutubu na kumpokea kuwa Bwana na mokozi wa maisha yetu,hivyo mtu hawezi kwenda mbinguni bila kupitia kwake!! na je unapitiaje kwake bila wokovu??? Mtu akifa hakuna kutubu tena huko ni hukumu tu,ndo maana mkristo unatakiwa kutengeneza njia zako ukiwa hai!! maana ukifa na yako yamekwisha huko ni hukumu tu, Wakatoliki jaman mtahukumiwa kwa neno,mnaombeaje wafu wapate rehema wao wakati wakiwa wazima walishindwa kuomba toba na kutubu??? inamaana hawakulisikia neno??? Kiukwl ni mara 1000 uwe tu mpagani kuliko kuwa mfuasi wa kristo usiyeyajua maandiko kama ww ndugu.!!Mungu wa mbingu na nchi akupe neema ya kuitambua kweli nayo ikuweke huru na vifungo vya fikra.
 
Usililolijua ni sawa na ucku wa giza
 
Wewe ndio wa kusoma Biblia vizuri....Biblia ipo wazi kabisa...Marehemu wanaombewa vizuri kabisa...Kitabu cha Wamakabayo kipo wazi mbona
Anhaa ok nafkiri Biblia yenu ni tofauti na yetu tunayoitumia hii ya vitabu 66,anyway kumbe yapo maandiko yanayowa guide?? Basi mkuuu ngoja niishie hapo kwa leo
 
Nataka uniambie mamlaka hayo yakutoa vitabu kwenye Biblia ukiyokamilika, yenye pumzi ya Mungu alipata mamlaka hayo wapi...???
hayo ni makosa yake binafsi. ila kuna mengi alifanya vizuri sana. hata watumishi wa Mungu kama Musa na Daudi walifanya makosa.
 
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao ni darasa la saba wanawapotosha, hawaijui biblia
Ushasema walikuwa harusini na mama na mwanae walikuwepo, walipomuomba mama amwombe mwanae ni kawaida kwa kimuono wa kibinadamu.
Je ni wapi katika Biblia tunaambiwa tukitaka kumuomba Mungu basi tupitie kwa mama maria?
 
Ingekuwa vyema ungeweka mistari ya Biblia inayoback up hicho ulichoandika.
 
hayo ni makosa yake binafsi. ila kuna mengi alifanya vizuri sana. hata watumishi wa Mungu kama Musa na Daudi walifanya makosa.
Kama ni yake binafsi kwanini Waprotestant wote mna biblia yenye vitabu 66...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…