MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Anhaa ok nafkiri Biblia yenu ni tofauti na yetu tunayoitumia hii ya vitabu 66,anyway kumbe yapo maandiko yanayowa guide?? Basi mkuuu ngoja niishie hapo kwa leo

Ndio maana mada inauliza, nini kilimpelekea Martin Luther kupunguza vitabu 7 vya Agano la Kale . ??
 
Nimeisoma na hakuna mahali nimeona tukiambiwa tukitaka kumuomba Mungu basi tupitie kwa maria, wala sijaona mahali ambapo maria alipaa kwenda mbinguni.

Kaburi la Yesu linajulikana, makaburi ya mitume yote yapo, umeshawahi kusikia mahali kaburi la Mama Wa Yesu lilipo...??

Ifunuo wa Yohana

"Ishara kubwa imeonekana mbinguni, mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake, na taji ya nyote 12 juu ya kichwa chake"
 
Endelea kusoma zaidi utaelewa kilichokuwa kinaendelea, ishara ilionekana mbinguni lkn matukio yalendelea duniani, kumbuka mwanamke alipewa mbawa akapaa hadi nyikani ambako shetani alijaribu kumdhuru lakini hakufanikiwa, je ni nini kilitokea huko nyikani?

Na kama kuna mahali panaonyesha alipaa kwenda mbinguni, au mahali panapitutaka tumuombe Mungu kupitia maraia hebu weka hapa.

Maana twapaswa kumuomba kupitia Mwana kwa msaada wa roho mtakatifu(utatu mtakatifu unakamilika)
Huo unne mtakatifu umeainishwa wapi?
 
 
Habali wana jf .. Hivi wa kathoriki mmeenda wapi pigo moja tu nanyi mkapotea.. Nilitaka nidondoshe jabari lingine lakni mmekimba sawa kwavile mmesalimu amli nami nakaa kimya
 
Habali wana jf .. Hivi wa kathoriki mmeenda wapi pigo moja tu nanyi mkapotea.. Nilitaka nidondoshe jabari lingine lakni mmekimba sawa kwavile mmesalimu amli nami nakaa kimya
Ukijibizana na kichaa ni wazi utakuwa kichaa....

Kajifunze kuandika kwanza pamoja na semantiiki ya lugha..
 
Hakuna haja yakujifunza wewe lete maandiko mm nimetoa maandiko nawewe lete maandiko aja asila huunimuchezo usiyo na hasila
 
Nimeisoma na hakuna mahali nimeona tukiambiwa tukitaka kumuomba Mungu basi tupitie kwa maria, wala sijaona mahali ambapo maria alipaa kwenda mbinguni.

Unaamini kwamba bikira Maria ni mbarikiwa?
unaamini kwamba amejaa Neema?
Unaamini kwamba Bikira Maria ni Mama wa Mungu?
Nijibu hayo kwanza kabla sijaendelea.
 
 
Nimeisoma na hakuna mahali nimeona tukiambiwa tukitaka kumuomba Mungu basi tupitie kwa maria, wala sijaona mahali ambapo maria alipaa kwenda mbinguni.
Unajua mkuu shida ya wa rc ni kwamba wao ni Wafia dini! Kamwe huwez kumshauri m rc hasa alietukuka yaani wao huwa wanapinga walioambiwa na padri wao waz waz hata kama maandiko yanakataza lakini as long as dini yao imesema baasi maandiko hayana nafasi,Kwhyo unaweza jikuta unauliza hoja za msingi lakini ukakosa majibu sahihi kutoka kwao kwa sababu wengi wao ni wafia dini,Lakini ashukuriwe Mungu wa mbingu na nchi hata mtume paulo alituambia mtu yoyote akija hata awe malaika wa nuru kutoka mbinguni lakini akitufundisha neno lolote ambalo yeye paulo hajafundisha basi huyo na alaaniwe kwa maana hiyo,Hata kama ni dini yoyote ile kama haisimamii misingi ya BIBLIA hio sio dini,maana dini ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu na Mungu atatafutwaje ikiwa neno lake lenyewe linapindishwa??? Jaman wakristo wenzangu Tukae na tudumu katika Neno tuache kufatisha dini kwn hakuna mahali pameandikwa dini zetu ndo zitatupelek mbinguni isipokuwa ni utii na unyofu wa moyo na kukaa katika neno,kwn neno ndo litakalohukumu na wala hutahukumiwa kwa sababu ulikuwa dini flan ama la!
 
kiukweli umekuwa mkristo usie na faida.
kuabudu miungu na kuvunja amri za Mungu ndiko kunakutesa mpaka umkosoe martini luther.
kajipange upya na hoja zako zenye kukinzana na imani ya ukristo.
Hapa ungeonekana wa maana endapo ungetuonesha kiundani alipoenda kinyume na maandiko au kuvunja amri
 
.
*uandishi wako unaonyesha kua huijui historia ya kanisa,,,
kwa mfano huzungumzii sala kwa bikira maria na cheo chake cha umalkia, ubatizo,,, imani, na neno..
Zungumzia wewe Kama unajua
 
wenzangu Tukae na tudumu katika Neno tuache kufatisha dini kwn hakuna mahali pameandikwa dini zetu ndo zitatupelek mbinguni isipokuwa ni utii na unyofu wa
Nipe sababu zs Martin Luther kuondoa vitabu 7 vya Agano la kale...

Nipe sababu za Martin Luther kutaka kuondoa vitabu vya Ufunuo, Yakobo na Waebrania....

Jikite kwenye mada...
 
Maria ni Mtakatifu kama Watakatifu wengine...Na Watakatifu wana kazi ya kutuombea....Wao ni Kanisa Shindi huko mbinguni..

Soma Ufunuo 5:8 uone maombi ya Watakatifu na Wale wazee 24 mbele ya Kiti cha Mwana Kondoo..
Soma 14.6 yohana mt. Kabla hujacomment mkuu.
 
nani kaviandika hivyo vitabu vilivyoondolewa? Hata mashuleni vimeondolewa baadhi ya vitabu kwa literature na riwaya vilivyokuwa vikitumika huko nyuma kama vile elfu lela ulela, hekaya za abnwas, tende hogo, kuli, n.k kutokana na sababu mbalimbali za wakati. Hata Luther kuondoa baadhi ya vitabu vya riwaya kwenye bibilia ni sawa kabisa. Hata wanawake hivi sasa wako mbioni kuzifuta baadhi ya riwaya za kwenye bibilia zinazowakandamiza, kuwabeza na kuwatweza kama zile zinazosema mwanaume ni kichwa cha nyumba, mwanamke kazi yake ni kuzaa kwa uchungu tu basi, mwanamke mpumbavu ataivunja nyumba yake mwenyewe, mwanamke alimdanganya Adam, na mwanamke katwaliwa kwenye ubavu wa mwanaume. Kwa mwanamke wa sasa wa 50% kwa 50% hizi ni riwaya tu zisizotekelezeka kamwe katika zama hizi, akitokea mtu atakayezifuta kwenye bibilia watashangalia sana. Hicho ndiko alichokifanya Padre Luther, na bado kufuta kutaendelea mariwaya yale yanayotumika kuwafilisi waumini kwa michango ya kilaghai makanisani kwa manufaa ya wajanja wachache wasiopenda kufanyakazi iko siku yatafutwa kwenye bibilia tu, ni swala la wakati tu.
 
Huwezi kuliona wanawake enzi hizo hawakuwa na heshima kwenye jamii, hivyo kabuli lake halikuwa kipaumbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…