MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Mtu anapinga Bikira Maria kutuombea, lakini akiambiwa aombewe na AKINA MWINGIRA, KAKOBE, RWAKATALE etc etc faster wanaenda... siwaelewi.
 
Kwenye harusi ya kana wale watu walimwambia Bikira Maria afanye nn!? Na pale msalabani Yesu alimwambiaje yule mwanafunzi wake anayempenda!? Acha akili za kushikiwa ww.
 
mnanishangaza sana na kunistua kwa kweli, hivo vitabu mnavodai vilipunguzwa mara viliongezwa (yani kama vipimo vya mchele), si vyote mnadai viliandikwa na manabii na mitume wa Mungu au?

sasa huko kupunguza mara kupunguzwa ni kwambo hao waliandika kwa msaada wa Mungu(according to christians) walikosea au vipi?

Naona mnataka mniaminishe kuwa biblia ni mchakato wa binadam flan waliokuwa na mpango wa kupga dili tu na kuzishika brain zetu aisee.....!
 
Ehhe! Hebu niambie anarudi lini...?


Maana biblia yangu inaniambia hakuna ajuaye siku wa saa ya kuja mwana wa Adamu....
Yesu alisema, "hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu lile lilinenwa na nabii Daniel (asomaye na afahamu)... Paulo anasema " siku ya Bwana haiji hadi afunuliwe yule asi, ajiinuaye nafsi yake kama Mungu ambaye Bwana Yesu atamuua kwa pumzi yake". 2 wathesalonike 2:1-5. Hilo chukizo la uharibifu kama alivyonena Daniel ni Papa. Paulo aliiona nguvu hii pia ikitenda kazi kuanzia kwnye dola ya kirumi na kisha kanisa la rumi.Huyo asi muda si mrefu atafunuliwa pale atakapoungana na wafalme wa dunia hii ili kushinikiza ibada ya uongo dhidi ya Ibada ya Mungu. Hapo Michael atasimama upande wa watu wa Mungu Daniel 12:1. Huyo asi na wafuasi wake wataangamizwa na wateule watatwaliwa Mbinguni. Kwa mujibu wa Biblia siku hizo haziko mbali.
 

Well said!!

Dini uliyo nayo leo ni urithi toka kwa jamii uliyokulia au inayokuzunguka. Hii ni pamoja na mila na desturi za kwenu.

Mara nyingi huwa binadamu anakubali na kutukuza values alizikuzwa nazo na mara nyingine yuko tayari hata kufa kwa ajili ya kuzilinda.

Wewe ni Muislam su Mkristo kwa sababu jamii inayokuzunguka ilikuaminisha katika Uislam ama Ukristo.

Yule ni myahudi ' judaism' kwa vile kukulia Israel/uyahudi.

Yule mhindu au dini za wachina na wajapani nk.

Kuponda dini, mila imani ya mwenzio si kuwa tu inajenga chuki na dharau miongoni mwa jamii, bali pia inasababisha unayejaribu kumuonyesha ubaya wa dini /mila au imani yake, aone ubaya wa dini yako wewe na azidi kuichukia dini yako na wewe mwenyewe!! Badala ya yeye kufuata unayoamini unazidi kumfukuza mbali zaidi.

Hivyo kuanika masuala ya imani mbalimbali hapa ambazo watu mbalimbali wanaziabudu sio jambo la mbolea!!

Ni upungufu wa busara!!

Amini ambacho wewe na akili yako na roho yako uneridhika nacho. Period.


Hakuna kitu kama Univesal faith au Universal religion!!!

Kwa akili za binadamu hakuna imani ambayo inakubalika au itakayokubalika kwa wote

Amani iwe kwenu!!
 
Umbumbumbu tu wa maandiko ndio unakutesa
 
Alafu hawa wasabato wameharibu Uzi kabisa, mtoa Uzi kata rufaa kwa mods maana wasabato wameshatutoa nje ya mada
 
Hii thread inahusu Padre Luther kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ambayo ndio mnayotumia Waprotestant ....tuambieni kwanini aliviondoa? Kwanini alitaka kuondoa hadi kitabu cha ufunuo hadi mwenzake Calvin alipoingilia kati (maana yake leo waprotestant msingekuwa na kitabu cha ufunuo kwenye Biblia yenu kama si juhudi za Calvin) ....mada za Bikira Maria, tunaabudu sanamu n.k fungueni uzi wake maana mshaharibu mada ....kama hujui historia waachie theologians waje kujibu hoja zetu .....nyie mliokariri vifungu vya Biblia hamuwezi kuja na majibu hayo maana hapa tunaichambua historia ya hiyo Biblia tunayoitumia ili ujue hicho unachoamini kimepatikanaje .....vifungu haviwezi kujibu hapo ....
 
Maria ametoka wapi kwenye Uzi huu....?watakatifu wametoka wapi...?tujikite kwenye mada kama unataka ya Maria anzisha Uzi alafu tutakuja.
 
Ukitaka kujua kuwa waroma ni vilaza wasomee mstari ya Biblia hawambulii kitu maana wao wamekaririshwa misale ya waumini tu. Hoja zozote zisizo pata support ya Biblia ni hoja mfu. Na si ajabu waroma kuabudu wafu na masanamu maana hawasomi Biblia.
 
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao ni darasa la saba wanawapotosha, hawaijui biblia
Kama wachungaji hawa wa kilokole ni darasa la saba ndiyo maana wanapotosha maandiko; Mtume Petro mnayemwita papa wa kwanza alikuwa darasa is ngapi?

Acha kuchanganya elimu yako ya darasani na uwezo wa Roho Mtakatifu.
 
Ukitaka kujua kuwa waroma ni vilaza wasomee mstari ya Biblia hawambulii kitu maana wao wamekaririshwa misale ya waumini tu. Hoja zozote zisizo pata support ya Biblia ni hoja mfu. Na si ajabu waroma kuabudu wafu na masanamu maana hawasomi Biblia.
Nani kakudanganya...?na biblia haitakiwi isomwe mstari kama mnavyofanya wasabato kisha mnaibuka na matusi,biblia ni fasihi ya hali ya juu mno,mf:Kitabu cha Daniel unatakiwa ujue historia ya kitabu,kwann Daniel anakuwa main character,ukifuatilia biblia za wakatoliki huwa kila kitabu kinaanza na historia ya kwamba kiliandikwa BD/AD na mtajwa kwenye kitabu husika ni kwann amekuwa main character na mahudhui ya kitabu kwa jamii za ulimwengu,ndg zanguni msisome biblia mstari tuu kisha mkaja na maswali na majibu,ebu angalieni babu yenu William Miller aliyetabiri ujio wa Yesu Kristo 1844....!hiyo aibu wasabato hamjawahi kuifuta na huku mkipambana na kanisa mama,kanisa lililoachwa na Yesu mwenyewe Roman Catholic.
 

Rejea hapo kwenye bold.Mimi naamini Biblia moja tu yenye pumzi ya Mungu 2 Timotheo 3:16-17. Hizo za waroma baki nazo ninyi huko mwendelee kudanganyana.
 
Baada ya kusoma nyuzi zote hapo juu, sema maneno haya kwa dhati:

"Mungu baba, nakuja mbele zako, Mimi ni mwenye dhambi. Natubu dhambi zangu zote, kwa maana ya kuziacha kabisa. Naomba rehema na neema zako Mungu zinifunike. Sitaki dhambi tena kuanzia sasa. Bwana Yesu, nisafishe kwa damu yako iliyomwagika msalabani. Asante kwa kunisafisha n.a. kunisamehe dhambi zangu. Ni katika jina la Yesu Kristo ninaomba. Ameni."

Asante kwa kusoma sala hii kwa dhati; Mungu amekusamehe dhambi zako zote. Na sasa wewe ni kiumbe kipya na umeokoka.
 
Rejea hapo kwenye bold.Mimi naamini Biblia moja tu yenye pumzi ya Mungu 2 Timotheo 3:16-17. Hizo za waroma baki nazo ninyi huko mwendelee kudanganyana.
Ndg yangu cjui umenipata concept yangu....?biblia imeandikwa na Mungu kupitia watu wake hata hiyo barua ya pili ya kichungaji kutoka kwa Paul kwenda kwa Timotheo mstari 3:16-17 ujaweza kuutumia vzuri,mm namaanisha biblia ya Kikatoliki yenye vitabu 73 imejaribu kumrahisishia msomaji aweze kupata mahudhui kirahisi zaidi kwani wanaanza na mhutasari kwenye kila kitabu kisha unaanza kusoma kitabu husika,NB:Unajua historia ya kuandikwa biblia...?Je unajua biblia ya kwanza iliandikwa kwa lugha gani...?Kwann Leo waprotestant biblia yao INA vitabu 66....?Kwann Leo wayahudi biblia yao INA vitabu 39....? na kwann Leo Wakatoliki biblia yao INA vitabu 73....?ndg hv ni vtu muhimu sana kabla ujaanza kunukulu barua za Paul kwa Timotheo.
 
Hapana bana. Kulikuwa na makanisa mengi toka mwanzo. Na juhudi za watu kuwa na makanisa yao zilikuwepo. Lakini ukatoliki ilikuwa ni dini ya dola. Hivyo kanisa lilizima juhudi hizo.

Sehemu ambazo zilikuwa nje utawala wa kirumi kama vile Ethiopia, India na Uarabuni zilifuata ukristo uliokuwa tofauti na Ulaya.

Na pale jamii za Ulaya zilipoanza kutengenisha kanisa na serikali, makanisa tofauti yalianza kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…