MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?


Nikufahamishe tu ndugu yangu, Kanisa la wasabato yaani SDA nguzo yao kuu ipo katika Utatu Mtakatifu, yaani Mungu Baba, MUngu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Yaani nafsi hizi tatu ndizo zinakamilisha Uungu. Hii ni nguzo kuu katika misingi ya Imani ya Waadvenstista wa Sabato (SDA). Hao walioko kwenye mjadala labda ni watu wengine ulizia vizuri.
 

Wewe ni mgeni kwenye hilo dhehebu, kwa taarifa yako miongoni mwa vitu vilivyoleta debate kubwa sana ndani ya Usabato ni hiyo habari ya Utatu, kama wewe unaamini hilo naona umeongoka na utaijua kweli soon

Pitia hizi nyuzi kwa moyo mkunjufu, utaona imani yako ya Kisabato kuhusu trinity na utakuja kugundua kuwa nyie wasabato mnaamini katika Tritheism na sio Trinity,

CultOrChristian.com - Does Seventh-day Adventism Teach the Trinity?

CC: Otorong'ong'o , jiwe la majiwe
 
SDA nguzo yao kuu ipo katika Utatu Mtakatifu, yaani Mungu Baba, MUngu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu.
Labda nikupe taarifa ambayo hujawahi isikia toka umezaliwa....

Kwataarifa yako Bi Ellen G White hakuwahi kuamini Utatu Mtakatifu mpaka anakufa yule bibi....Utatu Mtakatifu kiuhakusia ukitumia maandiko Matakatifu ku-prove hutaweza maana maandiko hajaongelea kiundani na wazi...Ni Mapokeo Matakatifu tuu ndiyo yana support Utatu Mtakatifu..


Since Mama Ellen G White yeye alikuwa anadai biblia ni kila kitu (Sola Scriptura) aliona Utatu Mtakatifu nikufuata Mapokeo ya Kikatoliki..Hivyo alisema Utatu Mtakatifu ni Upagani na akaandika Manuscript...

Nini kilichotokea basi,
Fuatana nami ..

Kanisa la Kisabato halikuwa Kanisa ila kilikuwa ni kikundi cha Kiharakati cha Millerite....Mwaka 1863 wakati wakitaka kujulikana kama Kanisa Rasmi Walipata upinzani mkubwa huko Marekani...Walitengwa....Na sababu ya wao kutengwa ilikuwa ni Mafundisho ya Ellen G White kuhusu Utatu Mtakatifu....

Ellen G White mpaka anakufa alipinga Utatu Mtakatifu kwa nguvu zake zote.....

Kilichotokea ni GC kuficha nyaraka za Ellen G White kuhusu Utatu Mtakatifu...Ndipo Kikundi cha Kiharakati cha Kisabato kikakubaliwa kama kanisa mnamo mwaka 1863.,,.

Mtafaruku huu wa Utatu Mtakatifu, ndio ulimfanya Joseph Smith Kujiengua Usabatoni na kuanzisha Kanisa lake la Jehova Witness...

Jehova Witness kiuhalisia ndio Wanafuata mafundisho Halisi ya Mama Ellen G White, huku wakilishutumu kanisa la SDA kwa kukumbatia mafundisho potofu ya Utatu Mtakatifu ya Kikatoliki...

Sasa fukuto hilo limeanza tena huko Marekani....Watu wanataka kurudisha mafundisho halisi ya Bi Ellen G White..

Naomba nigotee hapa kwasasa..ila nitafunguka zaidi
 
Kitaja kuna kipindi niliwaambia Kanisa La SDA linatengeneza Biblia mpya...Itakayoitwa Clean Bible....Wasabato walinipinga ila ukweli umeshajulikana..

Hiyo link inaonesha wazi kuwa Wasabato Wanayo tayari Biblia mpya ambayo huko ndani kuna Manuscript za Ellen G White....

Time will tell...

Ndio maana kila siku nasema SDA ni Cult Religion
 
Hii ni nguzo kuu katika misingi ya Imani ya Waadvenstista wa Sabato (SDA). Hao walioko kwenye mjadala labda ni watu wengine ulizia vizuri.
Ushahidi tumeshakupa...

Fuatilia habari Za GC pamoja na kitu kinaitwa Ellen G White Estate..

Vipi The Clean Bible imeshawafikia tayari..?
 
Kitaja na Wasabato wengine naendelea kusoma hiyo link...Hakina natetemeka mwili mzima...Inatisha sana ...

Wasabato mnadiriki kubadili Biblia..?
 
Kweli mmeishiwa hoja, habari haina ushahidi wa Biblia nyie mnaimeza kama ilivyo.Si ajabu Biblia katika 2 Timotheo 4 :3,4.Paulo anasema " utakuja wakati, watu watakataa mafundisho ya kweli na kuzigeukia hadithi za uongo." Huu ni mfano mojawapo wa hizo hadithi za uongo.
 
Unajua sijakuelewa unaposema ushahidi wa Biblia...Hebu fungua hiyo link uone jinsi Biblia yenu mpya na ushahidi jinsi vinavyotolewa..

Najua, umestuka sana..hukutarajia haya..

Au unataka ni copy hayo yaliyoandikwa niyalete hapa..?

Masikini Wasabato..Daah
 
Mkuu, unazungumziaje hiyo Clean Bible..? Ni kweli au si kweli...? Unataka kuniambia GC ni mashetani...? EGW Estate ni mashetani..?

Maana ushahidi umepewa upo wazi....
Endelea kujipa moyo ndugu lakini kumbuka Hili kanisa ndio mfano wa mwanamke wa Ufunuo 12:1 Mwanamke aliyevikwa jua na taji ya nyota 12.Ni Bibiarusi wa Kristo Ufunui 19:7 kwa kuwa hili kanisa linatii amri za Mungu na imani ya Yesu Ufunuo 14:12 .Tofauti na yule kahaba wa Ufunuo 17:5. Kanisa lisilotii amri za Mungu, ushahidi upo wazi katika Biblia.Kanisa hili limediriki kubadili amri Daniel 7:25. Yesu aliita chukizo la uharibifu Mathayo 24:15. Petro aliita Babeli 1 Petro 5:13.Yohana aliita Babeli Mkuu, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. Kanisa hili limetabiriwa kufanya vita na watakatifu hata kuonekana "kuwashinda" kama wanavyodai sasa.Lakini, siku si nyingi Biblia inasema "Mikaeli atasimama upande wa watu wa Mungu". Daniel 12:1.Jiandae utasimama wapi?
 

Mkuu mbona umeng'ang'ania hapo kwenye hizo ngonjera za zamani za Ellen G White...??

Hiyo link umepitia..? Umeisoma..?

Mnadiriki kubadilisha Biblia..?
 
Endelea kujipa moyo ndugu lakini kumbuka Hili kanisa ndio mfano wa mwanamke wa Ufunuo 12:1 Mwanamke aliyevikwa jua na taji ya nyota
Unataka kusema huo mstari unamaanisha kanisa gani..?

Ndiyo mafundisho ya The Clean Bible yanavyo wafundisha..?
 
Mkuu mbona umeng'ang'ania hapo kwenye hizo ngonjera za zamani za Ellen G White...??

Hiyo link umepitia..? Umeisoma..?

Mnadiriki kubadilisha Biblia..?
Hiyo link nimeisoma ila imejaa upotoshaji mtupu hasa pale wanapolazimisha kuwa kanisa la SDA linapinga Uungu wa Roho Mtakatifu, na pia Mungu Mwana. huu ni uongo na upotoshaji wa wazi.Katika misingi ya imani ya SDA, utatu mtakatifu ni nguzo ya kwanza kabisa. Kwa kuwasaidia tu kwa kipindi chote cha robo hii ya mwaka kuanzia January hadi March kanisa linaendelea na muongozo wa kujifunza Biblia, mada kuu ni kuhusu Roho Mtakatifu.Leo kulikuwa na mjadala mzuri sana kituo cha Radio cha Morning Star FM 105:3.Kuhusu Uungu wa Roho Mtakatifu.Mjadala unaendelea kila jumatatu hadi alhamisi kuanzia saa 12 hadi saa 1 jioni.Ijumaa mjadala hufanyika kwa lugha ya kiingereza.Kwa Neema ya Yesu nategemea kushiriki mjadala siku ya ijumaa.Sogea karibu na redio upate mafundisho ya Mungu hasa nini Wasabato wanaamini kuhusu Mungu Roho Mtakatifu kwa mujibu wa Biblia. Karibuni sana, achaneni na hadithi za kutunga kwenye mitandao.
 

Kaka unajua hawa jamaa wako bize kuuchunguza Ukatoliki, lakini wanashindwa kujua kwao kuna matundu makubwa, na ndio maana nikwambia kwa kitendo chake cha kukiri utatu mtakatifu yeye keshajitoa kwenye Usabato, Sabato hawaamini Utatu mtakatifu unaoaminiwa na Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume, ila jamaa hajui imani yake inasimiamia wapi

Hiyo habari ya Biblia ya Kisabato nadhani ndio kaiona leo
 

Utatu mtakatifu ni miongoni mwa Nguzo kuu za Ukristo nguzo nyingine kuu ni fumbo la Imani kuwa Kristo Kristu alikufa, Kristu alifufuka na Kristu atakuja tena.
kama wewe unaamini hivyo (utatu mtakatifu) basi sawa, ila Wasabato hawaamini unachoamini wewe, inawezekana wewe haujawahi kusoma historia ya Kanisa lako kabisa, na pia nadhani haufuati mafundisho sahihi ya Mtume na Nabii bibi Ellen G White
 
Thibitisha kwa fungu la Biblia
Ellen G White sio mtu anayeweza kudhibitishwa kupitia biblia.....!ebu jaribu kutafuta technical questions ndg......according to situation inaonekana huna uelewa mpana kwenye hicho kikundi(SDA)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…